Derby: Wataalamu wa lugha tunaomba hili neno mtuwekee Kiswahili chake vizuri

Derby: Wataalamu wa lugha tunaomba hili neno mtuwekee Kiswahili chake vizuri

I AM NO ONE

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2020
Posts
389
Reaction score
576
Huwa tunatumia sana hili neno katika mchezo wa mpira tukimaanisha (TIMU MBILI MASHUHURI ZA MJI MMOJA ZIKIKUTANA NA KUCHEZA PAMOJA) ndo tuna sema DERBY.

Sasa hili neno DERBY tumelizoea sana kanakwamba watu wengi wanaliona kama ni neno la Kiswahili kumbe Kiingereza.Msaada kwa anaejua kuliweka hili neno vizuri katika kiswahili chake.

From Longman Dictionary of Contemporary English, Derby - British English a sports match between two teams from the same area or city.
 
Kiswahili kisicho rasmi, wote wanaweza kuitwa 'watoto wa nyumbani'.
 
Hawakawii kuweka neno la Kiarabu, sababu tu za kidini. Mfano ni neno mubashara, kulikuwa na haja gani ya kuchukua neno jipya kutoka kwenye lugha ya Kiarabu?
 
Ni watani wajadi wanaotokea mkoa au mji mmoja,,Inter Milan VS AC Milan,Man Utd VS Man City, Simba VS Yanga,Atletico Madrid VS Real Madrid, Liverpool VS Everton,,,Lakini mnisaidie hii,,Vipi kuhusu Bayern Munich VS Borrusia Dortmund,Barcelona VS Real Madrid inaitwaje maana hii sio Derby coz hazitokei mji mmoja
 
Back
Top Bottom