Derby ya Ma ex wangu niliinjoi sana

marcoveratti

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2017
Posts
1,019
Reaction score
1,824
Ushakutana na zile meme wanasema "tunaangukia keki ya harusi ya ex wako kwa bei nafuu" [emoji23][emoji23]

Kwa tafrisi ya haraka ni wengi wetu hatupendi maex wetu watusue ..ni tunatamani wasotee kiasi kwamba wajute.

kwenye supper Sunday ya Jana ilikua vita ya ma ex wangu pale viunga vya white hart lane Tottenham dhidi ya West ham.

Wakati wengi wakiiona kama London Derby me bilikua naiona kama ex Manchester united coaches Derby José Mourinhol na David Moyes uso kwa uso

Mpaka dakika ya za 80 mzigo unasoma 3 mtungi Mosé yuko mbele

"Kwa nnavyo mjua mmi Mourinhol game ishaisha hii"- kimoyo Moyo

Dakika za 77 anachanga karata zale anamuinua game changer anatoka Fomals anaingi mkobgwe Manuel Lanzini

Enzi za Mourinhol wa Chelsea ni Michael Essien anapasha kwenye touch line,basi hapo kama ni kibanda umiza ni tuna hamisha Chanel nyingine,game ishaisha hyo!

Ila Mourinhol hyu dakika ya 80 anatoa Son anaweka Moura anapunguza kasi eneo la ushambuliaji na hajaongeza mkabaji, kwa hesabu ya haraka kwaacha West Ham warelax.


Tunarudi dimbani ndani ya dakika 10 José kashakula goli 2 ubao una soma Mourinhol 3-2 Moyes
" ingekua dakika bado nyingi Mou asinge toboa" jirani yangu wa kulia anafanya unajumu [emoji23][emoji23][emoji23]

Heeee!

Dakika za lala salama badi sekunde ipigwe filimbi ya mwisho Manuel Lanzini anapiga muaa! kama ule wa Paul Scholes 2008 anawadungua Barca pale matofali ya kuchoma.
Second ball ile anaiunga kama iliyo njee ya box imoooooo!!! 3-3 na game imeisha [emoji119][emoji119][emoji119].

Hahaha nikacheka, mpira ni mchezo katili sana [emoji119][emoji119][emoji119]

Sikufanya makosa kutimua hawa watu hawana jipya kwenye modern football mmoja kaishiwa mbinu mwingiune hadhi yake ni ya timu ndogo.. !

Itoshe kusema Mourinhol ni yule yule na Moyes ni yule yule mmoja kaishiwa mbinu mwingine hadhi yake ni ya timu ndogo!.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…