Dennis Nicholas Maria Bergkamp

Dennis Nicholas Maria Bergkamp

Matanga

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2019
Posts
2,281
Reaction score
3,976
_____________________________________________

Katika ligi kuu ulimwenguni zilizofaidi utamu wa wachezaji wa kidachi ,ligi ya Uingereza ni mojawapo.Achana na kina Virgil Van Dijk wa majogoo wa Liverpool na wengineo wa sasa .Walikiwepo kina Jaap Stam,Rud Van Nestoroy.

Katika orodha hiyo unamsahau vipi aliyekua golikipa wa Manchester United ,Edwin Van de Sir aliyepiga clean sheets 14 katika msimu wa 2008/2009 .Ndiye Golikipa pekee raia wa Uholanzi anayemiliki cleen sheets kuwahi kucheza ligi kuu ya Uingereza akiwa na jumla ya clean sheets 132.

Alikuwepo bwana mashoto Robin Van Parsie,Marc Ovamarc ,Mimacho Jimmy Floyd Asselbaink.Kabla ya hapo Walikuwepo pia kina Hans Segers na Michel Volnk na kutengeneza idadi ya wachezaji zaidi ya 133 wa kidachi mpaka sasa waliocheza ligi hiyo ya Malkia Elizabeth

When Asernal was Asernal walipita wadachi wawili Marc Overmac na wewe Denis Bergakamp.Ulikuwepo kwenye Asernal ya msimu wa 2003/2004 ambayo kwangu mimi haikua timu ya mpira ,ulikua ni mkusanyiko wa majiniasi wa soka.Lile jina mlilobatizwa la " the Invisibles" linathibitisha hiki ninachoamini.

Mechi 38 za ligi mkashinda 26 na kutoa sare mechi 12 ni vitu ambavyo hutokea Mara moja baada ya miaka mingi katika ulimwengu wa soka.

Perp Gardiola atakua amenielewa sana hapa.Msimu wa 2017/2018 alipojaribu kufanya kama mlivyofanya aliishia kuvunja rekodi ya kua na alama nyingi lakini sio kucheza ligi pasipo kupoteza mchezo hata mmoja.Majogoo wa Liverpool msimu huu walikipata walichokipata walipojaribu kuwaiga.

Kwenye kikundi kile Cha majiniasi wa soka chini ya Uongozi wa kaka mkubwa Patrick Viera ulikuwepo wewe muoga wa kupanda ndege .Wazazi wako waliokuzaa tarehe 10/5/1969 walikupa jina refu sana la Dennis Nicolaas Maria Bergkamp .Sisi wapenda soka tukachagua majina mawili tu ya kukuita ,Deniss Bergkamp basi ikatutosha.

Ulimfanya mfaransa Thiery Henry afurahie kucheza na kufunga kadri anavyojisikia.Wewe na bwana Matekenya Robert Pires mliufanya mpira wa miguu uonekane ni kitu rahisi kuliko kumeza mate.

Kaka Denis Bergkamp,nafahamu kama haukuwahi kuchukua ufungaji bora kwenye ligi ya Uingereza kama walivyofanya wadachi wenzako kina Jimmy Floyd Hasselbaink, Robin Van Persie na Van Nestoroy lakini ligi ya Uingereza pamoja na washika bunduki wa kaskazini mwa London hawana wanachokudai.

Wataanzaje kukudai ikiwa katika mechi 315 ulizocheza pale Highbury umefunga magoli 87 na kutengeneza 94?.Wakudai nini kama Asernal ya Wenger kupitia miguu yako umeicha na vikombe vitatu vya ligi kuu katika misimu ya 1997/1998,2001/2002/2003/2004?.

Hawakudai chochote wakikumbuka mara nne umekuwa mchezaji Bora wa mwezi katika ligi pendwa Ulimwenguni.Ulifanya hivyo August 1997,ukarudia September 1997 ,Kama haitoshi March 2002 ukamalizia February 2004.

Nikitaja jina lako nawatonesha Leicester city .Wanakumbuka February ya mwaka 1999 ulichowafanya hata ukabatizwa jina la the classic master .Wanakukumbuka ulivyohusika na magoli matano waliyofungwa na kuwafanya daraja la kuweka rekods ya kuwa mchezaji aliyetoa assist nyingi kwenye mechi moja kwa msimu ule.

Bergkamp ,Bergakamp Jina la kijanja sana kimaana kule Ujerumani kabla ya ujio wa Adolf Hitler . Maana yake ni mtoto wa mjini.Wakati pale Sweeden ukisema Bergkamp utakua ukimaanisha mapambano ya milimani.

Ndio umeishi kadri ya maana hizi mbili zinazobebwa na jina lako .Ulipambana tangu ukiwa kinda kwenye clabu yako pendwa ya Ajax kuanzia mwaka 1986 mpaka 1993 ,Ukaenda kwa wataliano kuonyesha ulivyo mtoto wa mjini ,ukawafungia magoli 11 katika michezo 52 uliyocheza.Kabla ya kwenda kushika bunduki pale Asernal mwaka 1995 mpaka utu uzima ulipokukuta ukawa tayari umeichezea klabu hiyo michezo 315 na kuwafangia magoli themanini na kenda.

Yes ,Yes,Denis Bergkamp ambaye leo tarehe 10/5/2020 anatimiza miaka 51 alikua mtoto wa mjini hasa na aliyepambana juu ya milima na mabonde katika historia yake ya soka.

Mwaka 1999 mwezi wa pili wakati Leicester city anakufa kwa goli 5 bila ulihusika kwenye magoli manne yaliyofungwa huku chogo mwingine toka Ufaransa Nicolous Anelka akiondoka na mpira kwa hat-trick wewe ukimchangia magoli mawili kwa assist zako.Baada ya mechi Ile nilisikia ukiitwa Master Class.Kweli mpira una watu wake na wewe ni mmojawao.

Kupitia miguu yako na majiniasi wakina ;
Jens Lehman,Ashley Cole,Martin Keown,Gael Clich,Sylvian Wiltold,Jose Antonia Reyes,Gilberto Silva,Fredrick Ljumberg,Ray Parlour,Robert Pires,Edu,Kolo Toure,Sol Campbell,Nwanko Kanu na wengineo mlifanya Aserna Wenger aweke alama isiyofutika kwenye mioyo ya mashabiki wa Asernal.

Ubora wako ukamfanya Wenger asifungwe na 4:4:2 yake na wakati mwingine akiamua anakuadhibu kwa 4:2:3:1 .Ni Asernal iliyokua na mkusanyiko wa majiniasi wa mpira toka nchi mbalimbali.Aliadhibu na kutoa burudani.Alicheza na kuwachezea wapinzani kwa Asernal ile iliyokua na mkusanyiko wa vipaji toka mabara ya Afrika iliyowakilishwa na Nwanko Kanu toka Nigeria,Sylivian Wiltod wa Cameron na Kolo Toure toka Ivory Coast,huku Edu na Silva wakileta burudani za America.

Haukuwepo tarehe 17 May 2006 siku Asernal inacheza fainali ya Uefa pale ufaransa katika dimba la Stade de France pale St Denis Ufaransa.Fainali ya kukumbukwa sana ikinogeshwa na tukio la mabadiliko ya galfa yaliyofanywa na Uefakwa kumbadilisha mwamuzi msaidizi aliyepangwa kwenye mechi hiyo Mnorway Herman Borgan baada ya picha yake akiwa amevaa jezi ya Barcelona kusambazwa mitandaoni.

Hata kama haukuwepo lakini ile ni Asernal iliyokua na roho yako.Ndio ulikuwepo uwanjani kiroho kama ambavyo ulikuwepo kimwili katika mechi dhidi ya wakatalunya hao pale Highbury msimu wa 1999/2000 round ya kwanza mkatoshana nguvu kwa magoli 1-1 kabla ya kufurushwa kwa magoli 4-1 baadae kule machinjioni Camp Nou ,Hispania

Leo tarehe 10/5/2000 unaposheherekea kumbukizi ya siku yako ya kuzaliwa nakushuru sana mimi binafsi kwa kunipa cha kuandika.Usingezaliwa ningeandika Nini?.Hata Ajax wangeuokosa mchangowako mkubwa wewe na mwenzako Marc Overmac dunia inafaidi ufundi wa Hakim Ziyech,Andre Onana,Donny de Beek,David Neres na Nicolas Tagliafico.Mikono yako ilishiriki kufinyanga kizazi hiki cha dhahabu cha Ajax .

Watu wa Real Madrid na Juventus wanapatwa na hofu wakiyasikia majina haya.Wanakumbuka kipigo cha magoli 4-1 pale Santiago Bernabeu na 2-1 pale Turin.

Leo Asernal inasumbuliwa na jinamizi la uwepo wenu.Kila inapopimwa kwa mlioyafanya msimu wa 2003/2004 wanaonekana hawatoshi.Wakasababisha mpaka mzee wenu Asern Wenger asepe, wakatimua Emery na sasa wapo nafasi ya 9 wakiwa wameshafungwa michezo sita na kutoka sare mara 13 chini ya Michael Arteta wakisubiri baraka za Mungu walau wacheze walau Uefa ndogo.

Good Night
___________
 
Mkuu lile goli dhidi ya newcastle umelisahau kabisa...kapokea pass safi kutoka kwa Pires ...kapokelea mguu wa kushoto beki hapo kaachwa tayar, ndani ya sekunde nyavu zinaweweseka.

Dah huyu jamaaa alikua motoooooo
 
Soka limepata mabadiliko makubwa mno zamani watu walikuwa wagumu mno na wahuni siku hzi watu n nyoronyoro sana

Wachezaji waliokuwa wana vipaji miaka hio walikuwa wanajua kweli ndo maana sio hata haja ya kumfananisha messi na kna maradona au pele
 
Sijui kwanini nimelisahau aisee lilikuwa moja ya magoli Bora kwa muda mrefu sana
 
Mkuu, unanikumbusha mbali mnoo...
Hao washkaji walikua wapo vizuri mno uwanjani...timu ya taifa ya akina Robben, Van persie pia ilikuwa moto sema hawakua wenye bahati mara nyingi wanaishia semi finals...kama unakumbuka 2014 walipigwa na Argentina nusu fainali, kisha wakaenda kukutana na brazil kuwania nafasi ya 3, brazil akanyukwa goli 3 wanaume Oranje Holland Clockwork Orange The Flying Dutchmen wakaibuka mshindi wa 3....

Germany 7-1 Brazil
Holland 3-0 Brazil
Germany 1-0 Argentina final

=10 katika mechi 2.

Walikuwepo akina Van der vaart huyu alikuwa attacking midfielder...Nigel de Jong is a Dutch professional footballer who plays as a defensive midfielder, kuyt n.k...
 
Soka limepata mabadiliko makubwa mno zamani watu walikuwa wagumu mno na wahuni siku hzi watu n nyoronyoro sana

Wachezaji waliokuwa wana vipaji miaka hio walikuwa wanajua kweli ndo maana sio hata haja ya kumfananisha messi na kna maradona au pele

Wanaojua mpira ndio wameamua iwe hivyo...hivyo sio wajinga kumfananisha Messi na hao uliowataja wewe... kusudio lako pia wakina Beckamps na wenzie ni zaidi ya Leo10s sio!!! Duh tatizo la wabongo ushabiki wa yanga na usimba umewaharibu kabisa 😀...tatizo mnapenda kukariri, kuigana ama kufuata mkumbo wa wengine wasiojua nini maana ya soka...
 
Wanaojua mpira ndio wameamua iwe hivyo...hivyo sio wajinga kumfananisha Messi na hao uliowataja wewe... kusudio lako pia wakina Beckamps na wenzie ni zaidi ya Leo10s sio!!! Duh tatizo la wabongo bwana ushabiki wa yanga na usimba mnauhamishia huku hilo ndio tatizo lenu 😀...mnapenda kukariri, kuigana ama kufuata mkumbo wa wengine wasiojua nini maana ya soka...

Hivi nikikuomba tu top 5 yako ya wachezaji bora wa muda wote, je utaniwekea + Individual capabilities/Awards katika team walizowahi kucheza??? Maana you speak without facts and evidence...
Sijamfananisha leombuzi na kina becks

Ndo maana nimesema leo na kina maradona na kina pele soma vzuri uelewe becks hawezi shndana na messi
 
Sawa kamanda nimekupata...so kwanini ukatae Messi sio wa kumfananisha na akina Diego na pele...je kigezo chako nini haswaa?
 
Sawa boss mm nimeangalia tu kwa juu katika mtindo huu, kama wale kina pele na maradona wana rekodi zile katika zile enzi za utabe maana soka halikuwa rahisi, vp kama wangecheza kpndi hchi??
Mm nadhani ingekuwa zaidi maana vipaji vyao ndo vinafanya kazi iwe rahisi, siwajui sana mabeki wa zamani hzo ila naamini aina yao ni mfano wa mtu kama maldini na zaidi

Hvyo booss
 
Mkuu, unanikumbusha mbali mnoo...
Hao washkaji walikua wapo vizuri mno uwanjani...timu ya taifa ya akina Robben, Van persie pia ilikuwa moto sema hawakua wenye bahati mara nyingi wanaishia semi finals...kama unakumbuka 2014 walipigwa na Argentina nusu fainali, kisha wakaenda kukutana na brazil kuwania nafasi ya 3, brazil akanyukwa goli 3 wanaume Oranje Holland Clockwork Orange The Flying Dutchmen wakaibuka mshindi wa 3....

Germany 7-1 Brazil
Holland 3-0 Brazil
Germany 1-0 Argentina final

=10 katika mechi 2.

Walikuwepo akina Van der vaart huyu alikuwa attacking midfielder...Nigel de Jong is a Dutch professional footballer who plays as a defensive midfielder, kuyt n.k...
Wale Holland sijui wanamkosi gani aisee hata ile final ya WC ya mwaka 2010 pale SA walifungwa na Spain yaani iliumiza sana
 
Soka lao la kuvutia unapenda kuwatazama jinsi wanavyosakata, but ndio hivyo kamanda, bahati hawana hawa jamaa...

Wanashikilia rekodi ya kucheza fainali nyingi za Kombe la Dunia bila kushinda mashindano hayo....They finished second in the 1974, 1978 and 2010 World Cups, wamepoteza na ujerumani Magharibi, Argentina na Spain respectively...walishinda ubingwa wa Ulaya wa UEFA mnamo 1988....
 
Back
Top Bottom