Dhana ya thamani ya muda na mwenendo wa bunge

mwikumwiku

Senior Member
Joined
Jul 15, 2011
Posts
153
Reaction score
35
Nafuatilia mwenendo wa Bunge la Katiba kwa kweli nasikitishwa na namna wanavyoenenda bila kujali muda. Kwanza wanachelewa kuanza mjadala,lakini pamoja na kuchelewa huko bado wanatumia muda mwingi kubishana kwenye hoja ambazo hazi tija kabisa! Kwa mfano wametumia zaidi ya dakika 45 kubisha juu ya nani aanze kuhutubia Bunge Kati ya Rais na Mkiti wa Tume. Kwa kifupi kuanzia jana mpaka leo (saa hizi) wamejadili Kanuni 8 tu.!

My take:wa utaratibu huu wanahitaji siyo chini ya siku 10 kujadili Kanuni tu! Huu ni ujanja wa kujiongezea kipato hasa baada ya hoja Yao ya kuongeza posho kukwama.

Ubabaishaji mtupu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…