Abdul Nondo
JF-Expert Member
- Oct 28, 2016
- 520
- 2,930
Dhamira na malengo ya kufanya mchakato wa mabadiliko ya sheria za uchaguzi chini ya Serikali ya awamu ya sita ilikuwa ni kuboresha mazingira ya kiuchaguzi nchini kupitia mabadiliko ya Tume ya Uchaguzi ili kupata Tume huru ya uchaguzi ambayo viongozi wake wanapatikana kwa mchakato kupitia kamati ya usaili tofauti na awali Rais ambaye ni Mwenyekiti wa CCM kuwa na mamlaka ya moja kwa moja ya kuteua wajumbe na viongozi wa Tume bila kupitia mchakato wowote.Lengo ilikuwa ni kuepukana na changamoto zilizojitokeza katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 na uchaguzi wa serikali ya mitaa 2019 na chaguzi zingine za nyuma.
Sheria Na.2 ya Tume ya Uchaguzi ya 2024 iliundwa na vifungu vya 5(1) ,5(2)(b) na 9(1) vinaelezea mchakato wa kupatikana wajumbe wa Tume,makamu na mwenyekiti wa Tume kupitia mapendekezo na mchakato wa usaili unaofanywa na Kamati ya Usaili.
Hivyo wadau na Wananchi wote tulitarajia ya kwamba kuelekea uchaguzi Mkuu wa 2025,Kamati ya usaili ingeundwa kwani ndiyo yenye jukumu la kufanya mchakato wa upatikikanaji wa wajumbe wa Tume na kupendekeza Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti na hivyo mchakato wa kupata wajumbe wapya,Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Tume ungefanyika ili kupata Tume ya Uchaguzi yenye uhalali wa kusimamia uchaguzi kwa mujibu wa Sheria Mpya ya Tume ya Uchaguzi ya 2024 .
Badala yake Serikali ya CCM imetuzunguka watanzania ,Vyama vya siasa ,Asasi za Kiraia ,wanaharakati na viongozi wa Dini kwa kugoma kufanya mabadiliko madogo ya katiba ya 1977 ili kuondoa changamoto zote za kiuchaguzi badala yake sasa wanatumia katiba ya 1977 kulinda Maslahi na matakwa yao ya kiuchaguzi ,kama wanavyoitumia ibara ya 74(4)(a) inayosema viongozi wa Tume watadumu kwa miaka 5.Ibara hii wanaitumia kutetea kifungu cha 27 cha Sheria ya Tume ya Uchaguzi Na.2 ya 2024 kinachosema viongozi wa Tume wasasa wataendelea hadi muda wao kuisha ambapo viongozi wote wa Tume wa sasa wanamaliza muda wao 2026 na wengine 2028 baada ya uchaguzi. Hii inamaana ya kwamba hakuna mchakato wa wowote usaili wala mapendekezo kupitia kamati ya usaili kupata viongozi wapya wa Tume ya Uchaguzi kuelekea uchaguzi Mkuu wa 2025. Dhamira ipo wapi?
Tume hii hii ambayo ilisababisha uchaguzi wa hovyo 2020 ,kura feki, watu kufa Zanzibar na Bara, walioshinda kuporwa, maamlaka ya Wananchi kuchagua viongozi wao kupokonywa ndiyo Tume hiyo hiyo itakayomamia tena uchaguzi wa 2025 . Kulikuwa na maana gani ya kufanya mabadiliko ya sheria ikiwa mambo yanabaki vilevile ?. Dhamira ya Serikali na Rais Samia ipo wapi?.Tume hii inapaswa kujiuzulu sababu haina uhalali, Sheria (Legality) bila Uhalali (Legitimacy) haina maana.
Pia Uhuru wa Tume ya uchaguzi hautokani na kuiita jina “TUME HURU YA UCHAGUZI” bali uhuru wa Tume ya uchaguzi unatokana na namna viongozi wa tume wanapatikana. Serikali kupitia Msemaji Mkuu wa serikali tarehe 10/April/2024 alitangaza ya kwamba kufuatia tangazo la Serikali Na.225 la tarehe 29 Machi 2024 kwamba Sheria ya Tume huru ya Taifa ya uchaguzi Na.2 imeanza kutumika tarehe 12/April/2024 na hivyo Jina rasmi la Tume ya Uchaguzi ni TUME HURU YA UCHAGUZI (INDEPENDENT NATIONAL ELECTORAL COMMISSION) huku ni kuhadaa wananchi na kudanganya umma.
Tume hii haina uhalali kuitwa Tume huru ya uchaguzi kama viongozi wa Tume ya uchaguzi kuanzia mwenyekiti, Makamu mwenyekiti na wajumbe wote wa Tume watabaki kuwa hawa hawa kuelekea uchaguzi wa 2025 kwani walipatikana kwa sheria ya uchaguzi ya zamani ,hivyo hawana uhalali. Dhamira ipo wapi?.
Hivyo viongozi wote wa Tume ya uchaguzi wa sasa wanapawa kujiuzulu nafasi zao ili kupisha mchakato wa kupata viongozi wengine wapya wa Tume ya uchaguzi kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025.
Hoja ya CCM na serikali kutetea Tume hii sasa ya uchaguzi iliyofanya uchafuzi na kuharibu uchaguzi wa 2020 kuendelea kupitia ibara ya 74(4)(a) ya katiba ya 1977 na kifungu cha 27 cha Sheria na.2 ya Tume ya Uchaguzi ya 2024 haina maana sababu ya UHALALI wao.
Hata kama jambo hili lipo kisheria (legality),ila mchakato wa kichaguzi na kisiasa huongozwa zaidi na uhalali (Legitimacy). Kwani katika muktadha wa ukinzani (Inconsistency/ contradiction /conflict/incompatibility) kati ya sheria (legality) na uhalali (legitimacy) katika siasa na uchaguzi kinachopaswa kusimama mbele ya mwenzake ni uhalali (legitimacy).
Na ndio maana wasomi na wanaharakati maarufu duniani wanasema sheria isiyo na uhalali na isiyokubaliwa na umma haipaswi kuheshimiwa “One has a moral responsibility to disobey unjust laws,because unjust law is no law at all”. Katika muktadha huu sio vyema kutumia kigezo cha kifungu cha 27 cha sheria No.2 ya Tume ya Uchaguzi kubakiza mwenyekiti, Makamu mwenyekiti na wajumbe kuendelea kuwepo kwenye nafasi zao sababu hawana uhalali mbele ya macho ya wananchi hivyo wanapawa kujiuzulu nafasi zao ili kupisha mchakato wa kupata viongozi wengine wapya wa Tume ya uchaguzi kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025. Dhamira ipo wapi?.
Lakini pia kama dhamira ya Mh.Rais Samia ni njema katika kuleta mabadiliko ya kisiasa, Kiuchaguzi na Demokrasia nchini kuna haja gani ya kusita kufanya mabadiliko madogo ya katiba ya 1977 (Minimum Reform) na mchakato wa katiba Mpya kuanza ili dhamira yake iwe dhahiri na falsafa yake iwe na maana . Kwanini mambo yanafanywa kwa kuviziana. Dhamira ipo wapi?.
Dhamira ipo wapi ikiwa hadi sasa mchakato wa katiba Mpya haujaanza ?.
Dhamira ipo wapi ikiwa mabadiliko madogo ya katiba ya 1977 hayajafanywa?.
Dhamira ipo wapi ikiwa Kikosi kazi cha Zanzibar cha kuleta mabadiliko ya kisiasa, Kiuchaguzi na Kidemokrasia kilichoundwa rasmi na Rais Hussein Mwinyi kimezikwa bila taarifa rasmi hadi sasa?.
Dhamira ipo ikiwa Sheria ya Tume ya Uchaguzi Na.2 ya 2024 kifungu cha 10(1) (c) imetaja uchaguzi wa Serikali ya Mitaa kusimamiwa na Tume ya Uchaguzi ilihali hadi sasa hakuna mchakato wa kuundwa Sheria kufanikisha hili , dhamira ipo wapi?.
Dhamira ipo wapi ya kuzuia machafuko ya kiuchaguzi (Post Electoral Violence) inayotokea kila wakati wa uchaguzi watu na vijana kuuwawa ,kufanywa vilema ,kupigwa,kukamatwa na kuumizwa sababu ya chaguzi Zanzibar na Bara ?.
Rai yangu kwa Watanzania,vyama makini vya siasa nchini ,Asasi za kiraia, Viongozi wa Dini , Wanaharakati na kila mtu ni kwamba bado tuna jukumu kubwa la kuendelea kupigania mabadiliko zaidi na zaidi .
Abdul Omary Nondo.
Mwenyekit wa Ngome ya Vijana Taifa -ACT Wazalendo.