Bila shaka uongozi wa mkoa wa Pwani umefanya jambo la busara kumleta DEO mpya mama Elithabeth Ngoyani kuwa Afisa Elimu sekondari wilaya ya Bagamoyo.Kwani baadhi ya watumishi idara ya elimu walikuwa wanauwajibikaji chini ya kiwango.Uchapakazi wa DEO huyu utaleta tija kubwa katika idara ya elimu sekondari.Nimefurahishwa sana na hatua yake ya kuwashughulikia watumishi wazembe kwa kuanzia na pangua pangua ya wakuu wa shule wanaokinzana na BRN.Wakuu hawa baadhi yao wanashirikiana na baadhi ya watendaji wa ngazi za juu kuhujumu jitihada za serikali kuboresha elimu wilayani Bagamoyo.Wamekuwa wakirudisha nyuma maendeleo ya elimu kwa kuzorotesha mambo mbalimbali kama usimamizi wa nidhamu kwa watumishi,ukwamishaji wa miradi mbalimbali katika vituo vyao vya kazi na ukaidi wa kufata maagizo ya wakubwa wao.