Dhambi ya uchaguzi wa Zanzibar oct 2015 Sasa yapamba moto UN

Kakke

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2010
Posts
1,883
Reaction score
1,482
CCM wanafanya hesabu hawapati jawabu hivi sasa na wakiangalia muda unatoweka kwa nguvu huku Jumuiya za kimataifa zikiwakodolea macho. Magufuli anaikimbia Ikulu ya Magogoni. Wengine wakipita Mkoa kwa Mkoa Tanganyika nao sasa wanawambia watu wao wapeleke madai katika Mahakama ya Afrika ya Mashariki wadai uhalali wa Muungano na kila Mkoa wasaini watu 300,000.

Sasa Tanganyika imeshajua na kuiona Hatari inayokuja mbele yake.

Wanatafuta pa kutokea hawapaoni, wanaomba ardhi ipasuke waingie wajifiche.

Baraza la Amani la Umoja wa Mataifa kupitia msukumo wa Liberal Party International hawasikii chochote ila haki ya Wazanzibari ya 2015 ipatikane.

Waziri wa Sheria na Katiba wa Tanganyika yuko Marekani kutafuta namna ya Kuiepuka kashafa hii nako imegonga mwamba.

Matumaini pekee sasa wanasubiri KIGODA cha Mwalimu Nyerere kisaidie nayo pia haiweze kani kwasababu walishampiga Joseph Sinde Warioba na huku Salim Ahmeid Salim ni mgonjwa haelewi tena kinachoendelea.

Iliyobaki sasa ni majuto na majuto ni Mjukuu. Walifanya haramu sasa wanajuta kwa hivo tutizameni hii cinema itaishia wapi. Lakini yajayo yanafurahisha.
 
Hakuna lolote mkuu.

Ila sio mbaya tukaendelea kujifariji.

Sent using Mikoyan MiG-29
 
Ni sababu mojawapo inayopelekea Mataifa ya Magharibi kutukwepa japo kutupa mkono wa salam!

Obama alikuja katika ziara yake binafsi tukajipendekeza kumtuma Foreign Minister eti akamsalimie huko huko mbugani maana mgeni asingeweza kuja kunywa chai bandari ya salama

Trump kamuita Uhuru akatete nae mawili matatu, sisi tumeomba lakini bado foleni haijafikiwa, naambiwa hata barua haijamfikia wala kufikiriwa pia tusahau!

Theresa May kapita hapo Nairobi juzi!

Nasikia suala za Zanzibar limetuweka pabaya katika diplomasia ya kimataifa, hao wakubwa huko katika dunia ya kwanza hawatuangalii vizuri kabisa na kwa bahati mbaya wale jamaa hawana dogo. Na sisi huku Tanganyika tunaendelea na siasa zetu za kiunafiki!

Karibuni Kijijini
 
Write your reply...Umeiokota wapi hii suala la Zanzibar limeisha mkutano 2020
 
CCM wanafanya hesabu hawapati jawabu hivi sasa na wakiangalia muda unatoweka kwa nguvu huku Jumuiya za kimataifa zikiwakodolea macho. Magufuli anaikimbia Ikulu ya Magogoni. Wengine wakipita Mkoa kwa Mkoa Tanganyika nao sasa wanawambia watu wao wapeleke madai katika Mahakama ya Afrika ya Mashariki wadai uhalali wa Muungano na kila Mkoa wasaini watu 300,000.

Sasa Tanganyika imeshajua na kuiona Hatari inayokuja mbele yake.

Wanatafuta pa kutokea hawapaoni, wanaomba ardhi ipasuke waingie wajifiche.

Baraza la Amani la Umoja wa Mataifa kupitia msukumo wa Liberal Party International hawasikii chochote ila haki ya Wazanzibari ya 2015 ipatikane.

Waziri wa Sheria na Katiba wa Tanganyika yuko Marekani kutafuta namna ya Kuiepuka kashafa hii nako imegonga mwamba.

Matumaini pekee sasa wanasubiri KIGODA cha Mwalimu Nyerere kisaidie nayo pia haiweze kani kwasababu walishampiga Joseph Sinde Warioba na huku Salim Ahmeid Salim ni mgonjwa haelewi tena kinachoendelea.

Iliyobaki sasa ni majuto na majuto ni Mjukuu. Walifanya haramu sasa wanajuta kwa hivo tutizameni hii cinema itaishia wapi. Lakini yajayo yanafurahisha.
Zambi ndio nini mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom