Dhamana ni haki ya kikatiba

The Infamous

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2009
Posts
731
Reaction score
121
Kuna mfumo mpya umeanzishwa na vyombo vya usalama na sheria ( mahakama na polisi) nadhani unaweza kuja shika mizizi kama usipopigiwa kelele mapema. kumezuka tabia ya kukamata viongozi hasa wa kisiasa na dini aitha wawe wanamakosa au hawana, kutengenewa kesi ambazo mlengo wake ni kawanyima dhamana. kosa halina mashiko lakini kwa nguvu zote wahusika wanahakikisha mtuhumiwa hapewi dhamana, eti kwa masilahi ya umma. kimsingi mimi binafsi nachukia sana huu mfumo kwani ni kinyume kabisa na KATIBA. Na hii inadhihirisha ni namna gani taasisi fulani hazitaki kwa makusudi utii wa sheria...

tabia hii haijengi na wala haiwaongezei wananchi uoga, bali chuki na hasira zinazojikusanya na kusubiri kulipuka. Kwa kiongozi mwenye weledi na upeo wa mungu( HEKIMA KAMA ZA MFALME SULEIMANI) hili tabia ni ya kukemea.

Nachukia watawala waonevu, hakika moto wa jahanam ni wao.
 

Sio hapa tz
 
viongozi wengine wa dini kama Ponda, bora wakae ndani tu hadi watakapokufa.....we huoni kumetulia kidogo
 
Serikali ya ccm inazidi kujiharibia kila siku kadri muda unavyokwenda, wanazidi kuwajaza wananchi hasira, they're failing at each and every move they make.
 
viongozi wengine wa dini kama Ponda, bora wakae ndani tu hadi watakapokufa.....we huoni kumetulia kidogo


mkuu tatizo la hili ni kwamba litajemga mazoea, itakuwa kitu kidogo wana refer kesi ya ponda, hivyo itapelekea watu kukosa haki kabisa. Kwanini waogope kutii sheria? tatito ni kwamba watu wanafanya mambo kwa kukomoa, lakini mwisho wa siku haitawasaidia kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…