Deni la Serikali hapa Tanzania ni kama kurithishana uchawi. Ipitishwe sheria Rais yeyote awe na ukomo wa kukopa!

Deni la Serikali hapa Tanzania ni kama kurithishana uchawi. Ipitishwe sheria Rais yeyote awe na ukomo wa kukopa!

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wakuu,

Ifikie muda tuache ku-judge wanasiasa kwa kutujengea vyoo na mabarabara.

Unakuta mwanasiasa anaenda kukopa World Bank na IMF alafu anaenda kujenga shule na zahanati

Kibaya zaidi anaenda kukopa hela ambayo mpaka anamaliza muda wake wa uonogozi hawezi kuilipa.

Hivi kuna kitu rahisi duniani kama kukopa na kwenda kufanya miradi? Hapo ni akili gani imetumika?

Hizi hela wanazokopa serikali ni kama kurithishana uchawi tu. Wanasiasa hawafikirii kuongeza vyanzo vya mapato, wanategemea mikopo ambayo kiongozi mwingine ndio anakuja kulipa.

Bunge lipitishe sheria kuweka kikomo cha Rais na awamu yake kukopa.

Deni lolote ambalo kulipwa kwake litazidi zaidi ya miaka 5 linatakiwa kuwa batili

deni 2.png
 
Hawa hawa walionunuliwa na marehemu ili wawe upande wake au wale walioburuzwa na kujikuta wamempitisha mgombea bila kufuata utaratibu wa chama?
 
Mbaya zaidi anakopa anaanza kununua magoli na kuwapa mamilioni taifa star badala ya kupeleka kwenye shughuli za maendeleo.
 
Back
Top Bottom