Aaron Arsenal
JF-Expert Member
- Jul 24, 2014
- 24,501
- 28,711
[emoji818] Naam ilikuwa ni mwaka 2005, kwenye nusu fainali ya Uefa Champions League iliyozikutanisha timu kutoka jiji la Milan, yaani Ac Milan vs Inter Milan.
[emoji818] Game ya kwanza iliisha vizuri tu kwa Ac Milan kuitandika Inter kwa goli 2-0. Ila varangati lilitokea kwenye mchezo wa raundi ya pili.
[emoji818] Ukiachana na battle ya Kaka na Pirlo, dhidi ya Cambiasso pale kati, kwa upande wa mashabiki kulitokea vurugu kubwa hadi kusababisha refa Markus Merk kumaliza gemu kabla ya dakika 90.
[emoji818] Mechi ilianza vizuri tu huku Milan wakitangulia kupata goli la kuongoza kupitia kwa Andriy Shevchenko ndani ya kipindi cha kwanza. Lakini vurugu zilianza pale refa alipolikataa goli la kusawazisha la Cambiasso, na baruti zikaanza kurushwa uwanjani na kusababisha moto, zimamoto walijitahidi kuuzima moto uliokuwa ukisambaa ndani ya 18 za Ac Milan. Huku kipa wa Milan wakati huo Dida na yeye akirushiwa baruti iliyonasa kwenye shati lake na refa akaamua kuustopisha mchezo huo kwa muda na kuwaamuru wachezaji waende kwenye vyumba vya kubadilishia nguo mpaka hali itakapotulia
[emoji818]Baada ya dakika 10 za mapumziko wachezaji wakarudi uwanjani, lakini hawakumaliza hata dakika moja mashabiki wa Inter Milan wakaanza upya kurusha baruti uwanjani, refa akamaliza mchezo na Ac Milan wakapewa ushindi wa Magoli 3 na kwenda fainali ambapo walifungwa na Liverpool kwenye hatua ya penati baada ya comeback ya kihistoria