#COVID19 Dhana mbalimbali zilizojengeka katika Jamii kuhusu maambukizi ya Virusi vya Corona

#COVID19 Dhana mbalimbali zilizojengeka katika Jamii kuhusu maambukizi ya Virusi vya Corona

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Joined
Aug 7, 2018
Posts
685
Reaction score
1,124
Je, Dalili za #COVID19 ni tofauti kati ya Watu Wazima na watoto?

======
JE, NAWEZA KUPATA #CORONAVIRUS KWA VITU NILIVYOAGIZA UGHAIBUNI?

Kuna tetesi nyingi na taarifa nyingi zinazozunguka kuhusu #COVID19 ugonjwa unaosababishwa na #CoronaVirus, hivyo ni vemakujua zipi ni taarifa za kweli na zipi ni uongo

Kuna baadhi ya watu wanasema ni hatari na unaweza kupata maambukizi ya virusi hivyo kwa kununua bidhaa Ughaibuni inayosafiri kwa muda fulani kukufikia

TAARIFA HIZO SI KWELI: Watafiti bado wanafanya uchunguzi juu ya virusi hivi ambavyo ni vipya kujua kwa namna gani vinaambukiza watu

Hadi sasa, Shirika la Afya (WHO) linasema uwezekano wa kuambukizwa #COVID_19 kutoka kwenye bidhaa hizo ni mdogo kwa kuwa bidhaa inasafiri kwa siku kadhaa na katika hali ya hewa tofauti tofauti

UFAHAMU: KUOGA MAJI YA MOTO SI KINGA DHIDI YA #CORONAVIRUS

Kupitia Mitandao ya Kijamii zipo taarifa kuwa kuoga maji ya moto ni kinga dhidi ya maambukizi ya Ugonjwa wa #COVID19

Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO) limefafanua kuwa kuoga maji ya moto sio kinga dhidi ya kupata maambukizi ya Virusi vya Corona

WHO: Joto la kawaida la Mwili wa Mwanadamu ni Sentigredi 36.5° hadi Sentigredi 37° bila ya kutegemea joto la maji ya kuoga ni kiasi gani

Wameonya kuwa kuoga maji ya moto sana inaweza kuwa hatari kwa ngozi yako na kukuletea majeraha

WHO wanashauri kuwa njia bora ya kujilinda dhidi ya maambukizi ya #COVID19 ni kwa kunawa mikono kwa sabuni na maji tiririka

Kuepuka mikusanyiko na ikibidi basi hakikisha unakuwa mbali na jirani yako kwa angalau mita 2. Usisalimiane kwa kushikana mikono

Tumia Vitakasa Mikono kila mara pale unapokosa sabuni na maji tiririka

JE, UGONJWA WA #COVID19 UNAAMBUKIZA KWA NJIA YA HEWA?

Kwa mujibu wa Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa(WHO) Virusi vya Corona vinasambaa kupitia majimaji yanayotoka kwa muathirika pindi anapokohoa, kupiga au kupiga chafya

Majimaji hayo hayana uwezo wa kuelea angani ili kuweza kuvutwa na Mtu mwingine. Majimaji hayo huanguka chini mara baada ya kumtoka muathirika

Mtu anaweza kuambukizwa #Coronaavirus kwa kurukiwa na majimaji yenye Virusi akiwa ndani ya mita moja kutoka kwa muathirika.

WHO inawahamasisha Watu kuepuka mikusanyiko au kukaa umbali wa zaidi ya mita 1

JE, KIPIMO CHA KUPIMA JOTO LA MWILI KINAWEZA KUTAMBUA MTU MWENYE MAAMBUKIZI YA #COVID19?

Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO) limefafanua kuwa Kipima Joto(Thermal Scanner) kinaweza kutambua Mtu mwenye homa lakini hakitambui Mtu aliyeambukizwa #COVID19 ambaye bado hana dalili za kuwa na joto lenye kuashiria homa

Aidha, inashauriwa kufika katika Vituo vya Afya au Hospitali endapo utahisi kuwa na dalili za maambukizi ya #COVID19

Je, watoto wako kwenye athari kubwa ya kuathiriwa na Virusi Corona?

Mpaka sasa hakuna ushahidi wa wazi wa Watoto kuwa katika hatari kubwa ya kuambukizwa Virusi vya #COVID19. Ingawa zipo taarifa chache za Watoto kuugua #COVID19 lakini takwimu zinaonesha kuwa watu wazima kuwa wahanga zaidi wa #coronavirus

JINSI YA KUWALINDA WATOTO

1: Wafundishe Watoto kuhusu #COVID19, na namna inavyosammbaa pamoja na madhara yake. Waeleze bila ya kuwatisha

2: Wafundishe kunawa mikono yuao kwa Maji Tiririka kwa kutumia sabuni au "Sanitizer" yenye kiwango cha kilevi kwa asilimia 60

3: Waeleze umuhimu wa kukaa mbali na watu pamoja na kuwaepuka watu wanaopiga chafya na kukohoa bila ya kujikinga

4: Safisha kwa kufuata maelekezo ya afya kwa kutumia sabuni ya "Sanitizer" maeneo yote ambayo watoto wanaweza kugusa(Meza, viti, na vitu vingine wanavyokula)

Virusi vya Corona havisambai kwenye hali ya hewa ya joto

Mnamo Machi 9, 2020 Rais wa Marekani, Donald Trump alinukuliwa akisema kuwa Vurusi vya Maambukizi ya Corona vitakoma mwezi Aprili kwasababu Marekani kutakuwa na joto

Aidha, alinukuliwa akisema joto huua virusi vya maambukizi ya ugonjwa wa Corona.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani(WHO), Virusi vya Maambukizi ya Ugonjwa wa Corona vinauwezo wa kusambaa katika hali zote za hewa

WHO wanasema bado hakuna ushahidi kuwa Virusi vya Ugonjwa wa Corona ni vya msimu au hulipuka katika kipindi fulani cha majira ya mwaka

Corona huwaathiri wazee pekee yao

Dhana hii imejengeka miongoni mwa watu wengi kwakuwa kinga yao iko chini ukilinganisha na watu wa makundi mengine

USAHIHI: 👇🏿

Sio kweli kwamba Virusi vya##COVID19 huwaathiri wazee pekee. Kwa mujibu wa takwimu kutoka vyanzo mbalimbali zinaonesha kuwa #COVID19 waathirika wa #coronavirus ni watu wa rika zote

WHO: Watu wenye Kisukari, matatizo ya Shambulio la Moyo na Pumu wako kwenye hatari zaidi na magonjwa mengine yanayopunguza kinga ya mwili

KUSHIKILIA PUMZI YAKO KWA SEKUNDE 10 BILA YA KUKOHOA AU KUJISIKIA VIBAYA SIO KIPIMO CHA #COVID19

Kupitia Mitandao ya Kijamii zimekuwepo taarifa kuwa watu wanaweza kujipima kama wamepata maambukizi ya #CoronaVirus kwa kushikilia pumzi yao kwa sekunde 10

Taarifa hizo zinaeleza kuwa ndani ya sekunde 10 endapo utashikilia pumzi na ukianza kujisikia vibaya au kuanza kukohoa basi umepata maambukizi

Shirika la Umoja wa Mataifa limefafanua kuwa taarifa hizo si za kweli na kipimo halisi cha #COVID19 kinapatikana katika Hospitali zilizoelekezwa na mamlaka za nchi husika pekee

======

Being able to hold your breath for 10 seconds or more without coughing or feeling discomfort DOES NOT mean you are free from the coronavirus disease (COVID-19) or any other lung disease.

The most common symptoms of COVID-19 are dry cough, tiredness and fever. Some people may develop more severe forms of the disease, such as pneumonia.

The best way to confirm if you have the virus producing COVID-19 disease is with a laboratory test. You cannot confirm it with this breathing exercise, which can even be dangerous.

=======

The World Health Organizaton

At a rally on March 9, US President Trump told his supporters that the coronavirus will go away in April as the weather in the US gets warmer.

Last month, he was also quoted saying that the virus would be gone by April and that "the heat generally speaking kills this kind of virus," referring to the idea that warmer weather will kill the virus and thus help minimize its spread.

Truth: According to the WHO, the coronavirus can be transmitted in all areas of the globe, including hot climates. It won't just go away in the Northern Hemisphere as the weather gets warmer in spring and summer, experts say. We do not yet know if COVID-19 is a seasonal virus like influenza is, meaning it loses the ability to infect cells as the temperature rises.

Covid-19 affects only older people

•While older people are at greater risk owing to weakened immunity, there’s no evidence to show that younger, healthy people cannot be infected. Currently, all demographics are affected by the virus across the world.

The mortality rate, however, is higher among older persons.

• WHO says people with diabetes, asthma and heart diseases are at higher risk of infection.

Mosquito bites can cause infection

•Covid-19 is a respiratory disease that’s chiefly caused by saliva or mucus droplets resulting from a cough or sneeze from an infected person. Mosquitoes cannot transmit the virus.

C|Net
 
JamiiTalks
hili gonjwa tunatisha kila mtu na lwake, China kwenyewe Wu-Han hakuna maambukizi kwa siku ya leo na Jimbo la Hubei, na watu wanaanza kwenda makazini, shule karibu zitafunguliwa
sisi huku ndio kwaanza kupambana, Wenzetu walijenga Hospital ndani ya wiki moja, na wamefanikiwa
Nilisikia DW pumzi ikakata, gonjwa limeisha???!!! 19/March/2020 sisi ndio tumemaliza siku 1 kati ya 30
Habari za Ulimwengu | DW
China leo imefikia hatua muhimu katika vita dhidi ya janga la virusi vya corona, baada ya kutangaza kutokuwepo na maambukizi mapya ya ndani kwa mara ya kwanza tangu kuzuka kwa mripuko, lakini maambukizi ya kutoka nje yanahatarisha maendeleo hayo. Mji wa Wuhan ambao ulikuwa kitovu cha mripuko wa virusi vya corona mwezi Desemba, umeripoti kutokuwa na maambukizi mapya ya ndani, ikiwa ni mara ya kwanza tangu mamlaka zilipoanza kuchapisha takwimu mnamo mwezi Januari. Mji huo ulio na wakaazi karibu milioni 11 uliwekwa chini ya karantini kuanzia Januari 23, huku wakaazi wengine milioni 40 katika jimbo la Hubei nao wakifungiwa siku zilizofuata.
Maisha yameanza kurejea kama kawaida katika maeneo mengine ya nchi, huku watu wakirejea kazini, viwanda kufunguliwa na shule zikijiandaa kuendelea na masomo katika baadhi ya mikoa
 
DHANA POTOFU KUHUSU CORONA: Virusi vya Corona havisambai kwenye hali ya hewa ya joto

Mnamo Machi 9, 2020 Rais wa Marekani, Donald Trump alinukuliwa akisema kuwa Vurusi vya Maambukizi ya Corona vitakoma mwezi Aprili kwasababu Marekani kutakuwa na joto

Aidha, alinukuliwa akisema joto huua virusi vya maambukizi ya ugonjwa wa Corona.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani(WHO), Virusi vya Maambukizi ya Ugonjwa wa Corona vinauwezo wa kusambaa katika hali zote za hewa

WHO wanasema bado hakuna ushahidi kuwa Virusi vya Ugonjwa wa Corona ni vya msimu au hulipuka katika kipindi fulani cha majira ya mwaka

=======

The World Health Organizaton

At a rally on March 9, US President Trump told his supporters that the coronavirus will go away in April as the weather in the US gets warmer.

Last month, he was also quoted saying that the virus would be gone by April and that "the heat generally speaking kills this kind of virus," referring to the idea that warmer weather will kill the virus and thus help minimize its spread.

Truth: According to the WHO, the coronavirus can be transmitted in all areas of the globe, including hot climates. It won't just go away in the Northern Hemisphere as the weather gets warmer in spring and summer, experts say. We do not yet know if COVID-19 is a seasonal virus like influenza is, meaning it loses the ability to infect cells as the temperature rises.

C|Net
Hawajasemea kama corona inaua mtu mweusi au la? Make hiyo nayo inasemwa sana kuwa mtu mweusi na corona ni sawa na mbwa na gono. Kwamba kila mbwa ana gona lakini lakini gono halina madhala kwa mbwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vinasambaa kama kawa kama dawa! Kikubwa tu ni kwamba hatutakufa, nenda kagonge K-Vant changanya na Nyagi pozea na Vile vibia vyenye rangi ya CCM aaghh nenda kwa familia yako kaimbe mapambio mwanzo mwisho. Utaishia ku-koroma tu na sio ku-corona
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] mkuu!!!

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
 
View attachment 1393108

hili gonjwa tunatisha kila mtu na lwake, China kwenyewe Wu-Han hakuna maambukizi kwa siku ya leo na Jimbo la Hubei, na watu wanaanza kwenda makazini, shule karibu zitafunguliwa
sisi huku ndio kwaanza kupambana, Wenzetu walijenga Hospital ndani ya wiki moja, na wamefanikiwa
Nilisikia DW pumzi ikakata, gonjwa limeisha???!!! 19/March/2020 sisi ndio tumemaliza siku 1 kati ya 30
Habari za Ulimwengu | DW
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] mkuu!!!

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
Naam Kaka
 
Lakini kwa mujibu wa Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) amesema, mapema leo, kuwa hawajui kama havisambai kwenye mazingira ya joto.

Maana yake kama wangekuwa wanajua kuwa vinasambaa kwenye mazingira ya joto angesema. Kuna tofauti kati ya kukanusha kitu na kutokujua kitu. Hiyo bado ni hypothesis.

Achana na wanasiasa wa Marekani na vyombo vyao vya habari ambavyo kila siku kazi ni kumpinga tu Trump. Hakuna anayejua, japo kwa kuangalia tu trend ya huu ugonjwa huenda kuna ukweli kuwa havisambai sana kwenye hali ya joto.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom