Tetesi: Dereva wa Kiwanda cha Kagera Sugar, atekwa huko Congo

njegere

Member
Joined
Nov 6, 2017
Posts
6
Reaction score
5
Habari jf,kwa taarifa za kuaminika kutoka kiwanda cha sukari kagera sugar,dereva wa kampuni hiyo bwana Ayubu ametekwa Kongo, ni km chache tu kutoka mpakan mwa Burundi na Congo,lkn pia kutoka alipotekwa mpaka kiwanda cha sukari kilipo alikuwa amebakiza kama km 5 kufika kiwandan,

Ayubu alitekwa siku ya alhamis tar 20/12/2017 jion,na kundi lililomteka bado halijafahamika maimai wamesema hawausiki,baadhi ya wafanyaki wa maimai wanafanya kazi kwenye kiwanda hicho kipya cha bwana seif Congo hivyo wanafahamiana vizur,

Watekaji wanataka $25000 ndio wamuachie lkn kiwanda mpaka sasa bado kinasua sua kutimiza,Ayubu katekwa akiwa kazini kwani alikua anapeleka mbegu ya mua Congo kwa ajili ya kupanda mashamba mapya,

Alipokua anatekwa wanajeshi wa Congo walikua mazingira ya pale na wao baada ya kuona tukio lile walijibishana kwa risasi na mwisho wanajeshi walizidiwa nguvu magaidi wakaondoka na mtanzania mwenzetu,
Kuna tetesi kua kiwanda kitapeleka pesa hiyo lkn haijulikan ni lin na magaid wametoa masaa tu vinginevyo watatuma kichwa chake, naomba tumuombee mtanzania mwenzetu arudi salama,

OMBI KWA BWANA SEIF.
Mwenye kiwanda cha kagera sugar ndio mwenye kiwanda hicho Congo,tunafaham unataka kujipambanua kimataifa lkn uwekezaji wa pale sio sawa kwa watanzania na wafanyakazi wako wa kagera sugar unao wapeleka kule kila mwezi kwa ajili ya kufufua kiwanda chako huko,

Kule ni hatari sana sababu mazingira Yale kuna makundi ya kigaid zaid ya 5 hivyo risasi ni nje nje,halipiti lisaa bila kulia risasi,wafanyakazi wako wanafanya kazi Kule huku nyuma mwanajeshi anamtumtu wa kumlinda,
Je! Wakienda kule unawapa risk allowance?

Nimeongea na wafanyakaz wako wa kagera sugar zaidi ya 10 walioenda na kurudi Kule wanasema hapafai hata kidogo kwani wamefanya kazi kwa mazingira magumu na ya hatar japo ni siku chache,,kwanini usisubir patulie ili uendelee na mchakato wako,

Mbona Tanzania bado tunauitaji wa sukari mkubwa why Congo? Kwann usiombe ujenge kiwanda cha sukari kingine Tanzania ili tupunguze gape lililopo la sukari,mh raisi Magufuri anasema Tanzania ya viwanda lkn wewe unaenda kuwekeza kwenye matatizo,[HASHTAG]#toroka[/HASHTAG] uje.

Hao wafanyakazi wanasema wafanyakazi wanapanda miwa mashamban kwa ulinz wa jeshi,wakija magaidi kazi inaisha mpaka patulie tena

Leo mfanyakazi wako katekwa lkn kuwajibika kumkomboa unasita why? Think twice brother,
CC@MWIJAGE

[HASHTAG]#MTIGANZI[/HASHTAG]
 


WaTanzania bana.....wacha uoga kijana. The higher the risk..the higher the returns! Wacha vijana wapambane.

Yaani jamaa aache kuwekeza huko Congo kisa kuna Mayi Mayi?

Otherwise nchi kama Iraq, Syria, Yemen, Libya nk..zisingekuwa na watu. Maana huko mabomu nje nje.... In fact nchi zenye Changamoto kama hizo ndo za kwenda maana hata mpunga wake umetulia.

Kipi bora? kugombana na JPM akuongezee elfu tano kwenye mshahara wa laki nne! au kwenda kwenye risk environment ila utengeneza decent income?

Kama ni kufa hata Tz (NCHI YA AMANI) wanakufa kila siku..kama siyo kipindupindu..Basi bajaji au pikipiki zitakuondoa.

Ushauri wangu: Vijana kuweni Tayari kutake risk katika maisha. Vinginevyo ugomvi wenu na JPM wa ajira na mishahara isiyokidhi mahitaji hautaisha!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…