Desemba inaisha kimya, Makalla, Waziri Mchengerwa walituahidi Mwendokasi njia ya Mbagala zitakuwa zimeanza

Nyakijooga

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2018
Posts
276
Reaction score
473
Siku kadhaa zimepita tokea baadhi ya viongozi mbalimbali ikiwemo wa Serikali pamoja na Chama cha Mapinduzi (CCM) walipotoa ahadi kwa wananchi kwamba usafiri wa Mwendokasi katika njia ya Mbagala kufikia Desemba utakuwa umeanza kutoa huduma, hata hivyo mpaka sasa kufikia (Desemba 20, 2024) hatuoni dalili za usafiri huo kuanza kama ilivyoahidiwa.

Katika marejeo ya kauli za viongozi ambao walitoa ahadi mbele ya umma na vyombo vya habari ni pamoja na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Amos Makalla.

Ambapo mnamo August 29, 2024 akiwa ziarani, Amos Makalla alisema kwamba kuna mabasi 200 yaendayo haraka yanayoyotarajiwa kuanza kazi katika barabara ya Mbagala.

Akizungumza wakati, akiwahutubia wananchi wa Mbagala katika mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa Maturubai wilayani Temeke, Makalla alinukuliwa akisema hivyo kwa msisitizo.

"Hii miundombinu ya barabara imekalimilika muda mrefu tangu nikiwa Mkuu wa Mkoa wa hapa (Dar es Salaam), nimefuatilia, niseme nisiseme? Mwenezi wenu nina habari nimefuatilia na wamenihakikishia wapo katika hatua ya mwisho kuleta mabasi 200 Desemba ili yaanze kufanya kazi," amesema Makalla.

Soma

Kufuatia kauli hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (Dart), Dk Athuman Kihamia alisema kwamba hayo ni maelekezo ya Serikali na kwamba yatatekelezwa kama ilivyoelekezwa.

Licha ya kiongozi huyo ambaye ni Msemaji wa Chama ambacho kinaunda Serikali, lakini pia Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa akizungumza September 2, 2024 alitoa maelekezo Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), kupata mabasi 500 ya njia ya mwendo wa haraka Mbagala ifikapo Desemba, ambapo alitoa siku 90 maelekezo hayo yawe yamefanyiwa kazi.

“Udart na DART shirikianeni kuhakikisha njia ya Mbagala inakuwa na mabasi 500 mpaka Desemba na kwa sababu njia imeshakamilika sitaki tena kusikia maneno ya michakato, nadhani mnanijua mimi sio mtu wa maneno maneno nataka vitendo zaidi,” alisema Mchengerwa

Soma

Katika udadisi ambao nimeufanya katika eneo hilo licha maelekezo hayo bado hatuoni jitihada za maandalizi au viashiria vya moja kwa moja vinavyoonesha ishara ya huduma ya usafiri huo kuanza kutola huduma ndani ya wakati ambao umesisitiwa na viongozi hao mbele umma.

Mazingira hayo yatupa mashaka kutupelekea kuwa na msukumo wa kutaka kuhoji juu ya uwajibikaji kauli hizi zilitolewa na baadhi ya viongozi wa ngazi za juu kimamlaka na kiutendaji ambao wapo kwenye nafasi za kuaminika.

Tunatamani kufahamu nini kinachokwamisha utekelezwaji wa maelekezo hayo? ieleweke wananchi tunapoona kimya bila jitihada zozote au taarifa rasmi za kuanza kwa huduma hizo, tunakuwa na shahku ya kutaka kujua mchakato huo umefikia wapi, ikizingatiwa zimebakia siku chache Mwezi (Desemba)uliohadiwa kuisha.

Itakumbukwa barabara hiyo kwa takribani miaka miwili imeonekana kukamilika kwa asilimia kubwa na tayari awali mabasi yalikuwa yameanza kutoa huduma kwenye njia hiyo lakini baada ya siku kadhaa huduma hizo zikasitishwa ikidaiwa kuwa ni kutokana na uhaba wa magari.
 
Wamesema kati ya February na March. Ikifika March watasema hadi June.
 
Barabara imeshaanza Kufa.... sikuhizi tunapita Tu kuanzia guta,baiskeli, bodaboda Hadi gari za taka
 
Si wanajua watanganyika mko bze na SIMBA na YANGA.
KAZI ni kipimo cha UTU
 
Weeeee!!!
 
Back
Top Bottom