Dharau: Mshahara wa Mgunda + Matola haufikii nusu ya mshahara aliokuwa akilipwa Benchikha

Mcheza Piano

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2024
Posts
562
Reaction score
1,339
Hii ni dharau, pili mshahara wa Benchikha ulitoka kwa mmiliki wa club ya Simba yaani Mo (alisema kainunua na hajawahi kufuta kauli yake), mishahara ya Mgunda na Matola inatokana na mapato ya club, yaani ikitokea watu wamechelewesha kodi kwenye lile jengo lao, au wanachama wamesusia kulipa ada, makocha wanaingia taabuni.

Ndugu yangu Mo, Mangungu na Try Again hebu kuweni serious kidogo, hawa watu mnawaumiza kisaikolojia.
 
Ndio maana kibu ameamua kuwakanda. Huyo kocha hajitambui wanchululia poa na yeye anacheka tu mpira saivi ni biashara yeye kama bado anatoa huduma aendelee tu kuwabeba wenzake
 
Wewe ni mbumbumbu unaongea vitu ambavyo hauna data ulitakiwa useme benchikha alikuwa anakunja sh ngapi na mgunda anakunja sh ngapi! Umetoka kijiwe cha boda boda unakimbilia humu kutupa taarifa, hivi unatuchukuliaje mkuu?
 
Sijui wamempa nini, hajui kuwa anajishusha thamani
 
Mgunda ni mwanachama wa simba naye lazima atoe mchango kwenye club.

Lakini kumbuka pia nabii hakubaliki kwao!
 
Wewe ni mbumbumbu unaongea vitu ambavyo hauna data ulitakiwa useme benchikha alikuwa anakunja sh ngapi na mgunda anakunja sh ngapi! Umetoka kijiwe cha boda boda unakimbilia humu kutupa taarifa, hivi unatuchukuliaje mkuu?
Nimesoma kwa speed nikidhani angetoa kiasi husika cha kila mmoja wao ili tulinganishe, kumbe porojo za kijiweni.
 
Mgunda aende South au Egypt akafundishe mpira
 
Mambo ya Simba tuwaachia chief Mangungo, try again na yule adui wa Bugati.
Kampuni nyingi ukiwa country manager mtanzania unalipwa Madafu na unapanga Buguruni. Akija mzungu anapangishiwa nyumba masaki ma kulipwa Dola.
 
Mkuu
Hii ni dharau, pili mshahara wa Benchikha ulitoka kwa mmiliki wa club ya Simba yaani Mo (alisema kainunua na hajawahi kufuta kauli yake), mishahara ya Mgunda na Matola inatokana na mapato ya club, yaani ikitokea watu wamechelewesha kodi kwenye lile jengo lao, au wanachama wamesusia kulipa ada, makocha wanaingia taabuni.

Ndugu yangu Mo, Mangungu na Try Again hebu kuweni serious kidogo, hawa watu mnawaumiza kisaikolojia.
Mkuu Tanzania michezo no ridhaa na siyo professional, ndiyo maana wanariadha wakienda kushiriki mashindano nje ya nchi wakishinda zawadi % kubwa zinaenda serikalini, Tofauti na Kenya wenzetu wao michezo siyo ridhaa, ndiyo maana hutaweza kusikia wala kuona Makocha au wachezaji wetu wakizishtaki Timu zetu Fifa.
 
Mgunda aende South au Egypt akafundishe mpira
Lini uliona kocha wa Kitanzania anafundisha timu za nje? Hao ni wa hapahapa tu.

Twalib Hilal peke yake ndio amejichimbia Uarabuni tena na yeye ni Mwarabu.
 
Back
Top Bottom