Dhambi kitu kibaya sana! Adhabu ya kwanza ni kukutoa ulipo na kukuvua nguo!

Dhambi kitu kibaya sana! Adhabu ya kwanza ni kukutoa ulipo na kukuvua nguo!

Morning_star

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2018
Posts
6,042
Reaction score
17,320
Mara tu ukishatenda dhambi yoyote! "You will never be same"! Inakutoa hapo ulipo na kukuvua ngua na kuwa uchi.

Mwanzo 3:1-24!

Mara tu Adamu alipotenda dhambi, alitolewa na kutupwa nje ya bustani ya Eden na kuvuliwa nguo! Hakuna cha kusubiri!

Hata wao akina Adam na Awa walishangaa saana! Walijikuta wako nje ya bustaji nzuri ya Eden tena wako uchi! (Wakijionea aibu wao wenyewe).

Hii ni kanuni ya dhambi! Dhambi yoyote ukiishaitenda inakutoa mahali pazuri ulipokuwa na kukuhaibisha! Kama ulikuwa katika ndoa uwe na uhakika migogoro ya ndoa inaanzia hapo!

Ukiiba kazini uwe na uhakika utaondoka katika ajira na uhaminifu wako kwa bosi na wafanyakazi wenzio unaondoka kuanzia hapo hata kama hawajakuona!

Hivyo hivyo katika nafasi ya yoyote uliyokuwepo! Na ni vigumu kurudi katika nafasi hiyo labda Yesu akurudishe! Shetani anaweza pia kukurudisha ila kwa kusudi la shetani ndo maana nasema :hutakuwa tena mtu wa kawaida". It is total destruction! Ogopa dhambi!

Ujumbe wa leo!
 
Back
Top Bottom