Deontay Wilder vs Tyson Fury -2

godson Lomayani

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2018
Posts
538
Reaction score
711
Kwa wale wapenzi wa masumbwi naomba kuulizia kama mpambano wa hao mahasimu utaonyeshwa live, na kama ndio ni kwenye king'amuzi kipi? Naomba kuwasilisha.


======

UPDATES:


Tyson Fury amefanikiwa kumpiga mpinzani wake Deontay Wilder kwenye pambano lao la marudiano Februari 23, 2020 akimpa tabu na kusababisha mwamuzi kumaliza pambano katika raundi ya saba (TKO).

Fury, maarufu pia kwa jina la ‘The Gypsy King’ amekuwa Bingwa wa Masumbwi ya Uzito wa Juu wa Dunia wa WBC, na kuweka rekodi ya kuwa bondia namba moja kwa sasa kwenye uzito huo asiye na rekodi ya kupigwa kwenye mapambano yake yote, akiwa na sare moja ya pambano la kwanza dhidi ya Wilder.

Hakuna aliyetarajia kuwa Fury angeweza kushinda pambano hilo kwa KO, wengi walitabiri kuwa Wilder angeshinda kwa KO au Fury angeshinda kwa alama baada ya kengele ya raundi ya 12.

Aidha, Fury ameweka rekodi ya aina yake kwa kuwa bondia wa kwanza kumuonjesha joto la kipigo cha TKO Wilder ambaye mapambano yake yote ameshinda kwa KO isipokuwa pambano lao la kwanza mbalo lilimalizika kwa sare.

Katika pambano la leo, Fury alimtesa Wilder akimpasua sikio lake na kusababisha damu nyingi kutoka huku watu wakisubiri mwamuzi tu amalize pambano.

Tangu raundi ya kwanza Fury alianza kwa kasi na kumpa presha kubwa Wilder ambayo ilimshinda kuhimili. Katika raundi ya 3, Fury alimpiga chini Wilder kwa mfululizo wa makonde mawili.

Fury ambaye ni bondia kutoka nchini Uingereza sasa ndiye mwenye nafasi ya kupambana na bondia mwenzake muingereza, Anthony Joshua.

Joshua naye alishachafua rekodi yake baada ya kupigwa kwa KO katika pambano lake la kwanza na Andy Ruiz Jr., ingawa alishinda tena kwa alama kwenye pambano lao la marudiano.

Kwa mara ya kwanza, Wilder alionja joto la kupigwa na kuanguka ulingoni, ingawa mwamuzi alimkata alama Fury kwa kurusha konde wakati ameamua mapumziko (break).



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yule bishoo black anatakiwa apambane ya hela yote aisee ashinde
 
Huyu Deontay Wilder ni Habari nyingine. its all about the Puncher and the Fighter huyo Black ndio Puncher and Ngumi hatari sana
Mzee Wilder anapiga punch za hatari ila Furry nae anajua kuzikwepa, kwenye mpambano wao wa mara ya kwanza jamaa alikuwa akipiga hewa tu hadi akachoka, wakatoa draw
 
SuperSport 1 na SuperSport 5

Anaetaka aje PM nimpe email na password acheki kwenye DStv now ale uhondo
 
Bila shaka zitakuwa ngumi nzuri kama tu Tyson fury ataamua kupigana ngumi za kiume na sio kukimbiakimbia na ring au kukumbatia ili zifike 12round.

Sina shaka na Wilder, he is good fighter with good punch and always fighting for KO like Iron Mike Tyson..
 
yule sio mtu wa mchezo mchezo ngumi ngumu kama tofali yaani kitu jiwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…