Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
DENIS PHOMBEAH KWA UFUPI
WanaMajlis,
Kuna mwenzetu mmoja kaniletea ujumbe huo hapo chini anataka
nimpe historia ya Denis Phombeah:
smarte_r said:
mzee wangu mohamed said itakuwa vyema kama utamuelezea kiundani huyo mnyasa hapa jf.
binafsi nataka sana kumfahamu vizuri na kufahamu uhusika wake katika harakati za kisiasa ndani ya tanganyika.
niwie radhi kwa ombi langu maana siku hizi nimekuwa sivutiwi kusoma magazeti ya hapa nyumbani hususani gazeti la raia mwema.
Jibu langu hilo hapo chini:
Smarte,
Sina taarifa nyingi kuhusu Denis Phombeah.
Denis Phombeah
Phombeah kwa mara ya kwanza nimemsoma katika kitabu, ''The Making of Tanganyika,''
Chato and Windus, London 1965.
Kitabu hiki kiliandikwa na Judith Listowel na alipokuja Tanganyika kufanya utafiti wake mwenyeji wake alikuwa Ally Sykes kupitia kwa Peter Colmore, Nairobi.
Kitabu hiki ndicho pekee katika vitabu vilivyoandikwa kuhusu historia ya TANU na harakati za kudai uhuru ambacho kimekaribia sana kusema kweli.
Ndani ya kitabu hiki Listowel anahadithia uchaguzi wa mwaka 1953 Ukumbi wa Arnautoglo kati ya Abdul Sykes na Julius Nyerere kuwania urais wa TAA.
Kuna kisa cha kueleza vipi Nyerere aliingizwa katika uongozi wa TAA kushindana na Abdul Sykes mwenyeji wake.
Kisa hiki nishakieleza hapa Majlis mara kadhaa naanimi unakijua.
Sasa kwa kuwa Denis Phombeah hakuwa anajua mipango iliyopangwa baina ya Abdul, Hamza Mwapachu na Ali Mwinyi Tambwe, yeye akitaka sana Nyerere ashinde uchaguzi ule akawa anawapitia wapiga kura kuwashawishi wamchague Nyerere.
Katika uchaguzi ule Nyerere alimshinda Abdul Sykes kwa shida sana kwa hiyo akawa Rais wa TAA.
Uongozi wa TAA 1953 kuelekea kuundwa kwa TANU 1954 ulikuwa kama hivi:
Viongozi hawa ni: J.K. Nyerere, President; Abdulwahid Sykes, Vice-President:
J.P. Kasella Bantu, General Secretary; Alexander M. Tobias and Waziri Dossa Aziz, Joint Minuting Secretary; John Rupia, Treasurer na Ally K. Sykes - Assistant Treasurer. Committee members Dr. Michael Lugazia, Hamisi Diwani, Tewa Said, Denis Phombeah, Z. James, Dome Okochi, C. Ongalo na Patrick Aoko.
Huyu Phombeah alikuwa mmoja kati ya vijana wa Dar es Salaam wa wakati ule ambao walikuwa katika siasa za TAA ingawa yeye alikuwa anatokea Nyasaland.
Kadi ya TANU ya Denis Phombeah ni no. 5.
Baada ya kifo cha Chihota kutoka Rhodesia ambae alikuwa meneja wa Arnautoglo Hall nafasi ile ikashikwa na Phombeah Mnyasa.
Chihota alifariki Uingereza mwanzoni mwa miaka ya 1950.
Phombeah rafiki yake mkubwa alikuwa Oscar Kambona.
Baada ya Oscar Kambona kwenda uhamishoni Uingereza mwaka wa 1967 Phombeah na yeye akamfuata huko.