Depression inaniathiri, nakaribia kujiua

....sikufika ata hatua 20 nikakutana na kidem flani kikiwa na boyfriend wake...

Mbona hata wewe waonesha ni mtu mwenye kudharau watu wengine...!!!

Kitendo cha kutumia ngeli ya 'ki-vi' kwa mtu si sawa labda kama umemaanisha kudogosha...
 
Asante mkuu kwa kunitia moyo
 
Haha Asante mkuu kwa ushauri
 
Nashukuru sana
 
[emoji120][emoji120][emoji120] nashukuru sana mkuu ubarikiwe
 
Mbona hata wewe waonesha ni mtu mwenye watu kudharau wengine...!!!

Kitendo cha kutumia ngeli ya 'ki-vi' kwa mtu si sawa labda kama umemaanisha kudogosha...
Mkuu! Ni kwakua walinikwaza ndio maana nikatumia ngeli ya 'ki-vi' .. ni hasira tu
 
Utani wa kuitwa, goviiii goviii na wale wanaojambisha wazee wa busha, haya maisha Ni vita eti
 
Kuna watu hawana miguu hawana mikono lakini wapo vizuri tu. Unabidi wewe umshukuru Mungu kwa hali yako. Wewe unaweza kutembea na alafu uhitaji msaada wowote kwa watu wa kulishwa, kutembezwa na mengineo. Watu ni watu tu na siku moja wote tutabakia shapeless baada ya kufa. Wakikucheka wewe wapuuze na kuwapa tabsamu kubwa tu.
 
Kijana pole sana kwa hiyo changamoto unayopitia.Ushauri wangu ni kwamba wawe usijishtukie uonapo watu wanacheka.
Kwa vile bado uko shuleni soma sana na ipo siku hao wanaokucheka watakuja kukupigia magoti kukuomba msaada. Mwisho tambua tu kuwa mungu kamuumba kila mtu kwa mfanowe.
 
Pole sana mkuu. Be strong, kuna watu wanapitia makubwa kuliko hayo. Wewe jikaze, soon utapata hela zako,utafanya unachotaka.. Tafuta rafiki yako wa kweli wa shida na raha mueleze. Halaf uwe unajichanganya nae sehemu mbalimbali. Lakin pia ujasiri wa kuja kuyaongea haya hapa umeshayashinda
 
Vuta picha kuna mtu ana zaidi ya miaka 19 yupo kitandani mpaka muda huu na hajiwezi kwa lolote

Punguza focus kwenye masikio yako

Emoj zako haziendani na kichwa cha habari
 
Pole kwa unayopitia.... jitahidi kujichanganya na kupuuzia hayo maneno, pia jikubali.
 
Watu wenye depression wakati mwingine hawapendi kuwaonesha watu huzuni yao, anaweza kucheka na wewe vizuri akiingia ndani peke yake anaanza kulia
 
Afya ya Akili ni muhimu sana sio kitu cha kuficha unawaona Waganga mambo uanakuwa mazuri.
 
Aisee polee sana, jikubali jinsi ulivo ukishajiona wewe upo kamili na wengine watakuona hivo, usiache nafsi yako na mawazo yako yakutawale kuwa ww ni kiumbe mbaya, jipende, jithamini, kamwe usijidharau! Soma kwa bidii tafuta pesa utasahau yote hayo!! Diamond mwenyew alikuwa anaitwa domo kutokana na maumbile makubwa ya mdomo wake, lakini kwa sasa anaitwa lips denda au Sadala.... so weka pamba masikioni songa mbele!!! Ukijiua ujue moja kwa moja jehanamu.
 
Pole mdogo wangu! Najua nivigumu kuyakataa maumivu ya kushtukiza ila nikutie moyo mkuu- kumbuka MUNGU amekuumba kwa mfano wake kwahiyo usitingishike na kebehi za wenye mizaha! Alafu utambue hili kwamba hakuna kilichokamilika kisipitie testing hapo unajaribiwa tu ili ujikatae sasa wewe jikubali tena uwe proudly na ulivyoumbwa! Binafsi nina pua kubwa kuliko maelezo na nilichekwa sana na watu ila baadae pua hii hii ikampagawisha mutoto ya kizungu na ninaenjoy maana navuta oxygen yakutoosha!
Mtangulize MUNGU na usali uikatae hiyo roho ya kujikataa na kujiua! Hilo ni roho la mauti linakuonea wivu, linajua wewe ni nani baadae utakuwa nani na utawasubua katika ulimwengu wa kiroho! Sasa mkimbilie MUNGU na umpinge shetani naye atakukimbia!
 
Wapotezee , tu hap mkuu focus kwenye Ndoto zako Pamoja na malengo Tafakari kesho yako ungependa kuwa nani na wapi!.

Umenikjmbusha nilipo kuwa mdogo nilikuwa nataniwa "kichogo" kiukweli pamoja na utoto wa shule ya msingi lakini ile hali ilikuwa inanipotezea kjjiamini sana nakujihisi kama mtu mwenye kasoro kubwa..

Siku zimeenda hadi nimekuwa mtu mzima nashaanga structure ya skull imebadilika kabisa sioni tena kichogo😂
 
Binafsi kama utafikia uamuzi wa kwenda kufanya surgery na ukapata kiasi cha pesa nami nitachangia.

Wadau huyu mtu ameshapoteza confidence yote, suala lilikobaki ni kuyapunguza au aendelee kuwa kwenye depression.

Mbona matako ya plastic mnayafurahia huko katika mitandao ya picha??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…