Depression inaniathiri, nakaribia kujiua

Kaka tembea na huu msemo utakusaidia Sana maishani.
Believe in yourself bcoz your created with the image of the god
 
Yaani ujiue kisa una masikio makubwa? Aaah kijana! Hebu achana na hzo habari sasa hiyo hali inakuzuiaje kufikia malengo yako? Hivi unawajua wenye changamoto za kimaumbile wewe? Chalii angu hebu kuwa na shukarani kwa sir God!
 
Nakiona kitu kikubwa sana ndani mwako na mpaka hapo unapoandika unaonekana kwenu maisha ni mazuri. Hebu maliza shule, kuwa mtu wa kuwapuuza wakutaniao tena wakikutania wewe ongezea maneno ya shombo tu(yasiwe matusi). Naiona fursa kubwa sana ndani mwako ya kutengeneza pesa nyingi hatari.

Kuna mmoja wakati anaanza muziki alikuwa akiitwa Domo leo aitwa Lips Denda.
 
Mkuu iyo ishu yako nyepesi sana. Mim pia Depression ilikuwa initoe muda sana ila ni vile nikawa najichanga nipate hela za mazishi yangu kabisa ili nikifa nisisumbe ndugu zangu hela ya majeneza na gharama za mazishi na mengine kama hayo. Few days aisee nimempoea Yesu life yangu imekuwa updated yaan imeanza upya na ishu nyingine just soma skills ambazo zitakufanya uwe Excellence (the quality of being outstanding or extremely good.) Ukisha kua na kitu unique haijarishi una Sura mbaya or huna miguu kila mtu atahitaji kuwa karibu yako na maisha yatakuwa mepesi sana. Mwenzako ni handsome tu ila hakuna anae jali[emoji16].. hii life hakuna atakae jali kama huna ishu yoyote ya ku offer yenye faida kwake. Usione raia wanashinda humu Jf wengi ni wana depression zaidi hata ya zako ndio maana wengi wanatafuta hata mtu wa kujibizana nae apunguze ma stress yake..
 
Kijana Unyayo acha mawazo ya hovyo hovyo.
Jikubali kama ulivyo. Jifunze kupuuzia maneno ya watu kuhusu muonekano wako. Maneno ya watu hayana nguvu yoyote ya kukufanya wewe chochote ikiwa tu utajifunza kuyapuuzia.

Mtu akikucheka na wewe cheka kisha endelea na maisha yako. Mtu akikukashifu, wewe mpuuzie na endelea na maisha yako. Ukiweza kufanya hayo wala hupata shida yoyote.

Siyo kila mtu atakuchukia kwa sababu ya muonekano wako, wapo watu watakaokukubali jinsi ulivyo. Wanaokukubali na wewe wakubali, wanaokudharau na wewe wapuuzie maana hakuna lolote watakalo kusaidia.

Muonekano wako haukupunguzii "ubinadamu" wako. Hao wanaokunyanyapaa hawana chochote kile cha ziada kukuzidi wewe. Wao ni binadamu tu kama wewe, na usikubali kuyumbishwa na mitazamo yao juu yako.

Jifunze kujikubali kama ulivyo. Narudia tena, JIFUNZE KUJIKUBALI KAMA ULIVYO. Tena JIFUNZE KUWAPUUZA WALE WANAOKUDHARAU.

Ondoa kabisa kichwani mwako fikra za watu wanasema nini juu yako. Siku zote wewe jali zaidi kile unachokifanya. Ukitilia sana maanani maneno ya watu hutaweza kufanya mambo yako.

Hakuna ugumu katika kuyatimiza hayo yote niliyokuandikia. Ni rahisi mno ikiwa tu kuanzia leo UTAJIKUBALI KAMA ULIVYO.

ANGALIZO :
Ikiwa utaukataa ushauri wangu na ukashikilia mawazo yako ya "kujikataa" na kujali sana "maneno maneno" ya watu wanaokunyanyapaa na ukaona ni bora ufe kuliko kuishi, basi nitafute nikuelekeze namna rahisi ya kufa bila maumivu.

Uamuzi ni wako. Uchague kuishi kwa KUJIKUBALI na KUWAPUUZA wanaokunyanyapaa au uchague KUFA ili uwafurahishe zaidi hao wanaokunyanyapaa.
 
Ni kweli mkuu kama hujawahi kupitia hii hali huwezi kujua jinsi gani inakata
 
Nashukuru mkuu
 
Pole sana mdogo wnagu kwa changamoto unayopitia, ni kweli watu wengi wana matatizo makubwa sana na wameyakubli maisha yakaendelea, jitahidi sana kuikubali hiyo hali usiruhusu ikatawala sana mipango yako ya kesho, jithaidi kumtafuta mwanasikolojia mzuri atakushauri pia namna nzuri ya kuishi na hiyo hali.Kwa kuwa wew ni mdogo sana soma kwa bidii na focus yako iwe ni kupata fedha nyingi ukafanye surgery uishi kwa amani.
 
Nashukuru mkuu
 
Simama na umshukuru MUNGU alafu usijari wala nini dunia tunapita tu, we soma tafuta sana pesa alafu vile vile hayo masikio yako makubwa ni “BRAND” tosha ebu jaribu kujibrand aisee utakuja kuona matokeo yake baadae 🦻🦻🦻
 
TL: DR; Nenda kwa Wataalam Wanasihi waliosajiliwa, kwa ajili ya kupata msaada unaouhitaji.

Mazungumzo baada ya habari: Huko mitandaoni, pana informal definion of Depression:

Depression ni pale ambapo delusions za mtu hukutana na reality.

Kwa mujibu wa definition hiyo, ukijihisi una depression, jiulize una delusions zipi, na vipi zimekutana na reality. Kuondoka kwenye depression becomes a simple matter of removing delusions.
 
Asante mkuu kwa ushauri mzuri
 
Ubarikiwe mkuu
 
Mwenyezi Mungu atakufanyia wepesi kwa hayo unayopitia mkuu. Siku moja watakuheshimu na kukuomba msaada.
 
Pole sana ila kwa jinsi unavyoandika wala huna hio depression unayosema ; una disappointment kutoka kwa watu fulani fulani...
Depression huwa inaleta huzuni; kwenye maandishi yako hakuna huzuni mkuu, mpaka kujiua una safari ndefu sana!

Kikubwa mind your own business" Acha kusikiliza nani anasema nini juu yako, we only live once!! maisha yako yaishi kikamilifu, wenye matatizo makubwa kuliko yako wengi wapo...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…