Depression Itaniua

Kama ulikopa kwa dhamana ya mshahara naamini mkopo una bima hivo bima itacover mkopo wako sababu shida mojawapo ni kupoteza kazi ndo bima huingilia kati. Mkopo wako hauhusiki na nyumba. And ukiona ishu mbaya ingia mkataba hata na ndugu yako kuwa umeuza nyumba ainunue ili bank wakose cha kuuza then pangisha nyumba yako wakulipe kodi ya mwaka halaf wewe tafuta nyumba ya vyumba 2 sebule lipa mwaka then hela inayobakia fanyia biashara ndogondogo. Nakushauri status weka pembeni piga hata bajaj ama boda hautojuta, mama mfungulie genge la mamalishe lililoenda shule
 
Kama ulichukua Mkopo Bank kwa Udhamini wa Mshahara wako iweje Bank waje wauze Nyumba yako??Dhamana yako wewe ni Ofisi ndio iliyokudhamini hivyo Bank hawawezi kuwa na Hati ya Nyumba yako
Sidhani kama kasema Bank ndio wanataka kuuza nyumba, alichosema hao Bank ndio wanamshauri aweke chochote kama dhamana aepuke kuingizwa kwenye black list.

Ni yeye ndio anawaza kuuza hiyo nyumba yake.
 
Ofisi yako ilikudhamini manake hawakutakiwa kukufukuza kazi hadi urejeshe mkopo na kama wamekufukuza basi wanapaswa kulipa wao. Fuatilia hili swala kisheria na usipaniki kabisa naona ofisini ndio kuna makosa.
 
Benki wanakudai PESA NGP?Nyumba yako ni dhamana?Nyumba yako iko kwa jina lako?
 
Jambo kama hili sio rahisi sana kukutana na ushauri makini kutoka kwa Mtu ambaye hajawahi kupitia hayo.

Mimi siungani na wanaosema usiuze nyumba kama haswa ndio itakayokusaidia kuishi kesho.

Iwapo utajiridhisha ya kuwa kuna pesa nzuri unaweza kuipata kwa kuuza nyumba basi weka mipango yako mezani mapema ujue utafanya nini kwa kiasi unachokitarajia.

Na iwapo utachelewa sana kufanya uamuzi basi kuna hatari ya kulazimika kuuza nyumba ukiwa na presha kubwa ukaishia kuiuza hata kwa robo ya thamani halisi ya nyumba yako.

Kwenye maisha kila dakika moja iliyopo mbele yako ina thamani kubwa, ndani ya dakika hiyo moja kuna ufumbuzi wa changamoto yako...hivyo fanya kila unaloweza kuhakikisha unaifikia hiyo dakika moja...na kwa kusema chochote basi hata kuuza nyumba ni moja ya hayo.

Sasa kipi bora, kukaa chini na kuangamia kwa depression ukaiacha familia au kuuza nyumba ukatafuta mlango wa matumaini?.

Wakati unasubiria kufikia uamuzi wowote ni vizuri wewe na Mkeo mkaanza kufikiria cha kufanya kuingiza chochote hata kama ni shughuli ya chini kama kupika vitafunio, mihogo, karanga n.k.

Unapopita pale Mbezi Luis ukawakuta wale wanaorundikana pale kuuza ubuyu na tambi wengi wamekutwa na hayo yaliyokukuta wewe ni vile tu huwezi kupita kwa kila mmoja na kumuuliza.
 
Ushauri mzuri
 
Pole sana mkuu kuzaliwa mwanaume ni shida ila shida zina mwisho wake AMINI HILO NAKUAMBIA
 
Kwa sasa naweza nisiwe na cha kukufariji, lakini nina nafasi ya kukwambia ukweli kwamba, pamoja na ugumu wa unayoyapitia, yatapita na kuwaacha wote mkiwa salama.

Siku moja yote yatabaki stori, na utakuwa sehemu ya faraja kwa wengine wanaopitia changamoto mbali mbali.

Asante.
 
Pole sana ndugu kwa changamoto ngumu unayopitia ninaamini utavuka salama ukiweka imani yako kwa Mungu.
Huna haja ya kupaniki kama dhamana ya mkopo wako ilikuwa kazi yako, hawawezi kuja kuuza nyumba maana hawana documents zako za nyumba.
Kingine tafuta kazi iliyo ndani ya uwezo wako ufanye, zipo kazi huhitaji kupeleka barua za maombi. Hasa kwa makapuni ya sales, uza bidhaa zao upate kamisheni zao.
Mfano unaweza ukawa na smartphone yako na ukasajili line za makapuni na ukapokea kamisheni, huu ni mfano tu.
Usikae nyumbani unasubiri kazi, tafuta kitu cha kufanya, hasa kile unachoona ni jepesi na rahisi kwako kutokana na mazingira yako na umri wako.
Asante sana.
 
niliwahi kupitia hiyo hali wakati fulani. depression ilinipeleka puta sana. pole sana ndg.

usijitenge oeke yako kwa maana ya kujifungia ndani ukiwaza, jichanganye na watu, tafuta watu wa karibu waeleze situation yako.
 
Ni kweli..na mimi nilipitia magumu lakini hakika yalipita..
 
Pole sana, mkopo wa Bank una bima, hivyo ondoa hofu, usiwaogope hao maafisa wa Bank, we waambie dhamana yako ilikua kazi hivyo kama huna kazi mkopo huo utakuwa written off, Nyumba acha ikuhifadhi tafuta namna nyingine ya kufanya, au hama mkoa nyumba pangisha
 
Hiyo Nyumba usiuze ila badirisha umiliki kutoka kwako kwenda kwa mtu mwingine ili bank wasije iuza

Hayo mengine ni changamoto tu za maisha utaweza kupambana nayo

Sent from my TECNO Camon CX using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…