Deni la Taifa la Tanzania kamwe halitalipika wala kupungua, tusidanganyike

Deni la Taifa la Tanzania kamwe halitalipika wala kupungua, tusidanganyike

markp

Senior Member
Joined
Sep 26, 2013
Posts
194
Reaction score
327
Deni la taifa kila rais anayeingia analiongeza kwa urefu na upana anaotaka.

Kama MKAPA trl 23, KIKWETE Trl 20 na MAGUFULI Trl 29 ukijumlisha hao tu unapata 72 na sasa tunaambiwa deni ni maeneo ya 70 huko huko sasa nani atakuja kuwa Rais ambae hatakopa ila atalipa au kupunguza deni kama wote wanajitahidi kulipaisha kama tai huku wakisema ni staimilivu.

Hao mnaowaita mabeberu unafikiri wanafikiria juu ya miaka 5 au 10 mnayowaza ninyi? Wenyewe wanapga hesabu hadi za miaka zaidi ya 100 huko wanajua kufikia huo muda mtawapigia magoti kuhusu hayo hayo madeni mnayoyaongeza huku mkiwa mnayaita ni staimilivu.

Kwasasa mnajiona wajanja kwakuwa mtakufu mkiwa mna pesa zenu ila nawahakikishia wajukuu wa wajukuu wataenda utumwani kwa haya madeni stahimilivu.

Hakuna hata mwenye mawazo ya tofauti kuhusu miradi na madeni wote wanatumia njia zile zile kutatua matatizo yote. Uozo mtupu.

Mkiambiwa Katiba Mpya itasaidia kuliweka taifa katika hali nzuri wabishi hatari. Endeleeni kufurahia mitano tena na tena na tena. Ila badae wajukuu wenu wasimtafute mchawi maana labda wabadili majina ya ukoo
 
Back
Top Bottom