Dharau by Ibraah FT Harmonize

Intelligent businessman

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2022
Posts
31,913
Reaction score
65,514
Ukisikia wiki ya Hit ndio hii, Ibraah wa Kondegang ameachia wimbo uitwao Dharau ambao ame shirikiana na Boss wake Harmonize nadiriki kuwa ambia ni kisanga, awa jamaa kwa Melody ni balaa yaani ni hatari tupu,

Ngoma inapanda Tending kwa speed ya 5G uko mjini Youtube.


.
 
Lyrics
Mungu alonipa ukilema hawezi ninyima mwendo

Na sikupanga imenibidi kulivua pendo

Maana mwanzo nilidhani umebadilika

Ofcourse hakuna aliekamilika

Masaa masiku miaka imekatika

Nachukia nikijiona nikilalamika

Bora ugali dagaa kwenye amani

Kuliko wali nyama vitani

Mateso vitimbwi purukushani

Kama unajiona kichwa shingo nani

Bora ugali dagaa kwenye amani

Kuliko wali nyama vitani

Mateso vitimbwi purukushani

Kama unajiona kichwa shingo nani



Mi sipendi dharau manyanyaso masimango siwezi siwezi

Dharau manyanyaso dharau masimango siwezi siwezi



Me nilidhulumu nafsi kujirikirihisha

Nikiamini mi mtu wa mtu

Kumbe bora ningechukuchuku

Aaaah kidogo ningefanya utukutu

Moyo ndo ulikupa nafasi kunisikitisha nilichoambulia maumivu tu

Bora ningechukuchuku

Ama ningewapa watu wakifanye supu

Kwako nilikuwa nyendo nikijua you are my destiny

Sina wa kumtunzia heshima kama hata wewe nitashindwa kukuthamini

Nitakwenda utakwenda mazima

Japo itakuwa ngumu kuamini

Nitamisi michezo ya mama Amina

Kwa kucheza kwa kuburuza ulimi



Mapenzi ulionipa wewe

Walai sikutamani mwingine we wa kiapo

Mwenzangu umebadilika wewe

Japo mi nakupa kila utakacho





Bora ugali dagaa kwenye amani

Kuliko wali nyama vitani

Mateso vitimbwi purukushani

Kama unajiona kichwa shingo nani


Mi sipendi dharau manyanyaso masimango siwezi siwezi

Dharau manyanyaso dharau masimango siwezi siwezi
 
Bado sijausikiliza huo wimbo, lakini kiukweli hawa jamaa wawili wakikutana huwa wanafanya kweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…