Depression inaniua

Hili ni jema sana mdogo angu. Unakomaa komaa kwa busara. Nimefurahi
 
Sasa siwezi hata ongea nikisema neno nalia.
Usione aibu kwenda hospital mara bila kuchelewa. Ni hatari mno na kwa kuwa umetambua kuwa una depression basi kubaliana kuwa una hilo tatizo na linatakiwa lipatiwe tiba.

Je imeanza baada ya tukio gani? Kujifungua, kufiwa na mtu umpendaye kugundulika una ugonjwa fulani unaohisi unahatarisha maisha yako, talaka, pressure ya kazi?
 
Sawaa...ndio utulie sasa hiv, usije ukavagaa wachawi tukutoe kafara mbuzi
Eh kama yule mwana sasa mie sitolewi kafara kindezi nampango wakuwa na utajiri wakutoa wachumba zangu kafara kila anayelala namie anakufa isipokuwa huyu mtu atakayenioa .
 
Watu hupuuzia sana hii kitu DEPRESSION(Sonona)
Leo watu wakisikia mtu kajiua huwa wanaamini kitu kama hicho hakiwezi kuwatokea wao.
Ikiwa unadhani hivyo basi hujajua kwa undani hatari ya DEPRESSION.

Depression ni hali ya kiafya inayosababisha hisia za Mfadhaiko, huzuni, upweke, msongo wa mawazo na kukosa matumaini kwa muda mrefu. Ni zaidi ya kuwa na huzuni, narudia tena NI ZAIDI YA KUWA NA HUZUNI ya muda mfupi; inahusisha mabadiliko ya kisaikolojia, kimwili, na tabia.

Wataalamu huweka bayana dalili za Depression, Aina zake, na Tiba. Athari ya Depression huongezeka kadri mda unaokaa pasipo matibabu ya kisaikolojia.
Japo kuna kiwango unahitajika kufanya mabadiliko fulani tu ya masisha yako kama itakuwa haijakuathiri sana.
Kumbuka kujua kiwango kilichokuathiri ni pamoja na kujua Aina ya Depression ulionayo, Mda na Tatizo lililokuathiri.

Kwa kuandika hayo yote hapa haiwezi ikatosha bali unapaswa kutafuta msaada wa kitaalamu itakuwa njia rahisi zaidi.

ILA USICHUKULIE POA.
 


Asante sana mkuu kwa haya maneno yako yamenitia nguvu mno.

Kuna hali ya kukata tamaa naipitia kwa sasa.

Kuna mahali nilikuwa nafanya kazi ila kwa sasa nimeipoteza hiyo kazi kutokana na kupishana kauli na maboss, pia kuna kiasi cha pesa niliwekeza kwenye biashara fulani sh. Laki tano ili nipotezee mawazo ya kupoteza hiyo kazi ila pia na hiyo biashara imekufa bila kuingiza hata mia kama faida.

Yani mambo yote hayo yamefanyika kuanzia 24 Aprili 2024 mpaka wiki hii ya mwisho ya mwezi May.

Juzi kati nimekaa kitandani nimelia sana kama mtoto mdogo mana naona giza mbele yangu na mpaka sasa sijui kitakachofuata kwenye maisha yangu.

Ulichokiandika hakiwezi kubadilisha uhalisia wa ninayoyapitia ila atleast nimepata amani ya moyo kuwa hali hii nayo itapita.
 
Pole sana Mpendwa, ila naomba nikuhakikishie kuwa hilo nalo litapita, ni kweli sasa huoni mwangaza ila bado haimaanishi kuwa hapatakucha..!! Patakucha mpendwa, lazima pakuche, be strong please..!!
 
Pole Mbaga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…