WomanOfSubstance
JF-Expert Member
- May 30, 2008
- 5,457
- 963
Nijuavyo mimi wachumba ni mwanamke na mwanaume ambao wamevuka hatua ya urafiki na kuingia hatua nyingine kwa maana kutambulishana na kutangaza nia ya kuoana.Wachumba siyo mke na mume au watu wanaoishi pamoja bila ndoa.
Siku hizi huenda dhana ya mchumba imechukua sura nyingine.
Je watu wanaoishi pamoja bila ndoa wakaanza kuzaa watoto ni wachumba?
Nijuavyo mimi wachumba ni mwanamke na mwanaume ambao wamevuka hatua ya urafiki na kuingia hatua nyingine kwa maana kutambulishana na kutangaza nia ya kuoana.Wachumba siyo mke na mume au watu wanaoishi pamoja bila ndoa.
Siku hizi huenda dhana ya mchumba imechukua sura nyingine.
Je watu wanaoishi pamoja bila ndoa wakaanza kuzaa watoto ni wachumba?
Ebu nikuulize kwanza wewe? wanaoishi pamoja bila ndoa huko nyuma kabla ya UKISASA walikuwa wanaitwaje?????
hawa watu kitaalamu tunawaitaga SENIOR BACHELORS!
Kwani zamani walikuwapo wanaoishi pamoja kabla ya ndoa?.... wataanzia wapi wakati zamani msichana akishakua tu huozwa kwa ndoa rasmi sasa kuishi pamoja kutaanzia wapi
MJ1,WoS maisha sasa yamebadilika badala ya sie kwenda mbele ya wakati wakati umetutangulia.
Ninadhani kuna sheria inayotambua mtu na mke/mume kama wakiishi pamoja kwa kipindi cha miezi 6 kama sikosei na wakiwa wanatambulika na majirani kama wanaishi pamoja kama mume na mke. Sasa kwa wale waliokaa hadi kuzaa sidhani kama bado wanajitambulisha au kujitambua kama wachumba bali ni mwanandoa. (Sina uhakika na hicho kipindi ni miezi sita au mitatu sikumbuki vema)
Unadhani ni kwanini?Mnajua mkiishi wawili bila kutambulishana au kufunga ndoa aamini usiamini uhusiano huu unadumu kwa muda mrefu sana.Nina jamaa zangu wameishi uhusiano huu zaidi ya miaka kumi lakini walipo amua kutambulishana na kufunga ndoa rasmi baada ya miezi kadhaa mitafaruko ikaanza ndani ya nyumba ugomvi hauishi.Maisha ya bila kutambulishana mazuri sana na kunakuwa na amani ndani ya nyumba na upendo unachanua kila siku kila mmoja akiwa makini na mwenzie.
Unadhani ni kwanini?
hawa watu kitaalamu tunawaitaga SENIOR BACHELORS!
Huu mtindo wachumba kukaa pamoja haufai na kinyume cha maadili. Itakuwa bora kama hamjafunga ndoa ya kidini au ya serikali, lkn ndoa ya kimila mmefunga hapo hata kama mkiishi pamoja inakubalika kimaadili maana watu wengi zamani walifunga ndoa za kimila na wanaendelea kuishi pamoja na kuzaa, hiyo inatambulika. Sio eti Bf na Gf mmeamua kukaa pamoja na wazazi hawajui posa wala mahari, hii itakuwa kinyume na maadili.
Unachosema Fidel ni kweli.
Mkiwa hamjafunga hizo pingu, kila mmoja anajitahidi kutokumuudhi mwenzake na kila mmoja natambua kuwa there are no strings attached.Hakuna zile hierachy ambazo zinapelekea mitafaruku au mmoja kujiona ana haki zaidi kuliko mwingine.
Ila hii ina risks zake hasa kwa mwanamke maana uhusiano ukiisha, kila mtu atamwona kuwa huyu alikuwa anaishi na fulani vikashindikana - lazima ana kasoro.Na pia huo ni ushahidi tosha kuwa historia yake ilikuwa kadha kadha kadha
Hiyo mila hata kule kwetu ilikuwepo, lkn baada ya kumuiba huo usiku na kukaa kama siku mbili hivi, upande wa mume unaenda kutoa taarifa kwamba binti yenu tunae. Baada ya hizo taarifa wanatoa posa na mahari na wanaishi kama mume na mke. hii ndio inaitwa ndoa ya kimila.Tatizo ni tafsiri la hilo neno maadili na mila. Kilicho maadili na mila kwenu unaweza kukuta kwa mwingine sicho. kuna makabila mengine ulikua mtu unaweza kumuiba binti usiku ukampeleka kwako akikaa zaidi ya wiki bila kurudi kwao basi huyo mkeo.
Hiyo mila hata kule kwetu ilikuwepo, lkn baada ya kumuiba huo usiku na kukaa kama siku mbili hivi, upande wa mume unaenda kutoa taarifa kwamba binti yenu tunae. Baada ya hizo taarifa wanatoa posa na mahari na wanaishi kama mume na mke. hii ndio inaitwa ndoa ya kimila.