Deni la mkopo la HESLB kwangu halipungui nikangalia mtandaoni licha kukatwa na kuoneshwa zimelipwa

markbusega

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2015
Posts
826
Reaction score
848
Nilitunza kumbukumbu za deni la mkopo wa wanafunzi elimu juu HESLB lililobaki hadi mwezi Juni 2021 la mtandaoni ili nije nilinganishe na la mwezi unaofuata nione kama linapungua nimebaini halipungui sijui shida iko wapi?

Hali ikoje kwako mkuu, mbona sasa nashindwa kuamini hata taarifa za kwenye account yangu ya HESLB ya mtandaoni?
 
Unavosema la mtandaoni unamaanisha lipi?

Salary Slip inasemaje?
 
Nahisi hii imetokea kwa wote ambao wanacheki namba. Yaani salary slip ya mwezi July inaonesha hela imeenda HESLB lakini kwenye akaunti ya HESLB-OLAMS deni haliko updated.

Binafsi naona tuwasubiri bodi mpaka tarehe tano Agost na kuendelea, labda bado hawaja-update kwenye mfumo wao, au bado hazina hawajapeleka hela kwenye akaunti zetu za bodi.

KUWAPONDA BODI;
Kwa nini bodi wanakuwa wababaishaji kuhusu madeni ya wadaiwa. Mwanzoni mwa mwaka huu, walisema wataunganisha mfumo wa bodi na hazina ambapo kila mdaiwa atakuwa anaona deni lake kila anapolipa.

Sasa leo mwezi wa saba bado hawajaunganisha huo mfumo maana yake nini?

Je, hawaoni kwamba wasipounganisha mfumo wa bodi, na hazina mtu anaweza kuwa amemaliza deni lakini anaendelea kukatwa na hazina? Ikumbukwe, baada kuondoa VRF, wadaiwa wengi deni halisi limepungua kwenye akaunti ya OLAMS-HESLB, lakini kwenye salary slip deni ni kubwa! Deni halisi lipo bodi.

Kama bodi walikuwa chapu kupeleka makato kwa waajiri, je, ni kitu gani kinawafanya washindwe kupeleka deni halisi hazina baada ya kuondoa VRF? Yaani wapo shapu kukata ila wamekuwa wazito kuhuisha taarifa hazina!

Je, wataalamu wa TEHAMA hapo bodi hawana uwezo wa kushughulikia hili suala la madeni bila kufika ofisini? Kwa mfano, tangu juni niliomba bank statement ila mpaka leo sijapata! Halafu website yao nzito kweli. Sections ambapo zipo kwenye website ni kama mapambo tu, uki-click hazifunguki. Ukiomba statement unaambiwa subiri. Sasa si wawatafute hata watengeneza blogu wawasaidie kuweka sawa hiyo tovuti!
 
ngoja tusubiri tuone huo mwezi Agosti
 
Pia hii VRF imefutwa nusu,kwanini wasiifute jumla ,hawa jamaa wanakwama wapi?

Wazir wa Elimu alisema mnufaika alipe pesa aliyokopeshwa tu na vrf ya nyuma ilitakiwa kufutwa maana haikuwekwa kwenye hati za mshahara za wanufaika ambao ni watumishi wa uma hiyo value retention fee walikuwa nayo wao kwenye data base yao sasa ugumu wa kuifuta unatoka wapi?Pia sasa hivi hawatoi statement kwa wanufaika ambao wako mikoani kwa njia ya barua Pepe mpaka uende ofsini kwao,watupe majibu juu ya hili.
 
Wazir wa Elimu alisema mnufaika alipe pesa aliyokopeshwa tu na vrf ya nyuma ilitakiwa kufutwa maana haikuwekwa kwenye hati za mshahara za wanufaika ambao ni watumishi wa uma hiyo value retention fee walikuwa nayo wao kwenye data base yao sasa ugumu wa kuifuta unatoka wapi?Pia sasa hivi hawatoi statement kwa wanufaika ambao wako mikoani kwa njia ya barua Pepe mpaka uende ofsini kwao,watupe majibu juu ya hil
Hapa inabidi wadaiwa wachangamke kulipa mwaka huu wa fedha, si ajabu bajeti ijayo ngoma ikarudi kwa makali maradufu
 
Back
Top Bottom