Deni la taifa kukua kwa kasi tafsiri yake nini?

G-son

Member
Joined
Sep 5, 2008
Posts
68
Reaction score
17
Wana JF Habari. Jana maada hii niliipelekwa kwenyejukwaa la "COMPLAINTS" nikashauriwa niilete hapa kwani ndo mahali pake ssahihi.

Ni kwamba nimekuwa nikijiuliza swali moja kuhusu uchumi wa nchi yetu. Mara nyingi nimesikia kwenye vyombo vya habari kuwa deni la nchi linaongezeka kwa kasi. Nikirejea kwa wananchi wa kawaida pindi mtu anaposhindwa kulipa deni mara nyingi huuziwa baadhi ya vitu vyake (hasa visivyo hamishika kama shamba, vyumba n.k.) ili kufidia deni lote au angalau kiasi cha deni.

Sasa swali langu la msingi hapa ni NINI HATIMA YA DENI LA NCHI KUKUA? NA UKOMO WA DENI ILI TUSIKOPESHEKE NI KIASI GANI? NA JE NI NJIA GANI NCHI HUTUMIA KUPUNGUA MADENI YA NCHI?

NATANGULIZA SHUKURANU ZANGU ILI NIELIMISHWE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…