Dhambi ni Nini

John Magongwe

Member
Joined
Jan 4, 2024
Posts
71
Reaction score
119
Dhambi ni Nini
Dhambi ni tendo, hisia, au wazo lolote linalopingana na viwango vya Mungu. Inatia ndani kuvunja sheria za Mungu kwa kutenda mabaya, au ukosefu wa uadilifu, kwa maoni ya Mungu
. (1Yohana 3:4; 5:17). Biblia pia inaeleza kuhusu dhambi ya kutofanya lililo sawa ingawa mtu anajua alipaswa kulifanya (Yakobo 4:17). Kwa kuwa Mungu ndiye Muumba, ana haki ya kuwawekea wanadamu viwango (Ufunuo 4:11). Tunawajibika kwake kwa matendo yetu (Warumi 14:12).

Inawezekana kuepuka kabisa kutenda dhambi
Hapana, haiwezekani. Biblia inasema kwamba, wote wamefanya dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu (Warumi 3:23; 1Wafalme 8:46; Mhubiri 7:20; 1Yohana 1:8).

Mwanzoni, wanadamu wawili wa kwanza, Adamu na Hawa, hawakuwa na dhambi. Sababu ni kwamba waliumbwa wakiwa wakamilifu, kwa mfano wa Mungu (Mwanzo 1:27). Hata hivyo, walipoteza ukamilifu wao walipomuasi Mungu (Mwanzo 3:5-6, 17-19). Walipozaa watoto, waliwapitishia/rithisha dhambi na kutokamilika (Warumi 5:12).

Kuna dhambi mbaya zaidi kuliko nyingine
Ndiyo, zipo. Kwa mfano, Biblia inasema kwamba watu wa Sodoma walikuwa “wabaya” nao walikuwa wakitenda dhambi “nzito sana” (Mwanzo 13:13; 18:20)

Kuna mambo yanayoamua uzito wa dhambi
Ubaya
: Biblia inatuonya tuepuke dhambi nzito kama vile uasherati, kuabudu sanamu, wizi, ulevi, unyang’anyi, uuaji, na kuwasiliana na pepo. (1Wakorintho 6:9-11; Ufunuo 21:8). Biblia inatofautisha dhambi hizo na dhambi zinazofanywa bila kukusudia, kama vile, maneno au matendo yanayowaumiza wengine (Methali 12:18; Waefeso 4:31-32). Hata hivyo, Biblia inatusihi tusipuuze dhambi yoyote, kwa vile zinaweza kutufanya tutende dhambi nzito zaidi (Mathayo 5:27-28).

Nia: Dhambi nyingine hufanywa kwa kuwa mtu hajui matakwa ya Mungu (Matendo 17:30; 1Timotheo 1:13). Ingawa Biblia haipuuzi dhambi hizo, inazitofautisha na kuvunja sheria ya Mungu kimakusudi (Hesabu 15:30-31). Dhambi zinazofanywa kimakusudi zinatokana na ‘moyo mbaya (Yeremia 16:12).

Kurudia dhambi: Biblia inatofautisha kati ya kufanya dhambi mara moja na mazoea ya kufanya dhambi kwa muda mrefu (1Yohana 3:4-8). Wale walio na ‘mazoea ya kutenda dhambi kimakusudi,’ hata baada ya kujifunza jinsi ya kufanya jambo linalofaa, hupokea hukumu kali kutoka kwa Mungu (Waebrania 10:26-27).

Wale walio na hatia ya kutenda dhambi nzito wanaweza kulemewa na uzito wa makosa yao. Kwa mfano, Mfalme Daudi aliandika hivi: “Makosa yangu yamepita juu ya kichwa changu; kama mzigo mzito, ni mazito sana kwangu” (Zaburi 38:4). Hata hivyo, Biblia inatoa tumaini hili: “Mtu mbaya na aache njia yake, Na mtu asiye haki aache mawazo yake; Na amrudie Bwana, naye atamrehemu, Na arejee kwa Mungu wetu, Naye atamsamehe kabisa” (Isaya 55:7).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…