#COVID19 Denmark yaondoa vizuizi vya kupambana na Covid-19

#COVID19 Denmark yaondoa vizuizi vya kupambana na Covid-19

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Denmark leo imekuwa moja ya mataifa ya mwanzo barani Ulaya kuondoa karibu vizuizi vyote vya kukabiliana na janga la Covid-19 baada ya taifa hilo la kanda ya Scandinavia kusema maradhi hayo siyo tena "kitisho kikubwa" kwa jamii.

Miongoni mwa kanuni zinazoondolewa ni masharti ya uvaaji barakoa kwenye usafiri wa umma, maduka, wateja wa mikahawa pamoja na amri ya kuonesha cheti cha chanjo kwenye maeneo ya burudani na mapumziko.

Maafisa wa taifa hilo la watu milioni 5.8 wamesema pamoja na kwamba kirusi cha Omicron bado kinasambaa nchini humo lakini hakijasababisha kuelemewa kwa mfumo wa afya na idadi ya wagonjwa walio kwenye vyumba mahututi imepungua.

Inatarajiwa mataifa mengine ya Ulaya ikiwemo Finland yatatangaza kuondolewa kwa vizuizi vya Covid-19 katika muda wa wiki kadhaa zinazokuja baada ya kupungua kwa kiwango cha maambukizi.
 
Back
Top Bottom