BAAJUN POET
Member
- Jul 15, 2021
- 6
- 11
DHANA YA USHOGA NA SINTOFAHAMU ILIYOPO JUU YA WAHANGA WA UKATILI WA KIHISIA, KIJINSIA, NA KIMAUMBILE TANZANIA
UTANGULIZI:
Kuna vilio vingi chini ya hiki kivuli cha woga. Kuna mambo jamii inaogopa kuzungumza. Familia nyingi zinasubiri muujiza; hali ya kuwa ziko katika sintofahamu juu ya namna gani wafanye maamuzi juu ya wao wenyewe au watoto wao ambao ni wahanga wa kihisia, kijinsia, na kimaumbile ambao miongoni mwao ni:
[Fig. 1: Source: Human Rights Watch]
Huo ni upande mmoja tu wa familia ambazo zimeijua changamoto hiyo. Upande wa pili ni familia ambazo bado hawajaijua changamoto hiyo vizuri lakini wao ndiyo namba moja kuwashambulia mitandaoni watu hao pindi tu zinapoongelewa mada hizi ambazo lengo ni kuibua kutafuta utatuzi ikiwa ndiyo njia ya pekee ya kuzisaidia familia hizi au mtu mmoja mmoja kujikomboa katika migogoro, fedheha, misongo ya mawazo, ambayo husababishwa na dhana hii ya ukatili unaopelekea maradhi ya kiakili na vifo.
DHANA YA UKATILI HUANZIA WAPI?
Dhana ya ukatili wa kihisia na kimaumbile huanzia pale ambapo makundi tajwa hapo juu hupitia changamoto kama:
[Fig. 2: Source: Tanzania Bureau of Statistics]
Ukweli ni kuwa makundi tajwa ya watu hapo juu ni miongoni mwa watu wengi kati yetu kwasasa, na ni watu ambao tunashirikiana nao katika mengi iwe kwa kuwafahamu au kutokuwafahamu. Kufahamu changamoto zao au kutozifahamu. Ni watu ambao wenye ndoto kama zetu, wenye matamanio ya kufanikiwa kimaisha, na wengine walishafanikiwa kabisa! Ni kweli baadhi yao ingali ni vijana wadogo wanaopambania ndoto zao, lakini wapo watu wazima pia ambao ni watu wa muhimu katika makampuni, taasisi na mamlaka mbalimbali [binafsi na za serikali] n.k., Huku wengineo wakiwa ni watu maarufu na wenye ushawishi kwa jamii. Si ajabu pia kuona wengi wao ni watu walio karibu zaidi na Mungu, na wenye mioyo misafi zaidi kuliko hata sisi wachache [baadhi yetu] tunaowazomea mitandaoni au kuwafanyia ukatili huku mitaani au majumbani.
Yote hayo ni kuonesha ya kuwa, pamoja na hali zao na changamoto zao [kama zilivyotajwa juu] ambazo jamii ndiyo chanzo kikubwa, ingali wanafanya mambo makubwa chanya pengine zaidi ya yale tunayoyafanya. Na ingali wana ndoto kubwa kwa wale wanaochipukia.
[Fig. 3 : Source: Save The Children]
Na kama ilivyo kwa binadamu wote, kuna wema na wabaya, basi hata katika makundi hayo wapo watu wabaya pia, wanaojaribu kutumia nafasi zao vibaya kuvunja maadili, na hapo ndipo baadhi ya watu katika jamii huongelea vibaya makundi hayo. Au huyachukulia kwa mtazamo wa tofauti. Lakini ukweli ni kuwa wapo watu wema pia katika makundi hayohayo ambao wana umuhimu mkubwa na hawastahili kujumuishwa katika makosa wanayoyafanya wengine.
Nitoe wito, na ieleweke ya kuwa, hali zozote za kihisia na kimaumbile ni matokeo ya athari za kibaiolojia anazozaliwa nazo mtu. Na hazihusiani na matakwa ya mtu binafsi! [Japokuwa wapo baadhi ya watu wanaoigiza hali hizo na matokeo yake huwa mabaya zaidi].
SULUHISHO NI LIPI?
Suluhisho kubwa ni kukubali uhalisia. Uhalisia wa kuwa watu hawa tunao katika familia zetu na jamii zetu, licha ya wao kutopewa nafasi katika jamii ikiwemo haki zao za msingi lakini ingali bado ni wanetu, marafiki zetu, ndugu zetu, na binadamu wenzetu. Chuki na ukatili wanaofanyiwa hauondoi ukweli ya kuwa; watu hao wapo, na wataendelea kuwepo, na watabaki kuwa wanafamilia wetu daima hata kama ulimwengu mzima hauwatambui!
Kikubwa ni kuwafanya wajikubali. Na kama ni wewe basi Jikubali! Kwani kila mwanadamu ni matokeo ya uumbaji wa Mungu. N a Mungu hajawahi kukosea. Sasa iweje leo hii Mungu awachukie viumbe wake sababu ya hisia, jinsia na maumbile aliyowaumbia kwa mikono yake? Viumbe ambao miongoni mwao ni watiifu kwake, tena wenye mioyo misafi ya kuisaidia jamii yake? Ukweli ni kuwa Mungu hawezi kukosoa uumbaji wake.
Pengine dhana nyingi potofu zilizopo katika jamii kuhusu watu hawa ambazo huhusianishwa na masuala ya kiimani bila shaka kuna sababu nyengine tofauti. Kwa hakika kuna ukakasi na maswali mengi juu ya jambo hili! Ila kikubwa ni kujikubali, kuwa karibu na Mungu [kuwa mtu mwema kwake na kwa wanaokuzunguka] kuwa na ndoto kubwa na juhudi katika kuyafikia mafanikio. Na kutokubali uhalisia wako udharauliwe au utu wako uchezewe. Chukua hatua! Kila mtu ni bora na wa tofauti kutokana na vile alivyo!
Haifai kuwalazimisha watu wenye hali hizi kuwa sawa na wewe ulivyo. Kufanya utakavyo. Na kuishi uishivyo. Kwani kwa kufanya hivi ndipo linapoibuka wimbi kubwa la matukio ya watu kujiua, n.k.
Hebu tafakari [kwa mfano] unapoamua kumlazimisha kijana mwenye jinsia/hisia mbili [kwa kujua au kutokujua] afunge ndoa na binti mrembo kwakuwa tu vijana wengine wanafanya hivyo. Hali ya kuwa yeye jinsia/hisia yake inayofanya kazi zaidi ni ya kike. Matokeo yake ni nini?
Au kwa kumfungia ndani kijana mlemavu ukimuaminisha kuwa hawezi kwenda shule sababu ya maumbile yake au akili zake. Je, Kesho yake ni ipi?
Mifano ipo mingi mno! Inayowagusa hawa wenzetu wenye jinsia/hisia zaidi ya moja na wale wenye ulemavu ambao hupitia changamoto nyingi za ukatili. Inafikia muda baadhi yao wanakubali kukatiliwa kingono na baadhi ya wanajamii ili tu kufichiwa uhalisia wao, pindi wanapotaka kusaidiwa shida zao, ikiwemo kupata usaidizi wa huduma za kiafya na kisheria.
Pinga ukatili! Kila binadamu ana haki ya kuthaminiwa! Vunja ukimya!
Makala hii ni matokeo ya yale niliyoyapitia katika safari ya maisha yangu ijumuishayo watu wa makundi haya na familia zilizopoteza matumaini. Kwenu marafiki zangu vipenzi, hakika dunia ipo na ninyi. Nani ajuaye pengine andiko hili likashinda na kwenda kuwa mwanga wa matumaini. Basi na ikawe heri!
DONDOSHA VOTE YAKO HAPO CHINI IKIKUPENDEZA.

- Watu wenye hisia zaidi ya moja
- Watu wenye jinsia zaidi ya moja
- Watu wenye ulemavu
[Fig. 1: Source: Human Rights Watch]
Huo ni upande mmoja tu wa familia ambazo zimeijua changamoto hiyo. Upande wa pili ni familia ambazo bado hawajaijua changamoto hiyo vizuri lakini wao ndiyo namba moja kuwashambulia mitandaoni watu hao pindi tu zinapoongelewa mada hizi ambazo lengo ni kuibua kutafuta utatuzi ikiwa ndiyo njia ya pekee ya kuzisaidia familia hizi au mtu mmoja mmoja kujikomboa katika migogoro, fedheha, misongo ya mawazo, ambayo husababishwa na dhana hii ya ukatili unaopelekea maradhi ya kiakili na vifo.
DHANA YA UKATILI HUANZIA WAPI?
Dhana ya ukatili wa kihisia na kimaumbile huanzia pale ambapo makundi tajwa hapo juu hupitia changamoto kama:
- Kupigwa
- Kunyanyapaliwa
- Kuongelewa vibaya
- Kuchafuliwa mitandaoni
- Kutengwa
- Kufukuzwa
- Kuhujumiwa kingono
- Kukosa huduma za afya
- Kukosa usaidizi wa kisheria na haki nyengine za msingi za kibinadamu. Ikiwemo haki ya kutambulika kikatiba N.K.

Upvote
2