JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Akizungumza na kituo cha Clouds FM, Kamanda wa Polisi wa kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Ramadhani Ng'azi amesema wameanza uchunguzi kubaini sababu za dereva wa basi la Simba SC kuendesha basi hilo reverse (Kinyumenyume) wakati akielekea katika dimba la Mkapa kwenye mchezo wa klabu Bingwa Africa, Simba 0-3 Raja Jumamosi Feb 18/2023.
Kamanda huyo amesema iwapo itabainika alifanya hivyo kwa makusudi atapelekwa Mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake.
=================
Baada ya kusambaa kwa video mitandaoni ikionesha basi likiendeshwa kwa staili ya kurudi nyuma, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Ramadhani Ng'anzi amesema wanafanya uchunguzi wa tukio hilo kwa kuwa ni kinyume cha sheria
Amesema “Dereva anayeendesha kwa kurudi kinyumenyume umbali mrefu bila dharura yoyote na kwa nia ya kuwabughudhi watumiaji wengine anakiuka sheria za barabarani na anaweza kushtakiwa Mahakamani.”
Ameongeza kuwa “Tunafanya uchunguzi kwa kuwa unaweza kusema ni la Simba kumbe siyo lao ni la mtu mwingine, hivyo hatujamshikilia mtu yeyote kuhusu taarifa hizo.”
Video: Basi la Simba SC likirudi kinyumenyume