Deogratias Kisandu amepatwa na nini? Tumsaidieni ushauri kijana mwenzetu

Tungepata vijana wenye akili kama yako nchi ingeendelea sana. Sana. Ngoja sasa waibuke waliokuwa wanalazwa sebulen na kwenye mabanda ya kuku.


 
Christopher Mtikila pia walidhani ni kichaa ila baadaye sana walianza muelewa. Mara nyingi binadamu wanaoongea kweli bali kweli tupu wanaonekana wehu kama si vichaa.
 
Kijana inaonekana dish lake zimeyumba channel zimepotea wasipomuwahi atachizika
 
Acha kumfananisha mtikila na watu wapuuzi wewe. Mbona mtikila nlikuwa namwelewa sana. Kisandu amepata tatizo la kiakili si wa kawaida. Maneno anayoandika ni ya mtu aliyechanganyikiwa mpaka ameona aanzishe chama..he is confused. Soma pale anaposema amerubuniwa na january ndo uta conclude amepatwa labda na malaria au ccm wamemfanya jambo.



Christopher Mtikila pia walidhani ni kichaa ila baadaye sana walianza muelewa. Mara nyingi binadamu wanaoongea kweli bali kweli tupu wanaonekana wehu kama si vichaa.
 
Halafu najua anakuja kujitetea humu kwa ids tofaut tofaut pamoja na jamaa zake waliokuwa wote wanalala mabandan mwa kuku au sebulen
 
Mmekuja. Good. Nioneshe maandiko ya kisandu yenye akili. Haya ya kulalamika alirubuniwa?ndo ya akili?kwa nini asifiche upumbavu wake?mwanaume mzima unalalamika ulirubuniwa na akina makamba?na akina dada watasemaje?
Hivi January Makamba yupo? Hasikiki kabisa.
 
Naona mkakati wake umeanza kufanya kazi. Tunamjadili!
 
Ana Vivid hallucinations(Kuota akiona vitu live), Auditory hallucinations /Delusions (Kuhisi anasengenywa, A anachekwa, anataka Kuuliwa) mixed with Grandiosity(kujiona mtu mkubwa na anayeweza kila kitu have hata yasiyotekelezeka(Uspika, Urais, Ubalozi, Ukatibu mkuu CCM, Uchiefu wa chama kipya etc

Hayo yote ni dalili ya ugonjwa wa ukichaa(Acute Psychosis, Mania na Major Depressive Disorder ) ndg zake kama hawatapa akili mapema kisandu atatembea uchi kwa hatua aliyofikia soon
 
 
Jam

Wadau salaam, Mimi ni mzima wa afya kabisa na hata kisaikolojia Niko fit kabisa. Tatizo ni moja tu "Telling the Truth is a Revolutionary act"

Deogratius N Kisandu
Chief Chairman elect of ACA expected.
 
ndugu kisandu tatizo si kusema ukweli. "ukweli uliochelewesha hauna tofauti na unafiki" ulikuwa wapi kuyaongea haya wakati huo? lakini pia unachoandika si kwamba unaongea ukweli. ila UNALALAMIKA. kuna TOFAUTI YA KUONGEA UKWELI NA KULALAMIKA. Ni aibu kubwa mwanaume kulalamika kuwa akina makamba walikurubuni. kurubuniwa ni neno baya sana. kusema ulifanyiwa utapeli wa kisiasa inaonesha wazi toka mwanzo wewe hukuwa na msimamo. we hukuwah kujua kuwa ccm ni walaghai?umehama vyama vingapi mpaka kuamua sasa kuja kuanzisha chako?

NI UONGO KUSEMA ETI CCM WANAKUWEKEA VIGINGI USIJE GOMBEA URAIS MWAKA 2020. NI upuuzi. wewe HUWEZI KUJA KUWA RAIS WA NCHI HII. siku WEWE UKIJA KUWA RAIS MI NTAHAMA NCHI HII NIKAISHI MWEZIN
I. maana kiukwel haupo ok. kaa chini tulia tuambie vijana wenzio tukusaidie nini. na nina waswas kuwa kuna jambo ccm wamekufanyia ili uonekane umechanganyikiwa kwa maandishi yako. ifikie hatua tuwe tunaheshimiana si kuwa tu watu mnakaa mnawaza mtakuja kuwa rais wa tanzania. hii ni dharau kwa sisi watanzania. si kwa sababu iliwezekana kwa kikwete sasa kila tom,dick and harry anataka kuwa rais. haya ni matusi makubwa sana kwa sisi wengine. ina maana mmetuona sisi ni punguani kiasi hicho?

ungetulia sehemu tafuta ubunge. tulia kwanza tuliza akili. umecheza kamali na CCM wamekula. unatakiwa ukae chini ujipange usilalamike kwa kuliwa na ccm. ulipoenda cheza nao karata tatu tayari ulikuwa umekosea.
nani kakwambia tatizo la watanzania ni chama? ndo maana nakuona una tatizo la kiakili si kawaida.

Jam


Wadau salaam, Mimi ni mzima wa afya kabisa na hata kisaikolojia Niko fit kabisa. Tatizo ni moja tu "Telling the Truth is a Revolutionary act"

Deogratius N Kisandu
Chief Chairman elect of ACA expected.
 
Nimekuwa nikifuatilia nyuzi mbalimbali za mwanachama mwenzetu anayejiita Deogratius Kisandu ambazo nyingi zimekuwa zikionyesha kuwa analaumu watu wakubwa nchini mfano aliwahi kumlaumu January Makamba kwa kukataa kwenda kwenye sherehe yake ya kumaliza chuo kikuu. na pia huwa anatoa mada zisizo za kawaida zenye dalili za uwendawazimu. lengo langu si kumtusi mwenzetu huyu ila kumsaidia kutokana na kuguswa na dalili za matatizo yake.

Ndugu Wanachama,

Tunapozungumzia afya tunamaanisha hali ya ustawi wa mwanadamu kimwili, kiakili na kijamii. Mtu mwenye afya njema ya akili anaaminika kutengemaa katika namna anavyofikiri, anavyohisi, na anavyotambua mambo, ambayo kwa pamoja hujionyesha katika matendo yake ya kila siku.

Magonjwa ya akili ni magonjwa ambayo yanaathiri uwezo wa mtu kufikiri, kuhisi, kutambua na kutenda, na hivyo kuwa na tabia au mwenendo uliotofauti au usioendana na jamii husika kiimani, kimila, desturi, na nyanja nyingine za kijamii. Tabia hizo zinatokana na ugonjwa wa akili kuathiri ufanisi na shughuli za mtu husika (mgonjwa) au huathiri jamii nzima inayomzunguka endapo mgonjwa huyo hatopatiwa matibabu stahiki na kwa wakati muafaka. Hapa nchini kwetu wagonjwa wengi wa akili hawafiki katika vituo vya kutolea huduma za afya na badala yake kuishia kwenye tiba za jadi au kutelekezwa na kunyanyapaliwa.

Takwimu zinaonyesha kuwa Tanzania ina idadi ya watu takriban milioni 45 na kutokana na taarifa ya afya ya akili kwa mwaka 2014/15 inaonyesha kuwa idadi ya watu 817,532 wanaugua magonjwa mbalimbali ya akili nchini, hii ni karibu asilimia 2 ya watanzania wote. Pia idadi hii ni ongezeko la wagonjwa 367,532 ukilinganisha na takwimu za mwaka 2013/14 walikuwa ni 450,000. Kati ya wagonjwa wote wa akili kwa mwaka 2014/15 wanawake ni ni 332,000 na wanaume ni 485,532. Mkoa wa Dar-Es-Salaam unaongoza kwa kuwa n awagonjwa wengi nchini ukifuatiwa n amkoa wa Dodoma na mkoa wa mwisho ni Lindi. Idadi hiyo ya wagonjwa ni wale walioweza kuhudhuria katika vituo vya kutolea huduma ya afya hapa nchini.

Magonjwa ya akili yapo ya aina nyingi na mengi huwa hayatambuliki kwa urahisi kwa jamii na hata kwa watoa huduma wa afya na hivyo wagonjwa wengi huchelewa kupata matibabu stahiki. Aidha wagonjwa wa akili wamekuwa wakibaguliwa na kunyanyaswa na jamii kutokana na imani potofu katika jamii yetu kuhusiana na sababu zinazo sababisha magonjwa ya akili pamoja na kutofahamu kuhusu matibabu ya magonjwa ya akili.

Dalili zinazoashiria magonjwa ya akili ni nyingi sana, baadhi tu ni ambazo zimegawanyika katika makundi matatu ni kama ifuatavyo:

i) Kihisia

  1. · Kukosa furaha kuhuzunika sana
  2. · Kuwa na furaha sana kupita kiasi
  3. · Wasiwasi na/ au woga kupita kiasina
  4. · Kupunguza kuongea au kutokuongea kabisa au kuongea sana kupita kiasi
  5. · Hasira za haraka haraka hata kufikia kupiga wengine
  6. · Kuwa na msongo wa mawazo
  7. · Kujitenga na watu na kupenda kukaa mwenyewe muda mwingi au kupenda kuwa na watu sana kuliko kawaida
  8. · Kutokuwa na ari ya kufanya kazi au kufanya kazi nyingi kwa wakati mmoja bila ya kuzikamilisha
  9. · Kutokuonyesha hisia yoyote usoni mwake (mf. furaha au huzuni nk)
  10. · Kutokujijali usafi na muonekano wake
  11. · Kuhisi maisha hayana thamani na kuona bora kufa kuliko kuishi na hatimaye kufikia uamuzi wa kujiua na hata kuua wengine.

ii) Kimwili

  1. · Mwili kukosa nguvu au kuhisi mwili una nguvu sana kupita kiasi
  2. · Kukosa usingizi au kulala usingizi sana kupita kiasi
  3. · Kukosa hamu ya kula au kuwa na hamu sana ya kula
  4. · Kutokutulia (kuhamanika) au kutulia sehemu moja muda mrefu bila ya kujisogeza
  5. · Maumivu sehemu mbalimbali za mwili kama vile kichwa, mabega, mgongo, na viungo mbalimbali ambavyo akienda hospitali vipimo havionyeshi tatizo lolote la kimwili.
iii) Kiakili
  1. · Kukosa umakini wa shughuli zake za kila siku
  2. · Kusahau kwa haraka au kupoteza kumbukumbu
  3. · Kukosa uwezo wa kupambanua mambo kwa mitazamo tofauti
  4. · Kusikia sauti ambazo hazipo na kuona vitu ambavyo havipo
  5. · Imani ya ajabu ambazo haziendani na mila, imani au desturi za jamii yake ; kama vile yeye ni mtu maarufu, au anaamini kuwa yeye ni Nabii
  6. au anaamini kupokea taarifa kutoka kwenye redio au mitandao ya simu
  7. · Pia anaamini ana nguvu ya ziada kutoka nje ya mwili yake inayomsababishia kutenda au kuwaza mambo anayoyawaza
  8. · Anaamini mawazo yake yanapunguzwa au kuongezwa na watu wasiojulikana, vyombo vya habari kama vile Radio na TV kuwa vinazungumzia yeye, au vinaongea mawazo yake yeye
  9. · Mawazo yake hayana mtiririko unaoeleweka.

Ndugu Wanachama,

magonjwa ya akili yanaathiri hisia (mood disorders) ambayo hupelekea watu kujiua pamoja na matatizo ya jinsia (sexual dysfuctions). Magonjwa haya mara nyingi yanapoanza yanaonekana ni hali ya kawaida tu na huenda pasiwepo na jitihada yoyote ya kupata msaada wa kitabibu hadi hali itakapokuwa mbaya au kuzidiwa.

Lengo langu tushauriane jinsi ya kumuokoa ndugu yetu kwani kila siku anazidi kupost mada zenye dalili za kuongezeka matatizo ya akili kichwani mwake. ikiwezekana mods wachukue hatua dhidi yake japokuwa natambua sheria ya uhuru wa kujieleza but not to that extension

NB: kwenye maandishi yenye rangi nyekundu ndio hasa dalili za matatizo ya akili anazoonyesha Deogratius Kisandu

Jembekillo
Paka Mweusi Gizani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…