Dhana ya “Product Lifecycle” Kwenye Fundraising Campaign

Dhana ya “Product Lifecycle” Kwenye Fundraising Campaign

Joined
Feb 5, 2022
Posts
38
Reaction score
60
1731490779426.png

Mojawapo ya dhana ya msingi katika biashara hususani upande wa masoko ni kwamba; bidhaa au huduma inapitia hatua tofauti tofauti tangu inapoanzishwa kwa mara ya kwanza hadi inapoondolewa kwenye soko. Hatua hizi hujumuisha; hatua ya utambulisho (Introductory Stage), hatua ya ukuaji (Growth Stage), hatua ya ukomavu (Maturity Stage) na mwisho kabisa hatua ya anguko (Decline Stage). Dhana hii inaeleza kwamba;
  • Bidhaa yoyote ina ukomo wa muda.
  • Kwa kila hatua ambayo bidhaa hupita, huleta changamoto tofauti kwa kampuni.
  • Mikakati ya kampuni yaani “strategies” zinapaswa kubadilika kulingana na hatua ambayo bidhaa inapita.
  • Faida itokanayo na bidhaa, hutofautiana kati ya hatua moja mpaka hatua nyingine.
Mashirika ya hisani yaani “charity organizations” yana mengi ya kujifunza kutoka kwenye dhana hii, hususani kwenye eneo la utafutaji wa rasilimali fedha kwa ajili ya kuendesha programu na miradi ya shirika (fundraising activities). Kwanza shirika linapaswa kutafsiri maana ya bidhaa au “product” kwa muktadha wa “fundraising”. Tafsiri ya bidhaa kwa muktadha wa “fundraising” inaweza ikawa ni aina au mbinu itumikayo na shirika kutafuta fedha, hii inaweza ikawa “corporate fundraising program from a particular industry”, “challenge event” n.k.

Hakuna kanuni moja inayoelekeza namna ya kutafsiri bidhaa kwa muktadha wa “fundraising”, kila shirika lina namna yake ya kutafsiri. Ijapokuwa dhana ya “product lifecycle” kwa muktadha wa “fundraising” inakosolewa vikali, lakini bado inaweza kulisaidia shirika kuboresha programu za “fundraising” Kwa maana ya kwamba shirika linaweza kuanzisha “fundraising programs” na kuzi-consider as products ambapo zitapitia kwenye hatua zifuatazo, kama ambavyo bidhaa hupitia.
  • Hatua ya Utambulisho (Introductory Stage): Hapa shirika linapaswa kuitambulisha “fundraising program” kwa umma (constitutiencies) na kuelezea faida zitokanazo na programu husika na namna ambavyo watu wanaweza kushiriki kwenye programu husika.
  • Hatua ya Ukuaji ( Growth Stage): Kwenye hatua hii, inawezekana baadhi ya mashirika yakaanza kuiga programu baada ya kuona uzuri wake, na hatimae kupata ushindani. Hivyo basi katika hatua hii, shirika linapaswa kuji-differentiate kwenye utekelezaji wa programu ili kudhibiti ushindani kutoka kwa mashirika mengine.
  • Hatua ya Ukomavu (Maturity Stage): Kwenye hatua hii shirika linapaswa kupunguza gharama za uendeshaji wa programu kwa sababu mahitaji katika hatua hii yanaanza kupungua. Hivyo ni vyema gharama zikaelekezwa kuhudumua mahitaji machache yaliyopo.

Article By
OMAR MSONGA
CONSULTANT
Project Management, Strategy, Fundraising & Training
Call: +255 719 518 367
Email: omarmsonga8@gmail.com
DAR ES SALAAM
TANZANIA
 
Back
Top Bottom