Dengue

Asheengai

Member
Joined
Mar 18, 2014
Posts
30
Reaction score
5
Iwapo itatokea una kila dalili za homa ya dengue, dawa ya kukimbilia kwanza ni Panadol; inashauriwa usimeze KABISA Diclopar wala Diclofenac. Iwapo utameza dawa hizi, utakuwa kwenye uwezekano mkubwa wa kupoteza maisha.

Upatapo taarifa hii mjuze na mwenzio, imetolewa na wizara ya afya.

Homa ya Dengue nini?

Homa ya Dengue ni ugonjwa unaoenezwa kwa kuumwa na mbu aina ya Aedes mwenye virus vya ugonjwa huu. Mbu hupata virusi vya homa ya Dengue anapomuuma mtu mwenye ugonjwa huu.

Ugonjwa huu unaenezwa kutoka mtu mmoja kwenda mwingine kwa kuumwa na mbu huyu.

Dalili
Homa kali ya ghafla, Kuumwa kichwa, hususani sehemu za machoni, Maumivu makali ya viungo na misuli ya mwili, Kichefuchefu au kutapika Kutokwa na damu kwenye fizi, na sehemu za uwazi za mwili na uchovu.

Ukimsikia ndugu au jamaa yako anasema kuwa na dalili hizi muwahishe hospitali mapema
 
asante sana mleta mada.kinga ni bora kuliko tiba.
 

Tiba ni nini, au tunakwenda hospitali kusaidiwa kufa kistaarabu? I'm serious. Mzizimkavu kuna tiba mbadala?
 
Katika pita pita yangu mtandaoni nikakutana na ujumbe huu Alhamdulillah leo ngoja tuzungumze yale ya fani yangu (Siasa na Dini baadae kidogo) Sasa hivi jijini Dar es Salaam na Nchini kwajumla kumekuwa na Gumzo kubwa juu ya Ugonjwa hatari wa Homa ya Dengue hii imekuja baada ya kutokea vifo na baadhi ya watu maarufu kupata ugonjwa huu, naamini kuumwa kwa watu hawa maarufu ndio kumevuta tension ya Serikali na jamii kwa jumla ingawa mlipuko waugonjwa huu ulikuwepo tangu miezi kadhaa huko nyuma.

Nakumbuka nilipokuwa nafanya kazi katika Hospital ya Mwananyamala katika Kitengo cha Utafiti wa HOMA.Tulikuwa tunatafiti sababu za Homa kwa wagonjwa wa matibabu ya nje (OPD) yaani (aetiological causes of Acute febrilenesses). Tulikuwa tunapata kwa siku hadi wagonjwa wa tatu hadi wa tano waugonjwa huu kuanzia kipindi cha mwezi wa pili, tuliitaarifu chini ya wizara husika. (Nisizame sana huko kwan mi simsemajiwa Taasisi wala wizara).

Jaman Ugonjwa wa Dengue ni ugonjwa hatari unaoenezwa na Mbu kama ilivyokwa ugonjwa wa Malaria tofauti yake nikwamba Mbu wa Ugonjwa huu sio yule wausiku wa manane,huyu ni yule anayepatikana mchana kweupee. Hakuna maambukizi kwa njia ya kugusana na mgonjwa wala kula nae. Pia tofauti nyingine na Malaria ni kuwa ugonjwa huu ni Viral infection ambapo Malaria ni Protozoa (Plasmo dium speciesnk)

DALILI ZAKE

Dalili zake zinafanana kwa kiasi na zile zaMalaria

1)Homa kali

2)Maumivu ya kichwa (ila kwa Dengue nikwa mbele Pembezoni mwa macho-periorbital.)

3)Mgonjwa anaweza kupata maumivu yaTumbo.

4)Kutapika na Kuharisha

5)Pia anaweza kutokwa na Damu katikaTundu za mwili kama Machoni, puani na masikion.

UTAGUNDULIKA VIPI?

Dalili peke yake hazitoshi kumdiagnose mgonjwa kwani hizo ni dalili za Maradhi mengi, So kuna kipimo maalumu chakumjua mgonjwa (RAPID TEST) ambapomgonjwa anachukuliwa damu yake nakupimwa.

Kwa kuwa ugonjwa wenyewe ni Wa Virus ni ngumu kumuangalia virus kama virus kwani inahitajika Electron Microscope au kipimo au PCR, kwa hiyo kinachofanyika nikuangaliwa Antibodies (king azilizozalishwa mwili baada ya kupatamaambukizi), hiv yo kipimo kitaoneshahaya maambukizi ni ya sasa au ni ya mudamrefu.

MATIBABU

Tofauti na Malaria ugonjwa huu hauna Dawa Maalum (kwasabab u ni wa Viralinfection). Kinachofanya mgonjwa atatibiwa kutokana na Dalili alizokuja nazo. Watu waondoe hofu mara nyingi ViralInfections huwa ni Self limiting yaanzinaisha zenyewe kama ilivyokuwa kwaugonjwa wa Mafua.

NIFANYE NINI NIKIJIONA NA DALILI ZAUGONJWA HUU

1) Nenda haraka katika kituo cha Afya kwaajili ya uchunguzi zaidi.

2) Usimeze Dawa yoyote ya kutuliza homaau maumivu zaid ya Paracetamol.Hapa ngoja niweke angalizo zaidiNi kwamba katika moja ya athari zaugonjwa huu ni kupunguza Platelets(chembe sahan zilizopo katika damu) kaziya hizi ni kugandisha damu paleunapopata jeraha,Na ndio maanamgonjwa wa Dengue anakuwa anatokadamu katika tundu za mwili kwasababuanakuwa amepungukiwa na hizi chembe.

Kuna aina ya dawa katika side effect zake ni kuzuia ufanyaji kazi wa hizi chembe. Dawa zenyewe kama;

1) Asprin

2)Diclofenac

3)DicloparDawa hizi mgonjwa wa Dengue akitumia atafanya ugonjwa uwe hatari zaidi kwake hivyo inapaswa asitumie.

UZURI WA UGONJWA HUU

1)Ili kujikinga na Mbu waumao mchana lazima uvae nguo ndefu, Hapa wavaa VIMINI lazima watajistiri tu mwaka huu haha ha ha ha

2)Wanaohamasisha watu walale kwenye Net na kuwacha kuhamasisha kutokomeza Mazalia ya Mbu Wawaahamisishe kutembea na Net pia.Ha ha ha haha.......(Mna kubali kupewa Net nyie mnatoa Dhahabu mwaka huu lazima mtahamasisha kutokomezwa Mazalia ya mbu tu na Miradi yenu kwishnehi ha haha)

saurce; HAPA
 
Daah eti uzuri wa ugonjwa huu! Tumefika hadi kwenye uzuri wa magonjwa?
 


DAWA YA UGONJWA WA DENGUE:JANI LA PAPAI


Nimeona nishee nanyi. Nitatoa tasfiri ya kiswahili kwa faida ya wote.


Nimeipata sehemu, kwa wale ambao hawajaipata taarifa hii


I would like to share this interesting discovery from a friend'sclassmate's son who just recovered from dengue fever. Apparently his son was inthe critical stage at the ICU when his blood platelet count dropped badly after15 litres of blood transfusion. His father was so worried that he soughtanother friends recomendation whose son was saved. He confessed that he gavehis son raw juice of papaya leaves. After drinking the raw papaya leaf juice,his blood platelet count rose instantly to a good level. Even the doctors andnurses were surprised and after the second day the sick son was discharged. Sohe asked me to pass this news around. Accordingly it is raw papaya leaves, 2pieces just cleaned, pounded and squeeze with filter cloth. You will only get 1tablespoon per leaf. So 2 table spoon per serving once a day. Do not boil, cookor rince with hot water, it will loose its strength. Only the leafy part and nostem or sap. That papaya juice is a natural cure for dengue fever as denguefever is rampat now, I think it is good to share this with all. Please spreadthe news about this as there are many dengue cases. It is great if such naturalcure could help release the suffering of dengue. Blend them and squize thejuice.


DAWA YA UGONJWA WA DENGUE


Ninaomba kushea nanyi kama nami nilivyotumiwa kwenye Whatsapp


Baada ya kuupata huu ujumbe nikawajulisha wengine kwa njia yasimu. Mtoto wa rafiki yangu mwenye umri wa mi a ka 4 ametumia hii dawa jana tarehe 12/5/2014, leo kaamka hajamno kabisa.

1. Chukua majani au matawi 2 ya mpapai

2. Yaoshe vizuri

3. Yatwange

4. Tumia kitambaa cheupe kukamua ili upate juisi

5. Utapata vijiko 2 vya chakula

6. Mpatie mgonjwa

Inasaidia sana, kama nilivyoelezea kuwa mtoto wa rafiki yanguimemsaidia kwa kiwango kikubwa.

ANGALIZO: Tunapenda ku share mambo mazuri jinsi tuwezavyo

Nimeileta kwenu kama nami nilivyotumiwa na nimeshirikisha wengineimewasaidia

Kama speed ya mtandao wako Inardhisha tembelea hapa:
http://www.youtube.com/watch?v=LqlTqcfhYGQ
 

DAWA YA UGONJWA WA DENGUE

Ninaomba kushea nanyi kama nami nilivyotumiwa kwenye Whatsapp

Baada ya kuupata huu ujumbe nikawajulisha wengine kwa njia yasimu. Mtoto wa rafiki yangu mwenye umri wa mi a ka 4 ametumia hii dawa jana tarehe 12/5/2014, leo kaamka hajamno kabisa.

1. Chukua majani au matawi 2 ya mpapai

2. Yaoshe vizuri

3. Yatwange

4. Tumia kitambaa cheupe kukamua ili upate juisi

5. Utapata vijiko 2 vya chakula

6. Mpatie mgonjwa

Inasaidia sana, kama nilivyoelezea kuwa mtoto wa rafiki yangu imemsaidia kwa kiwango kikubwa.

ANGALIZO: Tunapenda ku share mambo mazuri jinsi tuwezavyo
 
Last edited by a moderator:
Asanteni sana. Je hii homa dalili zake zinachukua muda gani au unaanza hapo hapo kuugua homa kali na kichwa au inaanza taratibu ndipo inashika kasi? Imekuwa ya hofu kubwa sana.
 
Kutokana na ugonjwa huu kuingia hapa nchini naitaadhalisha Serikali iache kuweka maisha ya watu rehani kwa kukataa kuchukua hatua za kukomesha kuenea kwa ugonjwa.

Namna ya kudhibiti ugonjwa huu unaoenezwa na mbu ni rahisi sana wala hauitaji kujiingiza katika hiki tunachosikia eti "NIMR wajitosa kufanya utafiti wa kutokomeza dengue fever" huu ni ufisadi kama fisadi nyinginezo walizozoea Serikali yetu!

Entomology ya mbu wote ni moja haijalishi ni Aedes Egyptae, Anopheles au Qurex, hivyo na control yake ni moja tu larvicide, source reduction na Organophospholous/ Organochloride insecticide spray kwa ulv method.

Kila manispaa ya Dar in Wataalamu wa Sayansi ya Afya ya Mazingira, watumike kufanya kazi hii na pia kutoa elimu ya afya kwa jamii jinsi ya kuangamiza mazalio ya mbu kwenye maeneo yao, waache kuwatumia kukimbizana na wamachinga na bodaboda kusudi wafanye kazi yao ya kitaalamu. Wamefundishwa kufanya surveillance na quarantine ya magonjwa yanayoambukiza, pia wanajua kufanya epidemiology ambapo kwa sasa ugonjwa huu unasemekana kuwa jijini Dar tu au pengine upo hata mikoani lakini hakuna reporter huko! Wawape kazi yao hii waifanye na wakishindwa watuombe msaada tuko tayari kuzuia watu wasife kwa ugonjwa huu unaozuilika.

Napinga NIMR kujichotea mapesa kwa kisingizio cha Dengue Fever Control Program! Manake wameshaanza kusuka deal hili, waache kwakuwa kitengo cha mradi wa kudhibiti malaria kiko chini yao miaka yote na wameshindwa malaria inaua mtu kila baada ya dakika tano hapa nchini.

Kununua dawa na vifaa hospitalini kama alivyoagiza rais hakutasaidia kwakuwa wapo watakaokufa bila kufika hata hospitali au kufika wakashindwa ghalama za matibabu.
 
Imekuwa kero sasa jijini, haina tofauti na kikombe cha babu Samunge enzi hizo. Huu ni ugonjwa wa kawaida sana upo tangu zamani sio mpya. Uko Malaysia na Thailand wameuzowea.

Wanajikinga kwa kunywa juice ya majani ya mpapai na asali iweje huku utafune masikio ya watu kiasi hiki, ukiwa na panadol na maji ya kutosha una kinga tosha kelele za nini sasa?

Bunge la bajeti / kiporo cha katiba mpya mbona havipigiwi kelele?

Misamaha ya kodi n.k au sio hbr izo?

Wake up guys.
 
Vipeperushi vingiii ujinga tuu
 

Attachments

  • 1400043362994.jpg
    80.5 KB · Views: 118
  • 1400043380934.jpg
    76 KB · Views: 122
  • 1400043400348.jpg
    82.3 KB · Views: 150
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UGONJWA WA HOMA YA DENGUE “DENGUE FEVER”


Utangulizi

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inapenda kutoa taarifa kwa Umma juu ya mwenendo wa ugonjwa wa homa ya dengue yaani “dengue fever” hapa nchini.Ugonjwa huu umethibitishwabaada ya sampuli zilizochukuliwa kutoka kwa watu waliohisiwa kuwa na ugonjwa huu jijini Dar es Salaam kupelekwa kwenye maabara yetu ya Taifa Dar es salaam na kuthibitisha kuwa na virusi vya homa ya dengue mnamo mwishoni mwa mwezi wa Januari 2014. Hadi sasa idadi ya wagonjwa ambao wamethibishwa kuwa na ugonjwa huuni 400 na Vifo 3. Kwa wiki iliyoshia tarehe 9 Mei 2014 ya idadi ya wagonjwa waliogundulika mkoani Dar es salaam ni 60 (42-Kinondoni, 14-Temeke na 4-Ilala) na idadi ya wagonjwa waliopo wodini mpaka sasa ni 13.

Aidha, mlipuko wa ugonjwa huu si mpya hapa nchini kwani uligundulika kwa
mara ya kwanza mnamo Juni 2010 mkoani Dar es Salaam ambapo idadi ya watu 40 walithibitika kuwa na ugonjwa. Pia, kati ya mwezi Mei hadi Julai 2013,wagonjwa 172 walithibitishwa kuugua ugonjwa huu.

Homa ya Dengue

Homa ya dengue ni ugonjwa unaosababishwa na kirusi ambacho kinaenezwa na mbu wa aina ya Aedes.

Dengue in ugonjwa uliosambaa duniani katika nchi za ukanda wa joto. Takribani asilimia 40 ya watu wote duniani wanaishi katika nchi zenye ugonjwa huu. Takwimu za Shirika la Afya Duniani zinathibitisha kuwa takribani matukio milioni 5 ya Dengue yanatolewa taarifa kila mwaka. Watu laki 5 hulazwa hospitali kwa kuathirika na Dengue kali. Homa ya Dengue imeshatokea katika nchi zipatazo 34 barani Afrika.

Hapa Afrika Dengue ni ugonjwa unaojulikana kwa kiwango kidogo sana. Licha ya kwamba milipuko ya kwanza imetokea tangu mwanzoni wa karne ya 19. Matukio ya Ugonjwa huu yameongezeka Afrika tangu miaka ya 1980, matukio mengi yakitokea nchi za ukanda wa Mashariki mwa Afrika ikiwa ni pamoja na Msumbiji, Somalia, Kenya, Komoro, Djibouti na Tanzania. Ikumbukwe kuwa jina “Dengue” linatokana na neno “Dinga” la kiswahili linalolomaanisha ugonjwa unaotakana na pepo yaani Kudinga pepo. Mabaharia wa Kispanish walipokuja kwenye pwani ya Afrika Mashariki walirudi kwao na kuuita “Dengue”.

Dalili za ugonjwa huu ni homa, kuumwa kichwa, maumivu ya viungo na uchovu Dalili hizi huanza kujitokeza kuanzia katisiku ya 3 na 14 tangu mtu alipoambukizwa kirusi cha homa ya dengue. Kwa wakati mwinginedalili za ugonjwa huu zinaweza kufanana sana na dalili za malaria, hivyo basi wananchi wanaombwa kuwa wakati wakipata homa kuhakikisha wanapima ili kugundua kama wana vimelea vya malaria ua la ili hatua stahiki zichukuliwe.

Kuna aina 3 tofauti za namna ugonjwa huu unavyoweza kujitokeza iwapo mtu aking`atwa na mbu mwenye virusi hivi;

i.Homa ya dengue (Dengue Febrile Illness): Aina hii huambatanana dalili kuu tatu za homa kali ya ghafla, kuumwa kichwa na maumivu ya viungo au uchovu.Aidha, kwa Tanzania mpaka sasa zaidi ya asilimia 90 ya wagonjwa wamejitokeza na dalili hizi.

ii.Dengue ya damu (Dengue Haemorrhagic Fever): Aina hii yahoma ya dengue huambatana na dalili za mgonjwa kutokwa na damu kwenye fizi au puani, vile vile kutokwa na damu chini ya ngozi.Iwapo mgonjwa huyu ataumia sehemu yoyote ni rahisi kwake kupoteza damu nyingi kupitia kwenye michubuko.

iii.Dengue ya kupoteza fahamu (Dengue Shock syndrome): Aina hii ya homa yadengue huambatana na mgonjwa kupoteza damu nyingi ambayo hupelekea mgonjwakupoteza fahamu. Dalili hizi zimeonekana kwa mgonjwa 1 kati ya wagonjwa 400 waliokwisha kuthibitishwa kuwa na ugonjwa hapa nchini.
Kirusi cha homa ya Dengue kinaambukizwa kutoka mtu mmoja hadi mwingine kwa kuumwa na mbu wa Jamii ya Aedes, na hasa Aedes aegypti. Mbu huyu anaishi katika mazingira ya makazi ya binadamu. Huuma wakati ya mchana ndani ya nyumba au kwenye maeneo yenye vivuli, hususani majira ya asubuhi na jioni kabla jua halijazama.

Mbu huyu anazaliana katika maji yaliyotuama hasa kwenye vyombo vya nyumbani, makinga maji ya paa za nyumba, matairi ya gari, ndoo, vikopo, na kadhalika. Kwa bahati mbaya mbu huyu huweza kuzaliana katika vifaa vidogo vidogo ambavyo watu wengi huvidharau. Hivi ni pamoja na makopo ya kuotesha maua, vikombe, vifuu vya nazi, na kadhalika. Majani mapana yanayohifadhi maji ni mazingira mazuri kwa kuzaliana kwa mbu huyu, hivyo maeneo ya bustani siyo ajabu kuwa mahali pazuri kwa mbu hawa.

Ugonjwa huu hauambukizi kwa kumhudumia mgonjwa au kugusa majimaji yanayotoka kwa mgonjwa. Homa ya dengue inaweza kutibika kama mgonjwa atapelekwa hospitali mapema na kupatiwa matibabu ya haraka.Hakuna dawa maalumu ya ugonjwa wala chanjo bali mgonjwa anatibiwa kutokana nadalili zitakazoambatana na ugonjwa huu kama vile homa, kupungukiwa maji au damu. Endapo mgonjwa atachelewa kupatiwa matibabu, mgonjwa anaweza kupoteza maisha.

Jinsi ya kujikinga na ugonjwa wa homa ya dengue

Kuangamiza mazalio ya mbu

Fukia madimbwi ya maji yaliyotuamaau nyunyuzia viuatilifu vya kuua viluwiluwivya mbu kwenye madimbwi hayo
Ondoa vitu vyote vinavyoweza kuweka mazalio ya mbu kama vile: vifuu vya nazi, makopo, magurudumu ya magari yaliyotupwa hovyo, nk.
Fyeka vichaka vilivyo karibu na makazi ya watu
Hakikisha maua yandayopandwa kwenye makopo au ndoo hayaruhusu maji kutuama
Funika mashimo ya maji takakwa mfuniko imara
üSafisha gata za paa la nyumba ili kutoruhusu maji kutuama


Kujikinga na kuumwa na mbu

Tumia viuatilifu vya kufukuza mbu “mosquito repellants”
Vaa nguo ndefu kujikinga na kuumwa na mbu
Tumia vyandarua vilivyosindikwa viuatilifu (kwa wale wanaolala majira ya mchana na hasa kwa watoto)
Weka nyavu kwenye madirisha na milango ya nyumba za kuishi


Hatua zinazochukuliwa na Wizara

(i)Hatua za Dharura

Uratibu

Timu ya Taifa ya Maafa inayoshirikisha wadau mbalimbali ikiwemo wa Halmashauri za Jiji na Wadau wa Maendeleo hukutana kila mara 2 kwa wiki kutathmini mikakati ya dharura iliyowekwa.

Uelemishaji na Uhamasishaji wa Jamii

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ilitoa tamko la Serikali kwa nyakati tofauti kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa Dengue. Tamko la kwanza lilitolewa kwenye vyombo vya habari tarehe 04 Februari 2014 na Machi 2014.
Kuendelea kutoa taarifa ya tahadhari ya ugonjwa huu kupitia kwa Waganga Wakuu wote wa Mikoa na Wilaya kwa Tanzania Bara. Aidha taarifa hii pia iinajumuisha namna mgonjwa anavyoweza kutambuliwa (Ainisho la Ugonjwa), “Ukweli Kuhusu Ugonjwa“(Fact sheet), Mwongozo kwa watumishi wa afya wa namna ya kuchukua sampuli. Vipeperushi vinavyoelezea jinsi ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huu vitatolewa.
Kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kupitia Radio, na Runinga. Aidha Wizara kwa kushirikiana na Halmashauri za jiji wameendelea kutumia Maafisa Afyaikiwemo wa kata kuwaelemisha wananchi namna ya kudhibiti ugonjwa kwakutumia vipaza sauti, uongozi wa mitaa


Mafunzo kwa watalaam wa Afya

Kuendelea kutoa elimu ya Afya kwa Watumishi wa Afya ikiwa pamoja na madaktari na mafundi maabara namna ya kutambua ugonjwa huu. Aidha watumishi wa hospitali za Muhimbili, Mwananyamala, Amana na Temeke wamekwisha kupewa mafunzo haya na bado wanaendelea kupewa kupitia mikutano yao ya asubuhi (Clinical meetings). Mafunzo haya pia yanaendelea kutolewa kwa vituo vya chini kupitia Halmashauri


Kuimarisha mfumo wa ufuatiliaji na mawasiliano

Kuimarisha ufuatiliaji wa ugonjwa huu katika vituo vya kutolea huduma za afya pamoja na mipakani kupitia mfumo wa saveilensi ya Wizara. Aidha, pamoja na Mwongozo huu, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imetoa maelekezo kwa Waganga wakuu wa mikoa na wilaya hapa nchini kutoa taarifa za wagonjwa wa Dengue Fever kupitia taarifa za kila juma.
Kutoa miongozo ya ufuatiliaji wa ugonjwa huu katika maeneo ya mipakani kuhusu kutokuwepo kwa aina yoyote ya vikwazo vitakavyowekwa kwa ajili kwa wasafiri. Aidha maelekezo hayo yameainisha kuwa iwapo msafiri anayeondoka au kurudi nchini akiwa na dalili tajwa atoe taarifa kwa watumishi wa afya wa mpakani ili hatua stahili ziweze kuchukuliwa
Kufuatilia kwa karibu ongezeko la wagonjwa wenye homa isiyo kuwa ya malaria kwa Mikoa na Wilaya zote nchini ili kuweza kufanya uchunguzi wa kina iwapo kuna ugonjwa huu. Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imeshafanya utafiti mkoani Kagera, Morogoro na Kigoma na kuthibitisha kuwa haijaadhirika na dengue.
Kuanzishwa kwa vituo maalum vya ufuatiliaji wa ugonjwa huu katika Hospitali za Manispaa za jiji la Dar es Salaam (Mwananyamala, Amana na Temeke). Aidha, Kituo cha ‘International School of Tanganyika – IST’ kilichopo Manispaa ya Kinondoni na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili zinaendelea na ufuatiliaji wa ugonjwa huu. Aidha Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii itafungua pia vituo mkoani Tanga na Mtwara, mikoa imayopakana na nchi jirani yaani Kenya na Msumbiji ambako ugonjwa huu pia umetolewa taarifa.
·Kupeleka taarifa ya mlipuko huu Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) kama mwongozo wa Kanuni za Afya za Kimataifa uvyaoelekeza.


Upimaji na Tiba

Kuimarisha uwezo wa kutambua ugonjwa huu kwa kina kupitia maabara ya Taifa (NHLQATC) iliyopo NIMR. Vile vile Wizara imepeleka vipimo sawia yaani “Dengue Rapid Test Kits” kwa vituo vya Dar es Salaam kuimarisha utambuzi. Vituo hivo ni pamoja na hospitali za Muhimbili, Amana, Mwananyamala, Temeke Hospital, na IST kliniki. Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imeagiza Bohari Kuu ya Dawa (MSD) kuhakikisha vitendanishi hivi vinakuwepo ili kurahisisha upatikanaji wake kwa Halmashauri zote na kupelekwa kwenye vituo vya chini zaidi. Wizara imeagiza vipimo sawia 750 vya kunyongeza ambavyo tunatarajiwa kuvipata tarehe 22.5.2014
Wizara imeweka utaratibu wa kuhakikisha vifaa Tiba vinapatikana wakati wote katika vituo vyote kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa watakaogundulika na kuwa na ugonjwa huu.


Udhibiti wa mbu na mazalia

Kudhibiti mbu kupitia kwa kupulizia na kunyunyizia viuatilifu katika baadhi ya maeneo yaliyoathirika katika mkoa wa Dar es salaam ambayo wametoka wagonjwa wengi wa Dengue. Hii inalenga kuangamiza mbu wapevu na viluwiluwi.

Utafiti
Taasisi ya Utafiti ya magonjwa ya Binadamu (NIMR) iko katika maandalizi ya kufanya utafiti kuhusu dengue kwa kuangalia maaeneo makubwa mawili.

Ukubwa wa tatizo katika binadamu
Mbu waambukizao ugonjwa wa homa ya Dengue- kujua jamii husuka, tabia ya kuuma watu, wapi wanapopendelea kuuma, wapi wanakozaliana kwa wingi na mazingira yao ya kawaida.

Tafiti hizi zinaanzia Dar es Salaam na kuhusisha wilaya zote tatu (Ilala, Kinondoni, Temeke). Tafiti zitaendelea katika baadhi ya mikoa, ikiwa ni pamoja na mikoa 8 ambako vituo vyetu vipo.Takwimu zitakazopatikana zitaboresha mbinu za kupambana na ugonjwa huu

(ii)Hatua za Kudumu

WAUJ imeandaa Mpango wa wa namna ya kukabiliana na ugonjwa wa Homa ya Dengue. Mpango huu kwa kushirikisha sekta mbalimbali.
Kuimarisha mfumo wa ufuatiliaji wa ugonjwa wa Dengue


Hitimisho

Wananchi wanashauriwa kutokuwa na hofu kuhusu ugonjwa huu kwani hauambukizwi kwa kumhudumia mgonjwa au kwa kugusa majimaji yanayotoka kwa mgonjwa. Hata hivyo tunawashauri wananchi kwenda kwenye vituo vya afya haraka pindi wanonapo dalili za ugonjwa huu.

Mlipuko wa Dengue unadhihirisha kuwa mazingira yetu tunayoishi si salama. Ikumbukwe kuwa, kwa sehemu kubwa, ugonjwa huu unachochewa na mazingira machafu. Aidha mvua hizi kubwa zinazoendelea zonachangia kuongezeka kwa mazalio ya mbu. Utupaji, uzoaji na uhifadhi wa taka katika miji yetu hauridhishi kiasi ambacho kinatoa fursa kwa mazalio ya mbu kuongezeka na hata kuwa karibu zaidi ya makazi ya binadamu.

Kwa kuwa, hadi sasa hakuna chanjo wala dawa maalumu kwa ajili ya kudhibiti au kutibu ugonjwa huu, njia kubwa ya kupambana na ugonjwa huu ni kumzuia binadamu asimwe na mbu. Hivyo basi, mbinu shirikishi za kutokomeza mbu inabidi zitiliwe mkazo katika mapambano dhidi ya homa ya Dengue. Njia bora na rahisi ni kuhakikisha mazalio yote ya mbu yanatokomezwa. Na hili laweza kufanywa na kila mtu kwa nafasi yake.Tunashauri watu wavae nguo zinazofunika mikono na miguu na dawa zinazofukuza mbu (mosquito repellent). Tunaelewa kuwa si kila mtu atakuwa na uwezo wa kununua dawa hizi na ndiyo maana tunakazania swala la kuangamiza mazalia ya mbu ambalo ni jukumu letu wote.Tunaendelea kuhamisisha watu na hasa watoto walale ndani ya vyandarua venye viatilifu wanapolala wakati wa mchana.

Ningependa kuwakumbusha wananchi wa Tanzania kuwa, huu ni muda muafaka wa kuzingatia utunzaji bora wa mazingira yetu. Tukitunza mazingira yetu, nayo yatatutunza na kutuepusha na maradhi yanayoambatana na mazingira machafu.

Charles A. Pallangyo
Katibu Mkuu
12 May 2014
 
Nasikia kipimo tu cha huo ugonjwa elfu 50?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Na mi nimesikia hivyo
Hili ss hatari
Kwann wasifanye bure as ni ugonjwa wa mlipuko?
Serikali ipo serious kweli?
 
Kwa wale waliothibitika kuwa na ugonjwa wa Dengue tafadhali fuata maelekezo haya;

1. Tafuta majani ya mapapai mabichi ambayo si machanga sana wala yasiwe yamekomaa sana.

2. Twanga majani hayo kwenye kinu kama tunavyotwanga kisanvu mpaka yalainike

3. Kamua hayo majani ili upate juice yake ambayo ni ya kijani sana.

4. Usiongeze kitu chochote kwenye hiyo juice, usiongeze maji wala sukari

5. Dozi: Kunywa vijiko vitatu vya kulia (si vya chai) mara tatu kwa siku kwa muda wa siku saba

6. Dawa ni chungu sana lakini haina side effect

7. Usithubutu kumeza diclopar au diclofenac.

Mgonjwa ataanza kupata nafuu baada ya muda mfupi sana. Baada ya siku moja au mbili tu. Hata alipata nafuu aendelee kunywa dawa. Kumbuka hakuna dawa ya hospitalini inayoponya Dengue.

Papaya leaves can fight dengue
Dengue fever, caused by the dengue virus that istransmitted by mosquitoes, can be fatal. Symptoms include high fever withheadache, severe muscle pain, joint pain and red rashes on the body includingitching.

Till date, no medicine has been approved to treatthe dengue virus, traditionally, the juice of papaya leaf has beenfound to be useful in the treatment of dengue fever.

Few recent studies haveshown the effect of papaya leaf juice in curing the dengue fever. A recent one,done on five dengue patients by Indian Institute of Forest Management in 2012,found interesting observations.

Among the five patients, papaya leaf juice wasfound to be effective in curing dengue. The platelet count increased in allfive patients within 24 hours of drinking the papaya leaf juice. All of themreported significant improvement in health.


A 2009 study, done on mice in Malaysia, reportedsignificant improvement in thrombocyte count in the group which received papayaleaf formulations compared to the control group.

It seems that this bittergreen juice is promising without posing any serious ill-effects. As a result,pharmaceutical and nutraceutical companies began formulating papaya leafextract preparations.
 
Jamani huu ugonjwa utatuua tukimbilie WAP had I muhimbil upon jaman tafwaaaaaaaaaaaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…