Dhana ya bunge kuwa muhimili unaojitegemea kuishauri na kuisimamia serikali iko wapi?

Dhana ya bunge kuwa muhimili unaojitegemea kuishauri na kuisimamia serikali iko wapi?

Nyumisi

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2010
Posts
13,499
Reaction score
19,292
Wote tumeona spika alivyoshushiwa spana na wakuu wa dola pamoja na wale wengine kwenye chama. Hebu tujiulize kidogo, mnapomuondoa spika kwa kutimiza wajibu wake mnapeleka ujumbe gani kuhusu bunge kuwa mhimili huru wa kuishauri na kuisimamia serikali, je, bunge litabaki kuwa kikaragosi cha kucheza mdundo unaopigwa na serikali?
 
Kwani hamkuelewa somo lililotolewa na Hayati Dr. John Pombe Joseph Magufuli alipokuwa akijibu swali la ndugu Pascal Mayalla kwamba kuna mihimili mitatu lakini kati ya hiyo mitatu kuna mmoja ambao umejichimbia kwenda kwa chini zaidi ?
 
Wote tumeona spika alivyoshushiwa spana na wakuu wa dola pamoja na wale wengine kwenye chama. Hebu tujiulize kidogo, mnapomuondoa spika kwa kutimiza wajibu wake mnapeleka ujumbe gani kuhusu bunge kuwa mhimili huru wa kuishauri na kuisimamia serikali, je, bunge litabaki kuwa kikaragosi cha kucheza mdundo unaopigwa na serikali?
Lenyewe lilishaikubali Hali hiyo long time a go, acha lipambane na Hali yake, huenda siku likazinduka usingizini, kwani jobo na msaidizi wake walituona hamnazo Kwa muda mrefu takribani miaka , 6iliyopita walisahau kama Mungu sii Athumani🏃.
 
Kwanini hukuuliza kipindi cha marehemu pombe uje uulize kipindi hiki tunapotaka kufungua nchi?

Tukisema katiba mpya mnatuzodoa... Hebu kafieni mbali
Tulivyosutwa na kuambiwa tunaleta chokochoko hawa jamaa walikua busy wanaimba mapambio ya kusifu na kuabudu.

"Wakimalizana na sisi watageukiana wao kwa wao" by Tundu Lissu
 
Back
Top Bottom