Eng Kimox Kimokole
JF-Expert Member
- Jun 9, 2010
- 1,037
- 767
DENI LA TAIFA NA GIZA TUENDAKO
1961 - 1985
Chini ya utawala wa Mwl. Nyerere (RIP) aliyetawala kwa takriban miaka 25, pamoja na vita ya mwaka 1978-1979 na Idi Amini wa Uganda, mpaka anang'atuka madarakani Deni la Taifa lilikuwa trilioni 3 pekee.
1985 - 1995
Kwenye utawala wa Ali Hassan Mwinyi (RIP) aliyetawala kwa miaka 10 kwa mujibu wa Katiba ya JMT Deni la Taifa lilifikia trilioni 18.
Yaani Mwinyi alikopa na kutufikisha trilioni 15 zaidi na kulipaisha Deni la Taifa.
1995 - 2005
Huu ni wakati wa utawala wa Benjamin William Mkapa ambapo alikuta Deni la Taifa likiwa trilioni 18 lililoachwa na Mwinyi.
Mkapa akalipunguza Deni la Taifa kwa trilioni 8 huku akikuza uchumi kwa ukuaji wa 6.7%
Mkapa akaondoka akiacha Deni la Taifa likiwa trilioni 10 . Huyu ndiye aliyekuwa Rais wa Uchumi, aliyefanikiwa kudhibiti mfumuko wa bei na kuinua ukuaji wa uchuni Tanzania
Mpaka anaondoka Deni la Taifa ni trilioni 10
2005 - 2015
Jakaya Mrisho Kikwete akachukua nchi kutoka kwa Mkapa naye akatawala kwa miaka 10.
Kikwete akaporomosha ukuaji wa uchumi kutoka 6.7% kufikia 4.5% rekodi iliyowekwa 2012.
Kikwete akalifikisha Deni la Taifa kutoka trilioni 10 hadi trilioni 35 hii ikimaanisha kwamba Deni la Taifa liliongezeka kwa trilioni 25.
Kikwete akatuachia Deni la Taifa la trilioni 35
2015 - 2021
John Pombe Magufuli akachukua kijiti kutoka kwa Kikwete, akatawala miaka 6.
JPM alilikuta deni likiwa trilioni 35. Hadi kufikia Aprili 2018 Deni la Taifa likafikia trilioni 49.9.
Ndani ya miaka mitatu ya JPM akapaisha Deni la Taifa kwa trilioni 14.9. Halafu mwaka mmoja baadae yaani Aprili 2019 Deni la Taifa likafikia trilioni 51.03 likipanda kwa trilioni 16.03 ndani ya miaka minne ya utawala wake.
Mpaka kufikia Aprili 2021 Deni la Taifa likafikia trilioni 60.7, ikimaanisha kwamba kwa miaka 6 ya utawala wa JPM amelifikisha kwa kuliongezaDeni la Taifa kwa zaidi ya trilioni 25.7. Hiyo ni miaka 6 tu ya utawala wake mpaka mauti yanamfika.
Kikwete ndani ya miaka 10 amelipaisha kwa trilioni 25 na JPM ndani ya miaka sita amelipaisha kwa trilioni 25.7.
Hiki ndicho kipindi tuliambiwa miradi yote inatekelezwa kwa pesa za ndani. Hatukopi!!!
Pia ndicho kipindi ambacho tuliaminishwa kwamba uchumi unakua kwa 6% hadi 7% wakati kumbe uchumi ulikuwa kwa 5.2%
Kwa hiyo, mpaka JPM anaaga dunia Deni la Taifa lilifika trilioni 60.7
2021 - 2024
Rais Samia Suluhu Hassan akachukua madaraka kwa mujibu wa Katiba ya JMT pale Rais anapofariki, makamu huchukua Urais.
Kwa sasa Deni la Taifa ni trilioni 91.7 kutoka trilioni 60.7 za JPM.
Hii ikimaanisha kwamba, ndani ya miaka mitatu (3yrs) ya Rais SSH Deni la Taifa limeongezeka kwa trilioni 31.
Tukifanya mahesabu ni kama Deni la Taifa limeongezeka kwa trilioni 10.33 kwa kila mwaka na huenda tukienda kwa sequence hiyo Deni la Taifa likafikia trilioni 102 mwaka 2025 na iwapo ataendelea na urais basi ikafikia trilioni 153.65 mwaka 2030. Haya ni makadirio yangu tu!!!
Sawa deni inasemwa ni himilivu lakini ni AFYA?
Kwa sasa nyepesi / tetesi zinasema Deni la Taifa ni trilioni 112 kwa namna Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba anavyoelezea Deni la Taifa na huenda kuna tatizo la kimahesabu mahala.
Huu ni uchambuzi wangu kwa mtazamo wangu, this time msije mkanitupa Somalia 😂😂😂
Eid Mubarak kwenu nyote
Eng. Kimox Kimokole
Ngara, Kagera, Tanzania
June 17, 2024
Pia soma: