"Nikajifanyia tathmini mimi mwenywe kwamba hivi mimi Mbunge mchango wangu ni upi kwenye kuhakikisha kwamba mambo mengi yanafanyika na kwakweli nilimuambia Mke wangu nasoma hapa asisikitike maana yake hela hizi ni za familia, Njombe mumshukuru maana nayasema naye amekubali anataka tuendelee kutoa huduma kwa Wananchi wa Njombe na kwa hesabu ya haraka haraka wakati ule nilikuwa nimetumia TSH. Milioni 400 za mfukoni mwangu katika miradi ya maendeleo" Deo Mwanyika, Mbunge wa Jimbo la Njombe Mjini.