Mi mi
JF-Expert Member
- Jul 14, 2024
- 2,748
- 5,112
Hii demokrasia ya Korea kusini inashangaza kweli.
Baada ya Rais aliyetolewa madarakani kwa kura za wabunge za kutokuwa na imani naye bwana Yoon Suk Yeol baada ya kutoa amri ya nchi kuwa chini ya sheria za kijeshi ili kudhibiti wakomunisti wa China na Korea Kaskazini kujipenyeza katika siasa za Korea kusini kwa mujibu wake yeye.
Sasa mahakama huko Korea kusini ilitoa amri huyu bwana kukamatwa na kufunguliwa mashitaka na polisi wa huko SK wakapewa kibali cha kutekeleza amri hiyo ila jambo la kushangaza polisi zaidi ya 100 hapo jana walishindwa kutekeleza amri hiyo ya kumkamata huyu bwana baada kukutana na kizuizi cha wanajeshi walinzi wa huyu Rais katika makazi ya Rais pamoja na baadhi ya wafuasi wa huyu bwana.
Inakuwaje hawa maafisa wanaweka kizuizi kwa amri ya kimahakama kutekelezwa na polisi wa SK na wao kuendelea kumkingia kifua huyu former president hii demokrasia yao SK ni ya namna gani hii ? Inashangaza
N.b
Katika historia ya SK jeshi lina ushawishi mkubwa sana wa kimaamuzi na kubadili kabisa taswira nzima ya nchi kwa kipindi kirefu SK iliwahi kuishi chini ya amri za kijeshi.