Sodium
JF-Expert Member
- Feb 14, 2014
- 754
- 404
KAHANGWA: NAGOMBEA TENA UBUNGE WA KARAGWE 2015
Deusdedit Jovin Kahangwa utagombea tenaubunge Wilayani Karagwe? Naulizwa swali hilikila kukicha kutoka kila kona ya Tanzania. Hivyo, kupitia ukurasa huu, nimeamua kulijibu.
Natangaza rasmi kwamba, ifikapo Oktoba 2015, nitagombea tena ubunge wa Karagwe, kupitia Chadema. Tangazo langu lina msingi wake katika mambo sita: Kanuni, Wasifu, Ajenda, Timu,Utajiri, na Akiba ya Kura (KWATUA).
KANUNI ZA KIKATIBA ZINANIRUHUSU
Sifa za kikatiba kama zinavyotajwa katika ibara ya 67 ya Katiba ya Tanzania (1977) ninazo. Mimi ni raia wa Tanzania kwa kuzaliwa; ninao umri zaidi ya miaka ishirini na moja; najua kusoma na kuandika Kiswahili na Kiingereza; ni mwanachama wa chama cha siasa kiitwacho CHADEMA; na katika kipindi cha miaka mitano kuanzia tarehe ya uchaguzi kurudi nyuma nitakuwa sijawahi kutiwa hatiani katika mahakama yoyote kwa kosa lolote la kukwepakulipa kodi yoyote ya Serikali.
Pia, mimi sina ugonjwa wa akili; katika kipindi cha miaka mitano kabla ya uchaguzi nitakuwa sijapata kuhukumiwa na kupewa adhabu ya kifungo kwa kosa linaloambatana na utovu wa uaminifu; sikusudii kugombea kiti cha ubunge na Rais kwa mpigo; na kuna yamkini kubwa kwamba nitapendekezwa na CHADEMA kupeperusha bendera ya ubunge.
WASIFU WANGU UNAVUTIA
Kifamilia, nilizaliwa Aprili 16, 1972. Baba ni Jovin Kahangwa na mama Matilda Zimbeiya. Makazi ya familia yetu ni Kitongoji Katamobwa, Kijiji Kibona, Kata Kanoni, Wilayani Karagwe. Wazazi wangu ni raia wa Tanzania kwa kuzaliwa.
Katika familia hii, kuna watoto 11, wote tuko hai, na kila mmoja ameanzisha familia yake, isipokuwa watoto watatu wa mwisho.
Kielimu, nimesomea taasisi zifuatazo:
Shule ya Msingi Kibona, Karagwe (1981-87); Seminari ya Katoke, Biharamulo (1988-91); Sekondari ya Tambaza, Dar es Salaam (1992-94); na Chuo Kikuu Dar es Salaam (1995-98).
Tambaza nilisomea Fizikia, Kemia na Hisabati (PCM). Na Chuo Kikuu nilisomea shahada ya Tekinolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).
Kiajira, nimefanya kazi zifuatazo:
Ualimu katika Shule ya Mtakatifu Anthony, Dar es Salaam (1999); Usanifu wa Programu za Kompyuta katika kampuni ya CATS (T) Ltd, Dar es Salaam(2000); Ualimu katika Shule ya Shaaban Robert(2001); Uhadhiri katika Chuo cha LearnIT, Dar esSalaam (2002-03); Usanifu wa Programu za Kompyuta katika kampuni ya Simu (TTCL), Dar es Salaam (2003-2008); Uhadhiri katika Chuo cha IIT, Dar es Salaam (2009-10); na Ualimu katika Shule ya Karaseco, Karagwe (2013-14).
Kiuongozi, tangu 2007 nimekuwa Mkurugenzi wa Hexadecalogue Ltd ya Dar es Salaam. Kampuni hii inajishughulisha na ushauri, utafiti, upangaji,uendeshaji, na usimamizi wa miradi ya TEHAMA.
Pia, kwa miaka 10 iliyopita nimekuwa mjumbe wa Bodi ya Taasisi ya Umoja wa Mataifa Tawi la Tanzania (UNA Tanzania) yenye ofisi zake Dar es Salaam.
Kidini, mimi ni Mkatoliki kwa kuzaliwa. Nilibatizwa, kupata kumunio, kipaimara na kurudia maagano ndani ya Parokia ya Rwambaizi, Jimbo la Kayanga.
Nilipokuwa kidato cha tano Tambaza, nilikuwa Katibu wa TYCS katika Jimbo Kuu la Dar es Salaam. Nilipokuwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam nilikuwa Katibu wa IMCS Kanda y aTanzania. Na tangu wakati huo nimekuwa natekeleza utume wangu kama Mlei kupiti chama cha kitume cha CPT.
Kiuandishi, tangu 2003 nimekuwa mwandishi wa magazeti ya Tumaini Letu, Rai, Mtanzania, Tanzania Daima, na sasa Mawio. Pia nimeandika vitabu viwili, Ilani ya Uchaguzi inayojali(1995) na An Empowerment Election Manifesto (1995) kupita kampuni ya uchapaji ya Ruvu Publishers,Dar es Salaam.
AJENDA INAYOGUSA MAISHA YA WATU
Kisera, ajenda yangu kuhusu Karagwe Mpya inavyo vipaumbele vitano muhimu. Napigania afya bora, elimu bora, itikadi ya ubinadamu ambayo ni msingi wa utawala bora, oikonomia bora, na uchumi bora. Hii ni ajenda inayoongelea Afya, Elimu, Itikadi, Oikonomia, na Uchumi. Vokali tano za a-e-i-o-u ni njia rahisi ya kuvikumbuka vipaumbele hivi.
Neno oikonomia linahitaji ufafanuzi. Kwa mujibu wa Mkusanyiko wa Mafundisho ya Kanisa Kuhusu Jamii(2006), kifungu cha 248, neno oikonomia linamaanisha usimamizi wa mambo ya nyumbani.
Msimamo wangu ni kwamba, hatua za makusudi za kisera lazima zichukuliwe ili kukuza na kuhami haki za familia, taasisi ambayo ni kikonyo cha taifa zima.
TIMU NZURI YA KAMPENI
Ninayo timu ya kampeni ya ushindi. Chadema ya Karagwe tayari imeenea kama taasisi kuanzia wilayani, katani, vijijini mpaka vitongojini. Kuna vijana, wanawake, na wazee walio tayari kukifia chama kila kona.
Kwa sehemu kubwa, Kamati za Utendaji wilayani na katani, haziyumbishwi na upepo wa siasa za tumboni. Red Brigedi nayo sasa ni imara. Karagwe hatusemani kwa mafumbo, hatupakani matope wala kupikiana majungu. Tunao umoja wa roho ambayo ni silaha ya ushindi.
UTAJIRI WA KUENDESHEA KAMPENI UPO
Uendeshaji wa kampeni unahitaji rasilimali zikiwemo fedha. Kuhusu jambo hili, tayari wapiga kura wangu 30,000 walionikubali mwaka 2010 wameahidi kunichangia buku buku kila mmoja.
Wasomaji wa makala zangu magazetini wameahidi kunichangia. Watu niliosoma nao Kibona, Katoke, Tambaza, na Chuo Kikuu wako nami bega kwa bega. Wana TYCS wote hawawezi kunitelekeza. Hata wafanyakazi wenzangu katika Kampuni ya Simu(TTCL) wananiombea usiku na mchana. Familia yangu nayo iko tayari kunichangia.
Hivyo, endapo nitateuliwa na chama changu kugombea ubunge, uwezo wa kuchangia gharama za kuendesha kampeni kwa wastani wa 33% ninao. Sehemu inayobaki chama kitamalizia.
AKIBA YA KURA ZA MWAKA 2010
Mbali na sababu zilizotangulia, kuna ukweli kwamba mwaka 2010 nilipata zaidi ya 30,000 ya kura zote. Hii ni sababu muhimu katika uamuzi wangu kwani kura hizi bado ziko hai. Kura zote zilihesabiwa kwa zaidi ya siku tatu. Mabomu na risasi za moto vikapigwa.
Hatimaye zikatangazwa 36% kama kura zangu. Mimi na wapiga kura wangu hatukuridhishwa na tangazo hili. Tuliibiwa. Kwa sababu ya uchungu wa kuibiwa ushindi, watoto wengi waliozaliwa siku hiyo waliitwa Kahangwa. Leo kuna Kahangwa Watoto wengi Karagwe. Hivyo, jina Kahangwa tayari limejisimika mioyoni mwa wapiga kura wengi wa Karagwe.
Kutokana na yaliyosemwa hapo juu ni wazi kwamba, kama uchaguzi ni nyumba, basi Kahangwa nimekwisha fika kwenye linta wakati wenzangu ndio wanachimba msingi. Kama uchaguzi ni riadha, basi Kahangwa nimekwishafika kati kati ya uwanja wakati wenzangu ndio wanaanzia golini.
Hivyo, mapambano yaliyopo leo kati yangu na watia nia wengine ni sawa na mapambano kati ya sungura na tembo kama sio mapambano kati ya kichuguu na mlima! Watabaki ni wasindikizaji rafiki tu.
HITIMISHO
Hivyo, ni wazi kwamba, kuhusu Ubunge wa Karagwe, Mwaka 2015 ni Zamu yangu Kahangwa. Naomba uniunge mkono kwa mawazo, kwa maneno, kwa vitendo, na kwa rasilimali kupitia barua pepe deus.jovin@gmail.com na simu namba 0758-341-483.
Chanzo: Ukurasa wake wa Facebook