The Infamous
JF-Expert Member
- May 11, 2009
- 731
- 121
Kuna mfumo mpya umeanzishwa na vyombo vya usalama na sheria ( mahakama na polisi) nadhani unaweza kuja shika mizizi kama usipopigiwa kelele mapema. kumezuka tabia ya kukamata viongozi hasa wa kisiasa na dini aitha wawe wanamakosa au hawana, kutengenewa kesi ambazo mlengo wake ni kawanyima dhamana. kosa halina mashiko lakini kwa nguvu zote wahusika wanahakikisha mtuhumiwa hapewi dhamana, eti kwa masilahi ya umma. kimsingi mimi binafsi nachukia sana huu mfumo kwani ni kinyume kabisa na KATIBA. Na hii inadhihirisha ni namna gani taasisi fulani hazitaki kwa makusudi utii wa sheria...
tabia hii haijengi na wala haiwaongezei wananchi uoga, bali chuki na hasira zinazojikusanya na kusubiri kulipuka. Kwa kiongozi mwenye weledi na upeo wa mungu( HEKIMA KAMA ZA MFALME SULEIMANI) hili tabia ni ya kukemea.
Nachukia watawala waonevu, hakika moto wa jahanam ni wao.