Depression inaniathiri, nakaribia kujiua

Mkuu pole Sana,hata Mimi huwa nachekwa na kudharauliwa kwa mambo mbalimbali lkn nachukulia poa,namwomba Mungu na kwa msaada wa Mungu nasonga mbele, maisha yanaendelea.
 
Nianze kwa kukupa pole mkuu,lakini Kwa mtazamo wa haraka haraka unaweza kufikiria kuwa hakuna njia ya kukabiliana na msongo wa mawazo kwa sababu hata iweje bili za umeme na maji zitazidi kuja, siku ndiyo ile ile ya saa 24 na kazi za kufanya zinazidi kuwa nyingi na majukumu ya familia yatazidi kuongezeka. Ukweli ni kwamba una uwezo wa kumudu kuukabili msongo wa mawazo kuliko unavyojifikiria. Kuelewa kuwa majukumu haya yote ni ya kwako na kuwa wewe ndiye mtu pekee wa kuyaweka sawa, ndio msingi wa kuanza kukabiliana na msongo wa mawazo. Kukabiliana na msongo wa mawazo kunataka uamuzi wa kuanza kuchukua hatua kimawazo, kihisia na kwa kujiwekea ratiba na hatua nyingine za kukabiliana na matatizo yako.



Kubaini Vyanzo Vya Msongo Wa Mawazo



Hatua ya kwanza kabisa ni kubaini vyanzo vya msongo wa mawazo katika maisha yako. Kazi hii siyo rahisi sana kwa sababu vyanzo hivi huwa sio vya wazi na ni rahisi kudharau mawazo, hisia na tabia ambavyo huwa ndiyo mwanzo wa kukupa msongo wa mawazo. Kwa mfano, unawezajua fika kuwa mara nyingi huwa upo katika wasiwasi mkubwa wa kukamilisha kazi ulizopangiwa katika muda uliopewa, lakini usijue kuwa tabia yako ya kuahirisha kazi ndiyo tatizo na si ukubwa wa kazi unazopewa.

Kubaini ni nini vyanzo vya msongo wa mawazo kwako, chunguza kwa ukaribu sana tabia, mwenendo na visingizio vyako. Kama hutokubali kuwa wewe mwenyewe ni mhusika katika kusababisha na kuvilea vitu vinavyokuletea msongo wa mawazo (Stressors), itakuwa vigumu sana kupamabana na tatizo lako la kuwa na msongo wa mawazo.

Andaa kijitabu kubaini ni nini kinakuletea msongo wa mawazo na vipi huwa unakabiliana na hali hiyo. Kila wakati utakapopatwa na msongo wa mawazo, fuatilia kwa kutumia kijitabu chako. Ukifanya hivyo kila siku, utajifunza ni mambo gani yanakusumbua na yanavyohusiana. Katika kijitabu chako andika yafuatayo:

Ni nini kilisababishia msongo wa mawazo

Nilijisikiaje, kimwili na kihisia

Ulifanya nini kilipotokea

Ni hatua gani ulichukua kurudi kwenye hali yako ya kawaida



Chunguza Namna Unavyokabili Msongo Wa Mawazo



Ni muhimu sana kujua jinsi unavyokabiliana na msongo wa mawazo. Kama uliandika vizuri kijitabu chako, kitakupa picha nzuri ya jinsi unavyokabiliana na msongo wa mawazo. Njia nyingine ni nzuri na nyingine ni mbaya na kwa bahati mbaya watu wengi hukabiliana na tatizo hili kwa kutumia njia ambazo huongeza tatizo na si kulipunguza.


Njia mbaya za kuondoa msongo wa mawazo

Hebu tazama njia ambazo baadhi ya watu hutumia, njia ambazo hupunguza tatizo kwa muda mfupi na kulifanya tatizo kuwa kubwa zaidi baadaye:

Kuvuta sigara

Kunywa pombe sana

Kula sana au kula kidogo

Kukaa kwenye TV au kompyuta, saa nyingi sana

Kujitenga na marafiki, familia na shughuli

Kutumia vidonge

Kulala sana

Kuahirisha mambo

Kujishughulisha saa zote kuepuka matatizo

Kuwatulia wengine msongo wao (kubwatuka, kufoka, kupigana)

Jifunze njia nzuri za kuondoa msongo wa mawazo

Sasa chukua nafasi hii kujifunza baadhi ya njia nzuri ambazo unaweza kuzitumia kukabilina na msongo wa mawazo. Kuna njia nyingine nyingi tu lakini zote zinakudai uanze kufanya mabadiliko kimatendo. Kwa sababu kila mmoja wetu yupo tofauti na atakichukulia tofauti kinapotokea kitu cha kusababisha msongo wa mawazo, hakuna namna moja tunayoweza kusema ufanye linapotokea jambo fulani, hivyo basi itabidi ufanya utafiti na kuona ni njia zipi zinaleta mabadiliko kwako. Zingatia kile unachokimudu na utakochoona kuwa kinachokusaidia.

Kimsingi kuna njia kuu mbili; kubadili mazingira ya chanzo cha msongo ambapo unaweza kukikwepa au kukibadilisha na pili kubadilisha jinsi hatua unazochukua ambapo unaweza kubalika ili uendane nacho au kukabaliana nacho. Tutazielezea njia hizo za kuukabili msongo wa mawazo hapa chini:



1. Kukwepa Vyanzo Vya Msongo Wa Mawazo:



Si rahisi kukwepa kila chanzo cha msongo wa mawazo na ni vibaya kukwepa chanzo cha msongo wa mawazo ambacho inabidi ukikabili. Ukiwa makini utashangaa kuona uwingi wa vyanzo vya msongo ambavyo unaweza kuvikwepa.

Jifunze kusema hapana: Tambua uwezo wako wa kimwili na kikazi na zingatia kufanya kazi kulingana na uwezo ulio nao. Kuchukua majukumu zaidi ya uwezo ni chanzo cha kujipa msongo wa mawazo.

Wakwepe watu wanaoklsababishia msongo: Kama kuna mtu anakusababishia msongo wa mawazo kila wakati, punguza muda wa kukutana naye au vunja kabisa mahusiano naye.

Dhibiti mazingira mabovu: Kama habari za jioni za kwenye TV zinakukera, zimisha hiyoTV na kama msongamano wa magari kwako ni kero, chukua njia nyingine isiyo na msongamano hata kama ni ndefu zaidi.

Kwepa mada zinazokupa maudhi: Kama mada za dini au siasa hukupa maudhi, acha kushiriki kwenye mada hizo. Kama kila siku unalumbana na watu fulani kuhusu mada fulani, acha kuanzisha mada hizo au tafuta kisingizio cha kuondoka mada hizo zinapoanzishwa.

Chunguza ratiba yako: Itazame kwa kina ratiba yako, majukumu yako na kazi ulizojipangia kwa siku. Kama mambo ni mengi mno, yagawanye kwenye makundi ya yale ambayo ni lazima yafanywe na yale ambayo ni muhimu kufanyika. Yale ambayo si ya lazima sana yaweke chini kabisa kwenye ratiba au yaondoe kabisa.



2. Badili Mazingira ya chanzo:



Kama inashindikana kukwepa chanzo cha msongo wa mawazo, badilisha mazingira yake. Jaribu kufikiria ni nini cha kufanya ili chanzo hicho kisijitokeze tena hapo baadaye, hii inamaanisha kubadili namna yako ya mawasiliano au namna unavyoendesha shughuli zako.

Onyesha hisia zako: Kama kuna kitu au mtu anakukera, mweleze wazi kabisa kwa njia ya kistaarabu. Kama husemi, unajenga chuki na kuiacha hali ikibaki pale pale.

Usilee matatizo: Usilikalie lile linalokukera, liseme wazi na chukua hatua mara moja ya kulizuia. Kama una kazi muhimu ya kufanya na rafiki yako mpenda hadithi anaingia, mwambie wazi kuwa una kazi muhimu na kwamba unampa dakika kadhaa tu za mazungumzo.

Tumia muda wako vizuri: Kushindwa kutumia muda wako vizuri ni chanzo kikubwa cha kupata msongo wa mawazo. Unapokuwa umechelewa kukamilisha jambo lako, utalifanya bila utulivu na utakosa umakini. Lakini ukiwa na mpango mzuri wa muda wako, utafanya kila kitu mbele yako kiufanisi na bila kupatwa na msongo wa mawazo.



3. Badilika Kuendana Na Chanzo:



Kama huwezi kukibadili chanzo cha msongo wa mawazo, wewe badili mtazamo wako kuhusu chanzo hicho:

Kitazame chanzo kwa mazuri yake: Kitazame chanzo cha kero kwako kwa kutazama mazuri ambayo yanaweza kupatikana kutokana na chanzo hicho. Badala ya kulalamika na kukasirika kutokana na foleni ya magari, chukulia kuwa huo ndio muda mwafaka kwako kujipumzika au kusikiliza muziki unaaoupenda ndani ya gari yako.

Kuwa na mtazamo wa jumla: Litazame jambo linalokukera kisha jiulize kama ni jambo litakalokusumbua kwa muda gani, mwezi mmoja, mwaka na jee mwisho wa siku ni madhara gani yatakayotokea. Kama ni suala la mpito tu, elekeza nguvu zako kwenye mambo mengine.

Rekebisha viwango vyako: Moja ya sababu ya kujipa msongo wa mawazo ni kutaka kila kitu kiende sawa kwa kiwango cha hali ya juu. Usijiweke kwenye mtego wa kushindwa kwa kujiwekea viwango vya juu kiufanisi. Jiwekee viwango vinavyowezekana kwako na kwa wenzako na jifunze kukubali matokeo ambayo hayakufika kiwango lakini siyo mabaya.

Yakumbuke mazuri yako: Msongo wa mawazo ukikunyemelea, chukua muda kidogo kushukuru kwa yale yaliyo mazuri katika maisha yako, ikiwa ni pamoja na vipawa nyako vizuri na vyenye nguvu. Hili litakusaidia kukupa mtazamo tofauti wa mambo yaliyo mbele yako.



4. Kubaliana Na Yale Ambayo Huwezi Kuyakabili:



Vyanzo vingine vya msongo wa mawazo huwezi kuvibadili wala kuvizuia. Huwezi kukizuia kifo cha mtu wa karibu yako, wala ugonjwa mkubwa, au mporomoko wa uchumi wa nchi. Hapa inafaa kukubaliana na hali ingawa ni vigumu, lakini ni bora kuchukua msimamo huo kuliko kugombana na kitu usichoweza kukibadili.

Usijaribu kudhibiti kisichowezekana: Vitu vingi sana katika maisha yetu vipo nje ya uwezo wetu – hasa tabia za watu wengine. Kuliko kung’anga’nia na kugombana nao wabadili tabia, fikiria zaidi namna unavyoweza kuepukana na matatizo yao.

Tazama upande wa pili: Unapokumbana na vikwazo vikubwa, chukulia kuwa ni nafasi ya kujifunza na kukomaa. Kama ni maamuzi yako mwenyewe ndiyo yaliyokusababishia matatizo, chukua nafasi hiyo kutafakari na kujifunza kwa maamuzi yako ya baadaye.

Jifunze kusamehe: Lazima ukubali kuwa tunaishi katika ulimwengu wenye mapungufu mengi na kwamba binadamu kufanya makosa ni kawaida. Usiwe na hasira na chuki, jifunze kusamehe na kuendelea na mambo mengine.



5. Pumzisha Na Burudisha Mwili Wako



Mwili wako utapata uwezo mkubwa zaidi wa kukabiliana na msongo wa mawazo endapo utaulea kwa kupata muda wa kuupumzisha na kuuburudisha. Katika kuulea mwili wako unaweza kufanya yafuatayo:



Fanya matembezi

Pumzika kwenye bustani au sehemu zenye mazingira ya asili

Mkaribishe rafiki nyumbani

Pata kikombe cha chai au kahawa

Jishughulishe kwenye bustani

Soma kitabu kizuri

Sikiliza muziki

Angalia vichekesho

Cheza na mnyama uliyemfuga

Kuulea mwili ni jambo la lazima na si jambo la kujifurahisha tu. Katika kuyafanya hayo, jipangie kabisa ratiba yako na usimruhusu mtu au vitu vingine kuvuruga ratiba yako, huu ni muda wako wa kuurudishia nguvu mwili wako. Jichanganye na marafiki wenye mawazo mazuri, hao watakusaidia kuondokana na madhara yanayotokana na kuwa na msongo wa mawazo. Jaribu kuwa ni mtu wa kufurahisha na kufurahia mambo kwani kicheko ni dawa ya kuondoa msongo wa mawazo kwa njia nyingi.



6. Mazoezi Na Chakula Kizuri



Unaweza kuongeza uwezo wako wa kukabiliana na msongo wa mawazo kwa kujenga afya ya mwili wako.



Fanya mazoezi

Kula chakula kizuri

Punguza matumizi ya kahawa na sukari

Acha sigara, pombe na madawa

Pata usingizi wa kutosha

Katika ukurasa unaofuta tutaona jinsi ya kukabiliana na mfadhaiko (Depression) na katika kurasa zilizopita

Mungu akusaidie Sana mkuu,na mawazo mabaya yakuondoke
 
Ushauri mzuri.Kweli maisha yapo kasi,wengi tuangukia ktk msongo wa mawazo km mto uzi.Sasa hii ni hatari sana Kwani wengi huona maisha hayana maana tena na suluhisho ni kujiua au kuanza Kutumia madawa ya kulevya na kunywa pombe.
 
Unaonekana uko vizuri kiakili. Tumia hicho kipawa kuandaa maisha. Dunia ya Sasa hakuna kisichowezekana. Andaa maisha kwa kuongeza bidii masomoni na baadae kutafuta pesa kisha fanya unachohisi ni sahihi kurekebisha hayo masikio.

Chukulia hiki ni kipindi hiki Cha mpito just accept what is happening, the bullying,the laugh behind,...... whatsoever. You are a good and smart kid. Don't let other people to affect your life.
 
Kwa maelezo yako nimeamini kweli watu wa depression huwa wanatoa hisia zao kwenye keyboard kama vile kucheka n.k but ushauri wangu unaweza tumia muonekano wako kama mchekeshaji na ukapiga pesa tu muonekano ukawa fursa maana social media ndo zina bust sikuhizi mtu kama chiku mbalanga kafanya nini la maana isipokuwa social media bust
 
mkuu binafsi nina characters flani za ucheshi na hizo imoji za kucheka ni namna tu ya kujaribu kutoyachukulia serious ila kuna time nashindwa
 
Upumbavu tu.. watu wana magonjwa ya kudumu wanavumilia we masikio unataka ujiue mattako kabisa wewe
 
Ona wenzio mpaka wanazeeka na wanajivunia masikio yao. Wewe unataka yafanane na ya mtu fulani wakati yako ndio Mungu kaona ndio yanakufaa???. Kwani kuna mkamilifu? Kila mtu kawekewa challenge za aina yake duniani , sasa hayo masikio kwani ni kilema? Ungekuwa kiziwi je?
Je, Ungeambiwa chagua kuwa kiziwi mwenye maskio madogo? Au usikie kwa masikio makubwa ungechagua nini?

Wanaokucheka ni wajinga actually. Maana hamna mtu anajiumba , wote tumejikuta hivi tulivyo. Wewe soma, tafuta hela, ukitaka surgery haya ila unamkosoa Mungu.





 
Kadri unavyokua yanapungua ukifikisha miaka 25 utasahau kabisa kama uliwahi kua bullied sababu ya hayo masikio, maana mwili utakua mkubwa umejaa nyama nyama kwa hiyo hata masikio hayataonekana,

Mara nyingi watu wenye huzuni maisha mwao hupenda ku bully wenzao wakiamini wanapata ahueni ya matatizo yao muhimu ni kuwadharau na kusonga mbele,

Usijali kitu mdogo wangu, dunia ni nzuri sana huna haja ya kujiua sababu kufa kwako sio mwisho wa hao kubully wengine, wataendelea kwa hivyo kifo chako hakitakua na maana.

Wewe ni Shujaa.
 
Pole na hongera ndugu kwa changamoto. Pole kwa sababu imekuwa ni mzigo kwa muda sasa. Hongera kwa sababu bado naona unaweza kucheka na kutabasamu licha ya hayo. Nianze kwa kusema ACHANA na wazo la kujiua. Kanuni moja ya maisha ni kuwa unaweza kugawa MAMLAKA yako kwa watu wengine kama UTAKUBALI furaha yako iongozwe na maoni waliyonayo juu yako; au unaweza kutwaa na kutawala MAMLAKA yako kama UTAKATAA kuongozwa na nini wasemacho watu kuhusu wewe. By any means simaanishi ni jambo rahisi lakini kama njia pekee ya kufika kisiwani ni mtumbwi, woga wa maji si jibu bali ni lazima ukubali kuwa jasiri. Rafiki - UNAWEZA. Funga vioo. Wanadamu hawataacha kusema. Acha waseme. Cheka na uchukulie easy kama ulivyofanya kwa jamaa mmojawapo. Hiyo ndiyo pona yako. Jiwekee malengo ya maisha yako na kakamaa kuyaendea hayo - ije mvua, lije jua. ACHANA NA WANADAMU BWANA! Aliyekuumba anakupenda na yapo mengi aliyoweka ndani yako. Hata mtu akisoma namna ulivyoandika post yako, aliye makini anaona kabisa kichwa chako kinafanya kazi. USIMPE MTU USUKANI WA KESHO YAKO. SHIKILIA USUKANI WAKO NA USONGE MBELE. Umebarikiwa na Aliye juu. Hiyo ni hakika kabisa.
 
Mkuu nashukuru sana, nimejifunza kitu
 
Asante sana
 
Kuna dogo walikuwa wamepanga nyumbani alikuwa na masikio lakini sio Kama yako ya kwake yalikuwa yamebana na yaani Kama akivaa miwani kunakuwa hakuna sehemu ya miwani kukaa na alikuwa na akili sana kwa maana kwamba akifocus na kitu anakijua kweli, alipokuwa mdogo alikomaa na dini na akaijua haswa na alipoanza secondary alikomaa na elimu haswa na alikuwa very bright bahati mbaya kadri alivyokuwa anakuwa mkubwa akaanza kujishtukia kuhusu masikio yake, hali ambayo ilianza kumfanya akae nyuma ya darasa ili wenzie wasione masikio yake, ikafikia hatua mtu akawa akiwa mbele yake basi atasubiri apitwe ili mtu asimuone masikio yake hakuna mtu aliyejali kwao ikafikia hatua akaamaua kuacha shule akiwa form four licha ya uwezo mzuri darasanina kushinda kavaa mizura tu mpaka sasa yupo kitaa tu Hana Cha maana lakini angepata ushauri wa kueleweka asingekatisha ndoto zake. Kwa upande wangu nadhani ukifika umri Fulani wa balehe unakua Kama kijana unajali sana kuhusu muonekano hata mimi niliwahi pitia hali hiyo kutokana na machunusi usoni ingawa sikupata bullying Ila nilikuwa najishtukia naamini baada ya kipindi hichi Cha makuzi kupita utaona kawaida tu vyovyote vile ulivyo. Ukiendekeza hali hiyo utashindwa kabisa kutongoza kwa kukosa kujiamini.Tafuta kitabu kinaitwa four agreement by Don Miguel kitaiusaidia sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…