Deusi Kibamba:Kuna njama kutaka Bunge la katiba lisionyeshwe "live"

Deusi Kibamba:Kuna njama kutaka Bunge la katiba lisionyeshwe "live"

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba,bwana Deusi Kibamba amesema kuna njama zinafanywa ili Bunge la Katiba lisionyeshwe "live" kwa wananchi.

Bwana Kibamba amesema jambo hilo halikubaliki.

CHANZO:ITV

MY TAKE:
Hii ni dalili ya wazi kuwa kuna watu(kundi) limejipanga ama kuhujumu au kuteka mchakato wa kupatikana katiba ndani ya Bunge la Katiba.
 
Washindwe na walegee hawa mizigo chakavu. Tanganyika tunaitaka na serikali 3
 
Hilo jukwaa la katiba limeundwa na kufadhiliwa na chadema ili kukwamisha upatikanaji wa katiba mpya..
 
MACCM yanataka kuficha madudu yao wanayotaka kuyafanya ili kuhakikisha katiba mpya ni ile ambayo wao wanaitaka ya kuwawezesha kuitawala Tanzania milele.
 
Kama watumishi wa serikali wamehujumu operation tokomeza kwa makusudi
si ajabu wakataka kuhujumu hata zoezi hili la katiba.
Natamani mh.rais kama amekusudia kutuachia katiba mpya pindi atakapostaafu basi aahakikishe zoezi hili linasimamiwa kikamilifu na kwa ukaribu.akiwaachia wetendaji wake tu,watamhujumu kama kwenye operationi tokomeza.
 
Rais alishawaambia ccm wenzake kwamba xWAJIANDAE KISAIKOLOJIA! wenyewe hawakumuelewa!
 
Mi nafikiri bunge likionyeshwa live itapunguza upotoshaji wa habari,kama watu hawataona live wataamini
lolote watakaloambiwa na yeyote atakayekuwa bungeni na hili linaweza kutuvuruga.
Tuondoe woga wa kuwaogopa wajumbe wapya kwa misingi ya kwamba watamwaga hoja nzito hadharani na kuwafanya wapiga kura kwenye majimbo kubadilisha misimamo pindi ifikapo 2015.
Dawa siyo kutoonyesha bunge live,dawa ni kila mmoja kuwa makini anapochangia na kuchangia mswada kwa faida ya watanzania wote.
 
Tushazoea ubabe, kwanza bila ubabe hiyo katiba isingekuwepo
 
Tatizo la ccm siku hizi siri zao zinavuja mapema sana,cjui wamechanganyikiwa kwa kuona watanzani wengi hawatishiwi nyau tena?

Wafanye yote ila tathimini ya uhai wao ni 2015,haina haja ya kuwapima kwa mizani ya gunia au ya bucha bali mizani ya wananchi;wazuie kuonyesha live or recorded ila kichapo chao kiko pale pale
 
Back
Top Bottom