Demu wa " UDOM" afungashiwa zawadi ya matambara machafu na mume wa mtu!

Kisingisa

Member
Joined
Jan 27, 2012
Posts
19
Reaction score
2
Nikiwa na my girlfriend asomaye udom week end hii nikiwa nimekwenda kumtembelea kama kawaida tukaanza kupiga story za hapa na pale tukiwa chuoni pale nikiangalia mazingira mazuri ya chuo kile mara akapita msichana mmoja na ndipo rafiki yanu huyo akaniambia,"Dear unamuona yule dada?nikamwambia ndiyo akaniambia ngoja nikupe story yake akaanza.............

Yule dada mwaka jana mwishoni alipatwa na bonge la skendo kifupi ni kuwa anatembea na mume wa mtu kwa muda mrefu na ana boyfriend wake,mwaka jana alipatwa na balaa la aina yake baada ya mke wa huyo mwanaume kugundua kuwa nantembea na mume wake, huyo dada alimpigia simu akamuuliza akajidai kukana na akamtukana sana yule dada na maneno mengi ya kejeli alimpa.

Baada ya hapo yeye aliendeleza mahusiano na huyo baba kama kawaida japokuwa baba huyo anaishi dar, ikatokea baba huyo anasafiri nje ya nchi binti si akaagiza mizawadi yakufa mtu, suti, pafyumu, digital camera, nguo za kutokea usiku na mazagazaga mengine.

Ikafika siku yule mbaba anarudi na kwa kuwa yule baba yupo dar na huyu msichana yupo dodoma akamuomba rafiki yake huyo msichanaaliyeko dar akampokelee mizigo toka kwa kale kababa kalikosafiri,rafiki yake akaenda na akapewa mizigi vizuri kufika nyumbani kufungua akakutana na matambara machafu hayafai kwa matumizi ya binadamu,eti pafyumu aliwekewa kopo la dawa ya mbu teh teh tehhhhh(akacheka sana na mimi ikabidi nimsapoti tu kwa kuchekakidogo).Baada ya muda akaamua kumjulisha yule rafiki yake yaliyojiri kuwa hakuna cha zawadi wala nini ni matambara machafu.................

Story ikaenea watu tukajua kuwa alikuwa anatembea na mume wa mtu sasa haieleweki ni kwa nini kuyo baba aliamua kumfanyia hivyo,hata hivyo huyu dada ana tamaa sana anataka kuishi maisha sio saizi yake yaani dear kila tukimuona hatuna mbavu tukikumbuka hiyo story! baada ya hiyo story nilipatwa na mawazo na hamu ya kwenda udom ikaniishia,nikajiuliza hivi sisi ambao hatujaoa ina maana tunakuja kuoa nyumba ndogo za watu?????

Maana kila msichana ana kadingi kanakompatia fedha na hii ni tamaa tu ya kuwa na vitu vizuri,sasa najiuliza huyo gf wangu je na yeye ana kababu kama hako ka kumhonga au alikuwa ananizuga kwa story ya mwenzie au aghhhhhhhhhhhhhhhh..............napata tabu nikarudi dar mdogo kama piriton.

.......jamani nikaribisheni ni mgeni leo nimeamua kujitosa kuwajulisha bachelors wenzangu kuwa tumeliwa .....bora niwe bachelor
 
story zingine basi waachieni wasimulie wasichana, dah inachosha kweli akisimulia mvulana.
 
Kuna maneno mengne yalipaswa kuachwa!

By the way, story imekosa mvuto!
 
Ile kitu si kiatu useme kina size na si msosi useme kina chacha, kama umedhamiria kuwa na girl wala usitake kujua hapo mwanzo alikuwa na nani kikubwa play part yako mwana!
Kumbuka, ukimchunguza bata huta mla....
 
unataka mvuto au kueleweka?hata shuleni mwalimu haangalii mwandiko ukoje anaangalia ulichoandika kinaeleweka??pole kwa kukosa kuuona mvuto kwenye story yangu
 
aiseeee wengine huwa tunachunguza kidogo manake bata nae ana mambo mkuu!!!
 
mkuu hawa mademu usikute hata siku unamuoa kibabu kinamnunulia hata nguo ya send off aiseee....halafu kinatoa zawadi kubwa..... nalog off aghhhhhhh
 
duuu, umekaa unasumuliwa yote hayo na unaruhusu, wangu mie angeshanikatiza katikati
 
Ha ha ha haaa! Kopo la dawa ya mbu badala ya perfume?..!???:lol::lol:
 
Huyo binti na huyo mzee sijui mbaba wote ni watu wazima hovyo.

Na wewe umepewa ruhusa ya kupeperusha story ya mwenzio humu? Usije ukamuharibia kwa buzi lake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…