Desemba 12, Siku ya Kimataifa ya Bima ya Afya Kwa Wote

Desemba 12, Siku ya Kimataifa ya Bima ya Afya Kwa Wote

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2021
Posts
1,147
Reaction score
2,008
Siku ya Bima Ya Afya Kwa Wote inalenga kuongeza uelewa kwa Jamii na Nchi kuhusu umuhimu wa kuwa na mifumo imara na endelevu ya afya na bima ya afya kwa wote kwa kushirikiana na washirika wa pande mbalimbali.

Pia inalenga kuhamasisha Serikali kufanya uwekezaji mkubwa katika sekta ya afya

Leo Tanzania inaadhimisha siku hii ikiwa ni Wiki moja tangu Rais Samia kutia saini Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote (Desemba 5, 2023) inayotegemewa kuweka msingi imara kwa Wananchi wote kuwa na Bima ya Afya itakayowawezesha kupata huduma bora za Afya mahali popote nchini kwa gharama nafuu
 
kukata BIMA huo ni uoga ma maisha !

je nisipoumwa hela yangu mnatudisha ?
 
Back
Top Bottom