Dhana ya Local Content imeishia wapi? Kivuko kukarabatiwa nje ya nchi

Dhana ya Local Content imeishia wapi? Kivuko kukarabatiwa nje ya nchi

Stuka

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
282
Reaction score
906
Kuna Dhana ilianza kupigiwa debe na Serikali ya kuwawezesha watanzania kunufaika na fursa zilizoko nchini ili kuchochea ajira na kukuza uchumi wa nchi yetu, Leo Bilioni 7.5 zinakwenda kunufaisha nchi jirani wakati angepewa Songoro Marine ambaye ni mtanzania fedha zingezunguka Tanzania.

Vijana wa kitanzania wangepata ajira, mama ntilie wangepata ajira, bodaboda wangepata ajira, viwanda vyetu vya ndani vingeuza malighafi nini hasa kilichowasukuma Wizara ya Uchukuzi kuamua kuiacha Kampuni ya Songoro Marine na kuwapelekea kazi hiyo nchi ya nje?

Au dhana ya Local Content haizingatiwi kwa sasa katika vipaumbele vya Wizara?
 
Billion 7.5 naona kama Maji..... maana mbona tulikubali Trillion 1.5 wakati wa Magufuli.
 
Hata mimi nimejiuliza kwanini isingepewa kazi kampuni ya tanzania vijana wetu wakapata ajira?
 
Sasa tuko kwenye uchumi wa soko huria. Hivyo muwe tu wapole.
 
lakini fedha zilibaki nchini kukuza uchumi nalo usilisahau

..uchumi gani ulikuwa wakati vyuma vilikuwa vimekaza.

..tuandike KATIBA MPYA ili huu utaratibu wa magenge ya wizi kupokezana, leo sukuma gang, kesho msoga gang, utaratibu huo ukome.
 
Back
Top Bottom