Dhamana chanzo cha chuki katika jamii

Dhamana chanzo cha chuki katika jamii

evergreen juggle

New Member
Joined
May 28, 2024
Posts
2
Reaction score
3
Kumekuwa na tabia ya kuchukiana na kuanzishiana migogoro isiyokuwa na ulazima katika Jamii zetu.

Migogoro hii imekuwa baina ya ndugu,rafiki,majirani na wakati mwingine hadi kwa wazazi

Ni vema Jamii ikafahamishwa na kueleweshwa kuwa DHAMANA ni jambo la hiyari ama hisani na sio HAKI ya m uombaji

Tunaposhindwa kuwadhamini ndug ama watu wetu wa karibu wanatuona tuna roho mbaya na hatuna ushirikiano.

Ukweli ni kuwa kuna baadhi ya watu hatupendi kusikia kabisa wala kujihusisha na kitu kinachoitwa MIKOPO hasa hii ya mitaani.

Mkopo uchukue wewe kwa mahitaji YAKO kisha msongo wa mawazo na misukosuko ya kulipa madeni yasiyonihusu nipambane nayo mimi.

Tafadhali tusilazimishane kusainishana mikataba yenye mfanano na ile yakina Chifu Mangungo. Ifahamike kuwa tunadhoofishana afya.
 
Back
Top Bottom