Depression inaniua

Mkuu! Sio sawa unajua
Elewa hali aliyonayo lovie na upotezee baadhi ya mambo
Muhimu wote tuwe na furaha, usiandike maneno ya kuumiza hivi.
 
Maisha yana milima na mabonde. Juzi nimeenda hospital kutibiwa ,aseeeee lile nyomi la wagonjwa nililolikuta pale hospital ni hatari sio kidogo.

Halafu daktari anakuambia mbona Leo wagonjwa ni wachache.

Hakuna kukata tamaa ,jipe moyo utashinda
 
Lovelovie unapitia kitu kinaitwa wanaume wa jf umiza ubongo. Hawajui wanataka nini kila daily wanakuaminisha humu kuna ndoa ila humu hakuna ndoa . Ila hawasemi wengi ni mariooo tu nawanakupiga na vitu vizito hadi unazima kimaukweli ushauri wangu kunywa maji mengi anza na kusali muombe Mungu msamaha umrudie yeye anaweza na anajua unapitia nini msirikishe ita roho mtakatifu akusaidie uweze kupata njia ile sahihi kwako atakuja wakwako hatojali wewe ni single mom .Good day usimshirikushe mtu wewe loa ba Mungu wako anatosha abafariji kuliko mtu yeyote.
 
Mimi nikiwa na stress huwa natembelea hospital nikitoka hapo natoka na nguvu mpya kabisa maana nakutana na mtu ana umwa wa leo na kesho ila ana tabasamu najikuta ni mjinga narudi kupambana tena.

Unaona maneno hayo? Kila mtu inabidi ajue ni kitu gani kinamntanyua au kumrudisha kwenye hali ya kawaida pindi anapokua na nyakati ngumu.

Bila shaka Lovelovie akisona andiko lako ataacha kulia na kutaona maisha katika mtizamo tofauti.
 
Sio kila changamoto ni ya kimahusiano mkuu. Hata mimi nilidhani kaumizwa kihisia, ila hakuna kitu kigumu kwa mtu mzima kama kuyumba kiuchumi.
 
Mkuu! Sio sawa unajua
Elewa hali aliyonayo lovie na upotezee baadhi ya mambo
Muhimu wote tuwe na furaha, usiandike maneno ya kuumiza hivi.
Hii inaitwa Double standard toka kwako,

Vipi yeye kunijibu mimi kifedhuli kua nibalehe nitoke Nyumbani alikua sawa? Ulifurahia yeye kuniambia hivyo? Kwanini yeye hukumwambia kua kuniambia vile ilikua ni dharau na sio sahihi tena kwa mtu usiyemjua? Mimi nampokea mtu kama anavyokuja,alileta lugha ya kejeli kwangu ikabidi na mimi nimpokee kama alivyokuja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…