pwilo
JF-Expert Member
- May 27, 2015
- 10,913
- 13,876
Uhali gani shabiki na mpenzi wa soka wa Tanzania na Afrika Mahariki kwa ujumla baada ya mechi ya jana kumalizika bila mbabe baada ya kugawana alama? Kwenye mchezo huo matokeo ya haki kila timu ilistahili alama moja, ila kuna vitu kadhaa vilijitokeza kama ifuatavyo:
Heroes
Dickson Job: Moja kati ya wachezaji waliokuwa na utulivu wa hali ya juu jana waliweza kufika haraka kwenye hatari na kufanya maamuzi sahihi kwenye muda sahihi, bila Dickson jana Yanga wangelala na viatu.
Aziz Ki: Kwenye mechi kubwa kama ya jana ndiyo muda sahihi wa mchezaji mkubwa kuonyesha ukubwa wake na alifanya hivyo, alionekana kwenye matukio muhimu na alikuwa ndiyo mkombozi kwa upande wa Yanga baada ya kufunga goli la kusawazisha.
Kibwana Shomari: Jana alikuwa na utulivu wa hali ya juu na aliweza kuusoma mchezo mapema alipogundua mpinzani wake alikuwa na kasi akaamu kubaki timu inapokuwa inashambulia, ili kuendana na kasi ya mpinzani wake aliyekuwa na kasi na maarifa kuliko yeye.
Chama Jr: Mchezaji mbunifu na mwenye uwezo mkubwa na ni ngumu kutabiri atafanya nini kwa wakati gani, sehemu unayotegemea atapiga yeye atatoa pasi, sehemu unayotegemea atatoa pasi yeye atapiga na ndicho alichokifanya jana. Pasi sahihi katika wakati sahihi inaipa simba bao la kuongoza kutoka kwa Okrah the Magic.
Enonga Baka: Mashambulizi yote waliyokuwa wanatengeneza Yanga wanapokaribia eneo la Simba yeye alikuwa wa kwanza kufika na siyo kufika tu bali na kufanya maamuzi sahihi. Mipira ya juu ilikuwa chini yake upenyo wa pasi zote zinaishia kwenye himaya yake, bila yeye leo hii tungekuwa tunaongea mengine na lawama zingeenda tena kwa Matola.
Mzamiru Yasin: Kazi yake ilikuwa moja tu kuhakikisha mipango yote ya mashambulizi inayoanzisha na Yanga inaharibika na alifanikiwa. Kipindi cha kwanza Simba walitawala eneo la kati, kila mpango uliyoanzishwa na Yanga ulizimika kwenye himaya yake na Simba walikamata eneo la kiungo huku Mkude akicheza naye kwa karibu kupokea mpira pindi anaponyang'anya kutoka kwa mpinzani. Mashabiki wanataka apige pasi sahihi, Mgunda alitaka awe anatibua mipango ya mpinzani game plan yake ilifanikiwa.
Villains
Diara: Nilishawahi kusema kwamba kipa nambari wa Yanga hayuko sawa toka kuanza kwa msimu huu, ana makosa mengi madogo madogo ni vile tu timu yake huwa inapata matokeo katika Ligi Kuu ila zinapokuja mechi za ushindani huwa anakosa utulivu.
Ni uchoyo tu wa Okrah ila jana alistahili kuadhibiwa kwa makosa yake ya kuanzisha mashambulizi yasiyo sahihi wakati wanamiki mpira na kuna muda alikuwa anawafokea wachezaji wenzake baada ya kosa kosa.
Aucho: Aliyemuita Aucho daktari wa mpira atuombe radhi Watanzania. Jana alioneshwa namna ya kufanya transition mnapokuwa na mpira wakati timu inashambulia, alikuwa mzito kukaba na pasi zake nyingi zilikuwa hazifiki zinapostahili. Alimpa mzigo mkubwa Feisal na kuna muda alimfokea kwa kukosa utulivu na kufanya maamuzi yasiyo sahihi, kiufupi alipotea eneo la kati, alishindwa vita dhidi ya viungo wa Simba. Sure boy mechi ilimuhitaji.
Kisinda: Tanzania nchi ya ajabu sana, mchezaji akifunga mechi ya Derby au kutoa asisst ya goli basi hata ashuke kiwango vipi atalazimishwa acheze. Kiufupi jana hakuwa na athari yoyote zaidi ya kuwa na kasi ambayo haina faida, kwasababu alikuwa anakimbilia kwenye kibendera badala ya kuingia kwenye box na mipira mingi ilikuwa inatoka nje kwasababu inamshinda kasi. Faridi Musa Maliki alistahili kuanza.
Sakho: Kijana toka ashinde tuzo ya Goli Bora la CAF Champions League amekuwa anacheza kifaza, siyo Sakho yule wa msimu mmoja uliyopita. Anafanya vitu ambavyo havisaidii timu wakati huo timu inahitaji matokeo kama kupoozesha mashambulizi na chenga zisizo za lazima.
Anatakiwa abadilike, alistahili kwenda benchi mapema sana, hajisumbui kukaba hata timu inaposhambuliwa. Kibu Denis alistahili kuchukua nafasi yake, mechi kama ya jana kila mchezaji alitakiwa kukaba siyo kusubiria mpira tu. Asipobadilika benchi ni halali yake.
Jonas Mkude: Kuna muda alikata upepo kabisa na alikuwa anakaba kwa macho, kwani hata faulu ya goli la Yanga alilofunga Ki Aziz lilianzia kwake baada ya kukaba kwa macho Mzamiru akaingilia movi ikawa faulo. Alitakiwa amalizane na Aucho mapema sana match fitness ilichangia kwa kiasi kikubwa kukata upepo mapema.
Mchezaji ambaye hajacheza siku za karibuni kuanza kwenye mechi yenye temper kama ile na inayohitaji nguvu ilikuwa hamna namna baada ya Vladimir Putin (Kanoute) kuugua ghafla muda mchache kabla ya mchezo.
Okrah the Magic: Mechi ya jana ilikuwa kwenye himaya yake, angefanya maamuzi sahihi kwa wakati sahihi mechi ya jana basi matokeo yangekuwa tofauti na yaliyopatikana. Alikuwa na siku nzuri sana jana, ila nadhani temper ya mechi ilimmeza akataka amalize mechi mwenyewe bila mchezaji mwingine kuhusika. Hatimaye mechi ikaishia kwa sare, anatakiwa kubadilika. Jana ndiyo amethibitisha kuwa Mzungu alikuwa sahihi kugombana kwa ubinafsi wake.
NB: Juma Mgunda alimuonyesha Nabi panapovuja arekebishe mapema kabla ya kukutana na Waarabu, maana jana walikuwepo taifa wakifuatilia mtanange huo na kuna muda Nabi alikuwa amejiinamia kabisa baada ya mashambulizi ya mara kwa mara.
Alamsik.