Dhana ya maslahi ya wasanii kupiganiwa na wasanii inatulemaza na kutuangusha sana

Dhana ya maslahi ya wasanii kupiganiwa na wasanii inatulemaza na kutuangusha sana

Sexless

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2017
Posts
23,683
Reaction score
55,898
Hivi wasanii kwa kaliba yao na ubutu wao wa uelewa, kuna la maana wanaweza kulijenga ktk meza ya majadiliano yahusuyo sera, mipango, mitazamo ya sanaa na mustabari wake?

Kulikuwa na haja gani ya mhe rais kuambatana na wasanii ktk ziara yake huko Korea ? Kwann rais asingeambatana na "watu vichwa" kutoka sekta za uchumi, mipango na sanaa ili wakapokee mawazo ya wakorea na kuyachakata kabla ya kusaini mikataba ama makubaliano yoyote?

Hivi wasanii, mfano Elizabeth Michael aka Lulu, mbali ya "make up" yake ana nini kichwani?

Kuna kasumba ya kuamini hata huko bungeni, kuwa maslahi ya vijana yatapiganiwa na wabunge vijana, walemavu na wabunge walemavu, vyuo vikuu na wabunge toka vyuo vikuu, wasaninii na wabunge wasanii.

Tangu tumepeleka wabunge wanawake na walemavu huko bungeni adha na shida za wanawake na walemavu zimeisha? Huyo MwanaFA ni msanii na naibu waziri, Kuna la maana kalifanya lililoibadilisha sanaa??

Hii kasumba itatumaliza.

Hakukuwa na ulazima kuwapeleka wasanii Korea Kusini..
 
Una point, ndio maana hata mawaziri hawapewi wizara kulingana na taaluma zao japo hilo ni muhimu pia.
 
Hao wameenda tu kumshangaa Jumong anavotembeza mkong'oto kwenye tv kweli ndiye, Swala la kujifunza ni kuwasingizia.
CCM hii inatengeneza popularity kupitia ujinga wa wapiga kura ambao ndo walipa kodi wenyewe.
 
Orodha ya watu wanaosababisha umaskiniiiii ni walimu,polisi,jeshi,wasanii
Haya makundi ni hasara kwa hili taifa, Walimu wakiongoza katika issue za siasa chafu.
Wasanii wakiongoza kutumiwa kwa upotoshaji na kunadi sera mbovu.
Askar wakitumiwa kukandamiza nguvu ya wazalendo na kuwalinda wezi na machawa.

Hata hivyo hua na mwisho mbaya sana.
 
Back
Top Bottom