Papaa Mobimba
JF-Expert Member
- Jan 27, 2018
- 882
- 3,337
WAFANYAKAZI wa The Guardian ambao baadhi hawajalipwa mshahara wa mwezi wa tano kutokana na matatizo ya kibiashara wameshangazwa na hatua ya meneja mkuu, bwana Srinivas Chintaluri kumnunulia gari ndugu yake Bw Balaji Balasubramaniyan ambaye ni Mkurugenzi wa Teknohama aina ya Toyota Sienta lenye thamani ya 13.5m/-.
Bw Chintaluri ambaye pia ni Mkurugenzi wa Fedha wa ITV na Radio One, amekuwa akiwalazimisha Watanzania wenye umri wa miaka zaidi ya 55 kustaafu na kuchukua mafao yako NSSF na baada ya hapo kuwapa mikataba kama vibarua kwa shabaha ya kupunguza gharama za uendeshaji.
“Haileti maana kampuni inashindwa kulipa mishahara, kodi ya serikali na michango ya NSSF kwa wakati lakini uongozi wa Chintaruli unamnunulia mtu ambaye kimsingi hana utaalamu wowote wa IT huku Watanzania wenye uwezo wakisitishiwa mikataba,” alisema mmoja wa wafanyakazi hao.
Wafanyakazi hao wanadai Bw Balasubramaniyan kama ilivyo kwa Mkurugenzi wa Biashara Ajay Goyal and Meneja Uendeshaji, Murugan Eswar ni miradi maalum ya Mkurugenzi wa Bonite Bottlers, Zoeb Hasuji ambaye kwa kushirikiana na Mkuu wa Ulinzi wa IPP Media, Ayoub Semvua wamekuwa wakifanya jitihada za kuwatafutia vibali vya kufanya kazi nchini pasipo na ujuzi wowote.
“Huyu Bw Balasubramaniyan hana utaalamu wowote wa IT, baada ya kuwafukuza kazi Watanzania vijana Dotto na Gaetano mwaka jana na kubaki na Allan Mshana, hali imekuwa mbaya kwani kazi zote zinafanywa na Mtanzania Mshana kwani huyo Mhindi hana kitu,” alisema mfanyakazi mwingine huku akitaka Ofisi ya Kamishna wa Kazi kuchunguza kama Wahindi waliopo The Guardian Limited wanastahili kuwepo.
Wamesema wakati kampuni inadaiwa kufanya vibaya kibiashara hali hiyo haionyeshwi miongoni wa Wahindi hao ambao wanaendelea kupeana mikataba minono ya kununuliana magari, kulipiana nyumba, ada za watoto, gharama za matibabu na likizo huku wakiwa himiza Watanzania wenye umri wa zaidi ya miaka 55 kwenda kuchukua mafao yao NSSF kwa lengo la kupunguza gharama za michango.
“Tunaomba sana Serikali yetu kuingilia kati jambo hili na kufanya uchunguzi wa kina kwa sababu hata vijana wa Kitanzania mikataba yao ikiisha wanalazimishwa kusaini mikataba ambayo ni kinyume cha sheria kwa kunyimwa matibabu na familia zao, kupunguziwa mishahara na kadharika,” walisema.
Mwaka jana, wafanyakazi hao waliandika waraka kulalamikia uwepo wa Wahindi wasio na sifa huku kazi zao zikifanywa na Watanzania ambao kwa sasa wamesitishiwa mikataba yao.
Wahindi waliopo wamesababisha Watanzania kupoteza kazi ni Bw Goyal, Balasubramaniyan na Eswar wakati Chintaruli anafanya kazi The Guardian na ITV kinyume na Sheria za nchi.
Kazi za akina Goyal, Eswar na Balasubramaniyan zilikuwa zinafanywa kwa ufanisi na Watanzania Kauthar De Souza na Moez Kaderbhai ambao waliacha kazi mwaka jana kwa mizengwe ya menejimenti.
Lakini cha ajabu ni kwamba, uongozi wa Chintaluri kwa kushirikiana na Hassuji walisitisha mkataba wa kijana mdogo wa Kitanzania, Avit Riwa ambaye alikuwa Mhasibu Mkuu mwanzoni mwa mwaka jana kwa madai ya mshahara wake wa 6m/- kuwa kubwa sana. Riwa ambaye ni msomi mwenye MBA na CPA, aligoma kupunguziwa mshahara. Mshahara wake ulijumuisha pango la nyumba na gari lake ambalo aliendesha mwenyewe.
Jambo la ajabu ni kwamba wakati Hassuji na wasaidizi wake wanafanya kila liwezekanalo kuwaleta Wahindi kufanya kazi TGL, kampuni imeendelea kufanya vibaya kibiashara kiasi kwamba wafanyakazi hawajalipwa mishahara kwa miezi miwili sasa huku pesa nyingi ikitumika kuhonga maafisa wa serikali ili kupata vibali vya kazi vya kuishi nchini na polisi ili kujinusuru na tuhuma mbalimbali za uhalifu zinazowakabili.