simaye
JF-Expert Member
- Nov 5, 2010
- 426
- 214
Walimu wa Tanzania wanaweza kuwa ni watumishi pekee duniani kupewa nafasi ya mwisho katika malipo. Wapo baadhi ya watu wanajiaminisha kwamba mgomo wa mwalimu hauna athari yoyote kwa nchi. Nafikiri wenye mawazo ya aina hii wamepotoka sana kwa sababu utendaji usiokidhi viwango wa mwalimu una athari kubwa kwa Taifa kwa vizazi vingi vijavyo. Mwalimu asipotulia na kufanya kazi ya kufundisha kwa kufuata maadili mazuri na hasa anapoonekana kudharauliwa na serikali kwa kupewa mshahara mdogo kama ilivyo sasa atapata muda wapi wa kujianda kwa ajili ya kuandaa watumishi bora wa Taifa hili? Ndio maana leo hii watumishi wengi wanazalishwa na walimu hawana maadili kwa sababu walimu hawana muda wa kuwapika vyema bali wamebaki kufanya kazi kama kutimiza wajibu tu na watanzania tunachekelea na kuwakejeli kwa kila namna.Kwa nini wadau tusiwaunge mkono walimu ili waweze kulipwa vizuri sawa na kada nyingine za utumishi ili kuwapa morali nzuri ya kufanya kazi?